Tanesco

Mulama

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
3,018
1,790
Hii tabia ya Tanesco kukata umeme na kurudisha watakavyo wao kama kwamba wanatugawia bure ni dharau sana na pia sio msingi wa kibiashara. Hivi hii tume ya ushindani na haki za mlaji haina mamlaka ya kuwawajibisha hawa Tanesco?

Watanzania tukatae hili, tutambue kwamba wao hawapati hasara yoyote kwakuwa bili zao zinabakia vilevile, wangekuwa wanakosa mapato kwa sababu ya kukata umeme wasingeendelea kufanya hivyo.

Kama vipi nguvu ya umma itumike kudai haki ya kutokatiwa umeme.
 
Kweli tunahtaji kubadilika....haya ndiyo mambo yanayowakera wananchi siyo mastori mengine ya wanasiasa!!!! hivi wana mageuzi ya ukweli hakuna kitu cha kufanya hapa kweli?siamini we have to start it somewhere!
 
Ni Tanzania pekee yenye tatizo la kukatika umeme, hata Rwanda ambapo wamepata amani ya kimagumashi lakini huduma muhimu za kijamii kama umeme ni uhakika kabisa. Ifike mahala tujue haki zetu na kuanza kuzidai si kila kitu tungojee mabadiliko ya kisiasa nchini
 
Kweli tunahtaji kubadilika....haya ndiyo mambo yanayowakera wananchi siyo mastori mengine ya wanasiasa!!!! hivi wana mageuzi ya ukweli hakuna kitu cha kufanya hapa kweli?siamini we have to start it somewhere!
Umeme bei ghali,
Na umeme wenyewe kwanza haupatikani wote. Watu wanateseka usiku joto sababu ya uzembe wa watu wachache tu, mgao sio mgao, wala shoti sio shoti, haueleweki eleweki.

Nyumba zinaibiwa usiku sababu usalama hakuna, pia watu wanakabwa mitaani yote sababu ya Giza!! Hakuna permanent solutions zaidi ya blah blah za kina Badra Masoud kila kukicha.

Tunahitaji strong commitment kwenye masuala muhimu kama haya, but Waziri Muongo yupo bize kupiga bei vitalu vya gesi pomoja na kulumbana na R. Mengi!!!
 
Watanzania tunapaswa kulaumiwa pia kwa sababu tumekalia porojo za kisiasa na matukio ya muda mfupi kama watu kutekwa na kuteswa nani kamfukuza nani kwenye chama na mambo mengine kama hayo, lakini kuna matatizo sugu hatuyapi kipaumbele kama maji umeme huduma za afya elimu nk.

Kama haya tungekuwa tunayapa wigo mpana katika kuyajadili tungekwisha pata ufumbuzi wa nini kifanyike kukomesha ujinga huu wa tanesco kwanza na ukawa mfano kwa watoa huduma za umma wengine
 
Jamani Tanesco Tanesco Tanesco! Huu ukatiri gani huu jamani??! Hivi kweli shilingi elfu kumi unapata unit tatu za umeme?? Enyi miungu watu mnajiweka kwenye daraja la usahaulifu kwamba watanzania wenzenu ni hoehae milo miwili kuimudu kwa mbinde achilia mbali kununua matibabu tena kwenye hospitali za serikali, leo mnawanyima hata haki ya kupata mwanga!!?

Hakika Mungu wa kweli Bwana wa Majeshi atawajibu, iko siku mnyonge atapewa haki yake.
 
''Symbion, IPTL, SONGAS na Agreco kila moja analipwa kiasi cha Tsh milioni 152 kwa siku'' huu ni wizi wa hali ya juu ambao umehalalishwa na rais mwizi Watanzania amkeni.
 
''Symbion, IPTL, SONGAS na Agreco kila moja analipwa kiasi cha Tsh milioni 152 kwa siku'' huu ni wizi wa hali ya juu ambao umehalalishwa na rais mwizi Watanzania amkeni.

Mkuu hawataki tuamke, wanatupiga upofu kwa kutuweka gizani kama hivi!
Inasikitisha kuona bado kuna watanzania wanashabikia chama hiki cha matatizo!!
 
Baada ya kuhomola mapesa yetu walala hoi kwa ghalama mpya za umeme, Tanesco yatutunuku giza totorooo masaa maane sasa giza limetanda mujini!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom