TANESCO yazitaja taasisi za Serikali kama changamoto kulipa bili

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,872
Katika Mpango Mkakati wa TANESCO 2020 hadi 2025 wamezitaja taasisi za Serikali kuwa ni changamoto ya kwanza kwa kuwa huwa hawalipi bili zao kwa wakati.

Changamoto nyingine ni watu kutumia vyanzo vingine vya nishati ya umeme kwa kuwa TANESCO hawana uthabiti wa huduma, hali ambayo inaathiri mapato ya TANESCO.

Uharibifu wa miundombinu, gharama na ushindani katika matumizi ya maji pia vimetajwa kama changamoto.
 
Electronic Government Agency(eGA) of Tanzania wanazo software kama hizi, sijui tanesco wanafeli wapi aisee mpaka kwenda india
DAE2265E-CDF9-4EB5-BCA9-432DBFA1A528.png
 
Ni kweli kabisa..

Sababu hata wao Tanesco huo hawalipagi bill zao za umeme, na pia hua hawawalipagi Dawasco bill za maji...
 
Katika Mpango Mkakati wa TANESCO 2020 hadi 2025 wamezitaja taasisi za Serikali kuwa ni changamoto ya kwanza kwa kuwa huwa hawalipi bili zao kwa wakati.

Changamoto nyingine ni watu kutumia vyanzo vingine vya nishati ya umeme kwa kuwa TANESCO hawana uthabiti wa huduma, hali ambayo inaathiri mapato ya TANESCO.

Uharibifu wa miundombinu, gharama na ushindani katika matumizi ya maji pia vimetajwa kama changamoto.
Wasitafute mchawi kwenye "saga" hili la mgao wa umeme!

Tangu enzi za Nyerere, taasisi za umma kama jeshi na wengineo huwa hawalipi na hawakatiwi.

Sababu za kutolipa wanadai hawapewi mafungu yao toka hazina kama bajeti zao walizoidhinishiwa.

Sasa taasisi hizo za kiserikali si chanzo cha upungufu wala mgao unaoendelaea hivi sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika Mpango Mkakati wa TANESCO 2020 hadi 2025 wamezitaja taasisi za Serikali kuwa ni changamoto ya kwanza kwa kuwa huwa hawalipi bili zao kwa wakati.

Changamoto nyingine ni watu kutumia vyanzo vingine vya nishati ya umeme kwa kuwa TANESCO hawana uthabiti wa huduma, hali ambayo inaathiri mapato ya TANESCO.

Uharibifu wa miundombinu, gharama na ushindani katika matumizi ya maji pia vimetajwa kama changamoto.
Njia ya kukabili wasio lipa bill ni kuwawekea mita za lulu. Kambi za jeshi mita ziwekwe km 1 nje. Matumizi ya vyanzo mbadala ni nafuu kwao, Tanesco hawajawahi kukidhi mahitaji ya umeme, na haina uhakika, ni giza mara moja.
 
Back
Top Bottom