Tanga: Anayedaiwa kuwa ni mgonjwa wa akili aua watu wawili kisha na yeye kuuawa na Wananchi

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Watu wawili wakazi wa kijiji cha Kilometa Saba, Kata ya Nkumba, Wilayani Muheza Mkoani Tanga wameuawa na mtu anayesadikiwa kuwa ni mgonjwa wa akili anayedaiwa kutoroka kwa Mganga wa Kienyeji

Tukio hilo limetokea juzi asubuhi na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe, aliyeeleza kuwa mtu huyo anadaiwa alikuwa kwenye matibabu kwa mganga wa kienyeji.

Alimtaja mtu hiyo aliyehusika na mauaji hayo kisha naye kuuawa na wananchi wenye hasira kali ni Juma Kuziwa.

Aidha, aliwataja waliouawa na mgonjwa huyo ni Omari Saidi Lugulu na Asha Mohamed, ambao ni wakazi wa kijiji cha Kilometa Saba.

Akielezea tukio hilo, alisema baada ya Kuziwa kufanya tukio hilo, wananchi wenye hasira kali walimvamia wakampiga hadi kufa.

Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kilometa Saba, Saidi Hasani, alisema alipelekwa kwa mganga wa kienyeji aliyejulikana kwa jina la Hamisi Kabweche ili kupatiwa tiba, lakini kwa bahati mbaya alitoroka.

Hassani alisema baada ya kutoroka alikutana na Asha Mohamed, na alimpiga fimbo sehemu ya kichwa na kupoteza fahamu na alipelekwa hospitali Teule Muheza mjini alifariki dunia.

Alisema mgonjwa huyo alikutana na Omari Lugulu ambaye nae

alimpiga kwa fimbo, na alianguka chini na kupoteza maisha yake papo hapo.

Alisema baada ya kumuua mtu wa pili, wananchi wenye hasira walimkamata wakampiga hadi alivyofariki.

Naye Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kilometa Saba, Rose Mdaki, walitoa taarifa polisi ambao walifika na kuchukua miili hiyo na kwamba mganga wa kienyeji alikimbilia kusikojulikana.

Diwani wa kata ya Nkumba, wilayani Muheza mkoani Tanga, Challes Mhilu, alisema kifo hicho kinasikitisha kwa kuwa wameuawa watu wasio na hatia, huku akiwataka wanafamilia kuwa watulivu wakati wa mazishi ya miili hiyo.

Katibu wa Chama cha Waganga wa Tiba Asili Wilaya ya Muheza, John Ngoda, alisema mganga huyo anafahamika kwenye chama hicho, lakini hajasajiliwa serikalini.
 
Huyu marehemu (aliyewaua wenzie) alikuwa collagemate na rafiki yangu wa karibu pia. R. I. P my friend Juma Abdallah.
 
Back
Top Bottom