TANESCO yatoa siku 14 kwa wadaiwa wote kulipa madeni yao ya bilioni 275 ikiwemo Zanzibar

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Shirika la umeme Tanzania(TANESCO) limetoa siku 14 kwa wadaiwa sugu kuhakikisha wanalipa madeni yao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kaimu mkurugenzi wa Shirika hilo, Tito Mwinuka amesema mpaka sasa wanadai bilioni 275.

Amesema notisi hiyo ni kwa wateja wote wakubwa na wadogo na kwamba wasipolipa watakatiwa umeme ikiwamo shirika la Umeme Zanzibar(ZECO)

=======

Zanzibar kukatiwa umeme baada ya siku 14

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa siku 14 kwa Shirika la Visiwani Zanzibar (ZECO) kulipa deni lote la ankara za umeme wanalodaiwa na endapo halitafanya hivyo basi hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kukatiwa umeme.

ZECO%20.jpg

Kauli hiyo imetolewa leo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Dkt. Tito Mwinuka alipokuwa anaongea na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam ambapo amesema hadi kufikia mwezi Januari mwaka 2017, Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) lilikuwa linadaiwa zaidi ya shilingi bilioni 127.8.

“Shirika la umeme linashindwa kutekeleza majukumu yake mbalimbali kwa wakati ikiwemo uendeshaji wa shirika, matengenezo ya miundombinu pamoja na utekelezaji wa miradi, hayo yote yanasababishwa na malimbikizo ya madeni kwa wadaiwa sugu hivyo tunatoa siku 14, wasipoweza kulipa tutawakatia huduma ya umeme”. Alisema Dkt Mwinuka

Mwinuka.png

Dkt Tito Mwinuka - Kaimu Mkurugenzi wa TANESCO

Aidha mbali na ZECO, Tanesco imewataja wadaiwa sugu wengine ikihusisha Wizara na Taasisi za serikali zikiwa zinadaiwa zaidi ya bilioni 52.5, makampuni binafsi pamoja na wateja wadogo wanaodaiwa zaidi ya bilioni 94.9

Kwa upande mwingine Dkt. Mwinuka amesema shirika hilo linatarajia kuanza oparesheni maalum ya kukusanya madeni hayo na matarajio yao ni kulipwa kwa malikimbizo yote ili yalisaidie kujiendesha kiushandani na kwa ufanisi mkubwa zaidi na kuchochea kasi ya ukuaji sekta mbalimbali zinazotegema nishati ya umeme nchini.

Hatua hii imekuja ikiwa ni takriban siku 4 tangu Rais Magufuli kuagiza TANESCO kufuatilia madeni yote ikiwemo deni ambalo TANESCO inalidai ZECO, na kuitaka kuwakatia umeme wote watakaoshindwa kulipa kwa wakati.

Chanzo: EATV
 
Habari jf
Niona habari kuwa shirika la Umeme Tanganyika ikiidai shirika la Umeme zanz na kuipa siku kumi na NNE vinginevyo itawakatia Umeme ,kumbe mnatumia Umeme kisha hamlipi haya sasa kama mmezoea vya dezo ndio hivyo mlipe deni
 
Shirika la umeme Tanzania(TANESCO) limetoa siku 14 kwa wadaiwa sugu kuhakikisha wanalipa madeni yao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kaimu mkurugenzi wa Shirika hilo, Tito Mwinuka amesema mpaka sasa wanadai bilioni 275.

Amesema notisi hiyo ni kwa wateja wote wakubwa na wadogo na kwamba wasipolipa watakatiwa umeme ikiwamo shirika la Umeme Zanzibar(ZECO)

Mwananchi
Safi TANESCO, bilioni 275 ni pesa nyingi sana msiziache zikapotea kizembe zembe
Ova
 
Awamu hii sio ya mazoea, walipe tu,,, gas na mafuta vyote viw vya kwenu halafu mtake tuwahudumie!?? U can't be seriuos
 
Hamna lolote, Zanzibar wanavodekezwa na Jamhuri ya muungano utafkiri bila znz hakutakua na tanganyika. Notice hiyo haitekelezeki, bure kabisa
 
Kwa upande mwingine Dkt. Mwinuka amesema shirika hilo linatarajia kuanza oparesheni maalum ya kukusanya madeni hayo na matarajio yao ni kulipwa kwa malikimbizo yote ili yalisaidie kujiendesha kiushandani na kwa ufanisi mkubwa zaidi na kuchochea kasi ya ukuaji sekta mbalimbali zinazotegema nishati ya umeme nchini.
Sijaelewa kabisa hapo.
 
Good, lazima kuheshimu agizo la Rais wa Muungano. Zanzibar jeuri sana kwa nini umeme usikatwe leo? Zanzibar mkome, Tanganyika mungu wenu.
 
_95051455_3948d5f0-bf83-44bb-b251-d3bc2fc08f7a.jpg

Shirika la umeme nchini Tanzania (Tanesco) limewapa muda wa siku 14 wale walio na madeni la sivyo wakatiwe umeme.

Mkurugenzi mkuu wa Tanesco Tito Mwinuka, aliuambia mkutano wa waandisi wa waandishi wa habari mjini Dar es Salaam kuwa, wizara na mashirika mengine ya serikali yanadaiwa deni la dola milioni 2.3 huku shirika la umeme la Zanzibar (Zeco) likidaiwa dola milioni 56.8.

Chanzo: BBC SWAHILI
 
Vibaya hivyo hamlipi mpaka mkatiwe? lipeni tujenge viwanda jamani. :D
 
Hamna lolote, Zanzibar wanavodekezwa na Jamhuri ya muungano utafkiri bila znz hakutakua na tanganyika. Notice hiyo haitekelezeki, bure kabisa
Zanzibar eneo muhimu la kimkakati wa ulinzi na usalama hatuwezi kuwaacha waende litakuwa kosa kubwa sana
 
Zanzibar eneo muhimu la kimkakati wa ulinzi na usalama hatuwezi kuwaacha waende litakuwa kosa kubwa sana
Kivipi mkuu vita ya mwaka 1970 ndo unataka kujenga hoja siku hizi unapigwa mtu anachezea papuchi mkuu!!
 
Back
Top Bottom