• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

TANGA: Dereva wa OCD afariki akiwa kwenye msafara wa Naibu Waziri

Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
20,278
Points
2,000
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
20,278 2,000
Dereva wa gari la Mkuu wa Polisi (OCD), wa Wilaya ya Pangani mkoani Tanga Koplo Nassoro amefariki katika mazingira ya kutatanisha wakati wa msafara wa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Juma Aweso.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba, alithibitisha na kusema tukio hilo lilitokea jioni katika kijiji cha Mwera, wilayani Pangani ambako Naibu Waziri huyo alikuwa Kijijini hapo akiwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya maji.

Kwa mujibu wa mashuhuda, dereva huyo alipoteza maisha baada ya msafara huo kufika Kijijini hapo na Naibu Waziri kufanya mkutano wa hadhara.

"Wakati Naibu Waziri akiendelea na shughuli zake dereva huyo alikuwa amekaa kwenye kiti chake akiwa ameinamia usukani, ilibainika kuwa amekufa alipoamshwa ili waendelee na msafara na kutoamka", alisema Hamza Jamari.

Gari alilokuwa akiliendesha Koplo Nassoro ndio lililokuwa likiongoza msafara huo na ndimo alimokuwamo OCD wa Pangani.

Wakulyamba alisema askari huyo alipatwa na umauti juzi majira ya saa 12 jioni na kwamba sababu za kitaalamu za kifo hicho ni kuugua ghafla.

Alisema jeshi la polisi limeshausafirisha mwili wa askari huyo kutoka Pangani kwenye Dar es salaam kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika baada ya kukamilika kwa shughuli za kifamilia

Naibu Waziri huyo wa Maji ambaye ameteuliwa hivi karibuni katika mabadiliko ya Baraza la mawaziri kushika wadhifa huo, yuko wilayani Pangani katika ziara yake ya kikazi ambapo pamoja na kukagua miradi ya maji alisisitiza kero za wananchi kwa mikutano ya hadhara.
 
jimmyfoxxgongo

jimmyfoxxgongo

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2013
Messages
5,279
Points
2,000
jimmyfoxxgongo

jimmyfoxxgongo

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2013
5,279 2,000
Tangulia polisi,

Mwenyezi Mungu akuru na mwanga wa milele akuangazie,

Huenda ni stress za home mwanae kakosa mkopo wa chuo huku anatumikishwa mwanzo mwisho
 
Steven Nguma

Steven Nguma

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2016
Messages
1,074
Points
2,000
Steven Nguma

Steven Nguma

JF-Expert Member
Joined Dec 6, 2016
1,074 2,000
Roho ya marehemu ipate pumziko la milele.wafiwa Mungu awape moyo wa subira ktk msiba huu mkubwa
 
Bacyclerbacy

Bacyclerbacy

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2016
Messages
1,647
Points
2,000
Bacyclerbacy

Bacyclerbacy

JF-Expert Member
Joined Sep 6, 2016
1,647 2,000
Inalilah wainailah rajiûn

Mwenyez Mungu awape subra familia ya Bro Nassor
 
KIDUDU

KIDUDU

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2012
Messages
2,523
Points
2,000
KIDUDU

KIDUDU

JF-Expert Member
Joined Sep 17, 2012
2,523 2,000
Polisi huwa wana roho mbaya especilly hapa nchini. Wanakula rushwa mno jaman, tangulia kamanda tutakutana siku ya mwisho
 
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
20,278
Points
2,000
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
20,278 2,000
Huenda ni stress za home mwanae kakosa mkopo wa chuo huku anatumikishwa mwanzo mwisho
Huenda ikawa hivyo haya maisha kila mmoja anasumbuliwa kivyake ijapokuwa hata kama siku yake imefika. Lakini kila kifo kina sababu zake
 
Joselela

Joselela

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Messages
4,045
Points
2,000
Joselela

Joselela

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2017
4,045 2,000
R. I. P Kamanda..
Mawazo mengi + Muda mdogo wa kupumzika + Kutumikishwa ovyo hadi kwenda kinyume cha sheria +mshahara kuchelewa ukizingatia ana tegemezi wengi...

Nadhani hii haina tofauti na iliyotokea babati last week, askari kumtandika mkewe risasi akiwa maeneo ya lindo!!!!!!
 
N

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Messages
27,910
Points
2,000
N

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined Aug 1, 2007
27,910 2,000
Tunaambiwa tukeshe tukiomba maana hatujui siku wala saa!
Mungu akulaze mahala pema peponi koplo Nassoro
 

Forum statistics

Threads 1,406,596
Members 532,389
Posts 34,520,665
Top