Tanga: Aliyemuua ndugu yake bila kukusudia ahukumiwa miaka mitatu jela

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,867
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tanga imemhukumu mkazi wa Kijiji cha Lunguza wilayani Lushoto, Jafari Kijangwa (45) kwenda jela miaka mitatu baada ya kukiri shitaka la kumuua ndugu yake Ibrahim Kijangwa bila kukusudia.

Hukumu hiyo ilitolewa leo Jumatano Februari 12, 2020 na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Amir Mruma kufuatia kuanza kwa shughuli za mahakama kwa mwaka wa sheria wa 2020.

Jaji Mruma amesema Jafari itabidi aende jela miaka mitatu ambapo licha kwamba hakukusudia lakini alifanya uzembe uliosababisha kifo cha ndugu yake.

“Hasira hasara na kama Jafar asingechukua hatua ya kumpiga ndugu yake kusingetokea kifo na katika hili jamii inapaswa kujifunza kwamba siyo kila jambo linatakiwa kutatuliwa kwa kipigo,” amesema Jaji Mruma.

Awali, ilidaiwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali, Rebeca Msalangi kuwa Mei 26 mwaka 2019 katika kijiji cha Lunguza kilichopo Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga mshtakiwa huyo alimshambulia Ibrahim baada ya kumwaga ndoo ya mafuta ya kukaangia chipsi.

Aliendelea kudai baada ya kumwaga mafuta hayo ukaanza ugomvi uliopelekea wawili hao kupigana na hatimaye Ibrahim alikufa.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom