Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,426
- 7,736
TANESCO katika mpango mkakati wake wa miaka mitano imesema pamoja na kupungua utegemezi wa matumizi ya mafuta mazito kuzalishia umeme, gesi nayo majanga. Gharama ya kufikisha gesi kwenye vituo vya kuzalishia umeme kutoka inapochimbwa inabakisha gharama ya uzalishaji wa umeme kuendelea kuwa juu.
Kati ya mwaka 2015 mpaka 2019 megawats 320 ziliondolewa kwenye gridi ya Taifa kutoka kwenye makampuni binafsi ya Aggreko(100MW), Symbion (120MW), IPTL(100MW) na umeme kutoka nje ya nchi mojawapo ya sababu ikiwa kupunguza gharama ya uendeshaji TANESCO.
Mpango kazi wa TANESCO ukaitaka TANESCO kuendelea kuwekeza kwenye vyanzo nafuu kama mbadala wa vyanzo vya gharama.
Hii ni sababu ya awamu ya tano kuamua kwenda Rufiji badala ya kujikita Kinyerezi?