Tanga amkeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanga amkeni

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by chema, Oct 12, 2010.

 1. c

  chema Member

  #1
  Oct 12, 2010
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanga ya Mjerumani, nimji wakizamani
  kavutiwa mkoloni ,kukaa hapa nchini
  wambali wamikoani,walikuja mashambani
  sikwambii viwandani,napirika bandarini
  unani tanga kunani,akuonae ni nani?

  Umaarufu mwambao,kwenye bahari yahindi
  umeandikwa ubao,kuwa siku hazigandi
  elimu ndio funguo,idai japo hupendi
  jamani muhimu ngao,ndio siri yaushindi
  unani tanga kunani,akuonae ni nani?

  Inakuponza imani ,nahiyo yako subira
  umeanikwa juani ,kwakuipenda hadhara
  Tanga umaskini,nahali wewe nibora
  amka upo vitani,kabla hujawa ngawira
  unani tanga kunani,akuonae ni nani?

  Umekuwa Tanga bora,kwakutaka yakokura
  nawe sifanye papara, ukaipata hasara
  bali uwape harara,natumbo lenye kuhara
  silaha yako nikura,mpe kiongozi bora
  unani tanga kunani,akuonae ni nani?

  Kashindwa kulinda maji,chura nachake kijicho
  amkeni wana mji,fungueni yenu macho
  sasa niwenu mtaji,mtapata mtakacho
  danganya kuitwa jiji, wacheza mwan jificho
  unani tanga kunani,akuonae ni nani?


  Watizame mikoani, watu naheshima zao
  wapewa kitu makini,kuridhi matakwa yao
  ajira za viwanadani,afya navingi vyuo
  wewe upo makwapani,wafanya lako hashuo
  unani tanga kunani,akuonae ni nani?

  Naongea kiswahili,nasio kiingereza
  fungua zako akili,wito kuutekeleza
  usijekuwa dhalili, wenzio watakubeza
  Kura yako ya awali,mazuri kutengeneza.
  unani tanga kunani,akuonae ni nani?
   
 2. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #2
  Oct 13, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  umejitahidi, ila watu humu JF wanataka hoja sio mashairi. kipindi hiki cha uchaguzi ndugu, sio rahisi mtu asome mashairi yako yote. nimejitahidi kuyasoma sijayamaliza. sikushauri uandike tena mashairi kwenye uchaguzi 2010.
   
 3. O

  Ogah JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kuna thread ilianzishwa ni mashairi kwa kwenda mbele................inapendeza sana.....Mods ikiwezekana hii iunganisheni na HII HAPA
   
Loading...