TANESCO yatoa “hongo” kwenye mitandao ya kijamii ili “isishambuliwe”?

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,975
Katika kupambana na kile kinachoonekana kwa uongozi wa juu wa TANESCO kuwa ni taswira hasi(negative image), Uongozi wa TANESCO umewalipa pesa wanaoitwa “washawishi wa kwenye mitandao ya kijamii(social networks influencer)” ili waisaidie katika kubadilisha taswira na kuwa taswira chanya kwenye jamii.

Kwa sasa ukiingia kwenye mitandao ya kijamii kama twitter, facebook na clubhouse utakuta jumbe mbalimbali za kuisifia TANESCO katika utendaji kazi kutoka kwa washawishi “wakubwa” katika mitandao nchini.

Kwa sasa, wale wale ambao walikuwa wanalalamika sana kuhusu huduma mbovu za TANESCO na “kumzodoa” Waziri wa Nishati, January Makamba kwa sasa wanaimba tena “mapambio” ya kuipongeza TANESCO na Waziri Makamba.

Kuna msemo usemao, “Penye udhia penyeza rupia". January Makamba amepenyeza rupia ili kuondoa udhia!

Inashangaza kuona TANESCO wanatumia pesa nyingi za serikali/wananchi kuwalipa washawishi wa kwenye mitandao ili wawasafishe kwa propaganda wakati wananchi wengi wanachohitaji ni umeme wa uhakika na pia kuunganishiwa umeme kwa haraka.

Waziri wa Nishati, January Makamba na bodi yake ya TANESCO wanadhani propaganda zitaondoa tatizo la msingi la TANESCO.

Baada ya kuteuliwa na kuapishwa, Waziri Makamba alitoa matamko mbali mbali kuhusu tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara lakini imeanza kugundulika kuwa baadhi ya matamko hayo hayakuwa na ukweli.

Baadhi ya wabunge ambao wanaunda kamati ya kudumu ya bunge ya Nishati na Madini wameanza kuhoji kuhusu kauli zake huku kamati ikimtaka awasilishe bungeni maintanence schudule kuonyesha jinsi ambavyo mitambo haikufanyiwa service kwa miaka 5 mfululizo kama alivyodai.

Kwa yanayoendelea kwa sasa, kuna uwezekano mkubwa kwa TANESCO kupenyeza pia rupia kwa wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini kama ilivyofanya kwa “washawishi wa kwenye mitandao ya kijamii(social networks influencer)” ili iwanyamazishe!
 
Mimi huwa sipendi kushiriki katika madai yasiyokuwa na ushahidi. Mleta mada jazia nyama kwenye hoja yako kwa kutoa ushahidi wa madai yako.

Bila ushahidi itakuwa yale yale ya kumpa mbwa majina mabaya ili ukimuua upate justification.

Bila ushahidi JF tutakuwa kijiwe cha uzushi na majungu.

Napenda whistleblowers lakini wa back up madai yao kwa ushahidi.
 
naona mnamkomalia Makamba balaa..

Kijana ana miezi 4 kazini, unafikiri anaweza kufanya miujiza kwenye shirika lililooza tangu uhuru.. Hakuna siku Tanesco iliwahi kuwa na ufanisi, TUKIACHA UNAFIKI KUNA SIKU TUNAWEZA KUELEWANA..

Kijana amesema ukweli, mitambo ilikuwa haifanyiwi matengenezo, kifupi ulikuwa mtego wahusika wakiamini stieggler itakuwa tayari inarun hivyo wangekuwa safe, bahati mbaya jumba bovu limeangukia mtaa mwingine..
 
Hii nchi pambana na hali yako.... ukitaka kujua rangi za watu halisi subiri imwagwe pesa, utashangaa unavyobaki peke yako.

Hukuona vijana wa CHADEMA walivyomshabikia Edward Hoseah kwenye uchaguzi wa TLS....
 
Dah.....Tanesco ndiyo shirika lenye tija nchi hii.....linaongoza kwa kuipatia serikali mapato.....na tangu liwe chini ya waziri mchapakazi na mwenye maono ya kweli...mh JYM... 90% ya bajeti ya serikali inabebwa na Tanesco🤭
Welp!

Kama hilo shirika ndiyo lenye tija nchi hii basi ndo maana tupo kwenye hali tuliyonayo kama nchi/ taifa.
 
Tanesco ni shirika la kupiga bei tu .. maana hata haieleweki wanamkomoa nani kwa maslahi gani
 
Miaka yote hii nchi umeme haujawahi kuwa stable, na ukweli ni uleule, miundombinu ya umeme ni mibovu.

Bila kurekebisha hii miundombinu mibovu tutakuwa kila siku tunatafuta mchawi. Tatizo lingine ni kukosa backup ya mitambo ya kuzarisha umeme incase unapiga down mtambo mmoja au miwili kwa ajili ya planned maintenance au hata kukitokea breakdown..

Leo hii hizo hydro plant zote zikipigwa na radi zikaungua maana yake nchi nzima inakuwa kizani, au ukipull out mtambo mmoja say Mtera tayari grid inakuwa haina zaidi ya 100MW...
 
Back
Top Bottom