TANGA: Dereva wa OCD afariki akiwa kwenye msafara wa Naibu Waziri

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Dereva wa gari la Mkuu wa Polisi (OCD), wa Wilaya ya Pangani mkoani Tanga Koplo Nassoro amefariki katika mazingira ya kutatanisha wakati wa msafara wa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Juma Aweso.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba, alithibitisha na kusema tukio hilo lilitokea jioni katika kijiji cha Mwera, wilayani Pangani ambako Naibu Waziri huyo alikuwa Kijijini hapo akiwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya maji.

Kwa mujibu wa mashuhuda, dereva huyo alipoteza maisha baada ya msafara huo kufika Kijijini hapo na Naibu Waziri kufanya mkutano wa hadhara.

"Wakati Naibu Waziri akiendelea na shughuli zake dereva huyo alikuwa amekaa kwenye kiti chake akiwa ameinamia usukani, ilibainika kuwa amekufa alipoamshwa ili waendelee na msafara na kutoamka", alisema Hamza Jamari.

Gari alilokuwa akiliendesha Koplo Nassoro ndio lililokuwa likiongoza msafara huo na ndimo alimokuwamo OCD wa Pangani.

Wakulyamba alisema askari huyo alipatwa na umauti juzi majira ya saa 12 jioni na kwamba sababu za kitaalamu za kifo hicho ni kuugua ghafla.

Alisema jeshi la polisi limeshausafirisha mwili wa askari huyo kutoka Pangani kwenye Dar es salaam kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika baada ya kukamilika kwa shughuli za kifamilia

Naibu Waziri huyo wa Maji ambaye ameteuliwa hivi karibuni katika mabadiliko ya Baraza la mawaziri kushika wadhifa huo, yuko wilayani Pangani katika ziara yake ya kikazi ambapo pamoja na kukagua miradi ya maji alisisitiza kero za wananchi kwa mikutano ya hadhara.
 
Polisi huwa wana roho mbaya especilly hapa nchini. Wanakula rushwa mno jaman, tangulia kamanda tutakutana siku ya mwisho
 
R. I. P Kamanda..
Mawazo mengi + Muda mdogo wa kupumzika + Kutumikishwa ovyo hadi kwenda kinyume cha sheria +mshahara kuchelewa ukizingatia ana tegemezi wengi...

Nadhani hii haina tofauti na iliyotokea babati last week, askari kumtandika mkewe risasi akiwa maeneo ya lindo!!!!!!
 
Tunaambiwa tukeshe tukiomba maana hatujui siku wala saa!
Mungu akulaze mahala pema peponi koplo Nassoro
 
Back
Top Bottom