beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Zaidi ya asilimia thelathini na tatu ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza huko wilayani kilindi mkoani Tanga hawajaripoti shuleni mpaka sasa.
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wilayani humo Walda Maulidi wakati akiongea na wakuu wa idara pamoja na madiwani wa halmashauri ya wilaya Kilindi.
Amesema Pamoja na wanafunzi hao wa kidato cha kwanza kutokuripoti shuleni hadi kipindi hiki cha robo ya mwaka, lakini pia hata wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya ufundi kwa ufadhili wa Mfuko wa Kaya Maskini (TASAF) nao hakuna hata mmoja aliyeripoti kwenye vyuo hivyo huku ada za wanafunzi hao zikiwa zimeshalipwa.
Naelezwa kuwa inawezekana hali hiyo ikawa ni moja kati ya sababu zinazoshusha kiwango cha elimu wilayani kilindi hivyo serikali wilayani humo imehimiza wazazi nao wakatambua umuhimu wa elimu kwa familia yao.
Chanzo: ITV