TANESCO yatangaza mgawo wa umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANESCO yatangaza mgawo wa umeme

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Josh Michael, Oct 4, 2009.

 1. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  • Siasa zaliumiza taifa, Zitto akumbukwa
  na Mwandishi Wetu

  HATIMAYE Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza mgawo wa umeme nchi nzima kutokana na upungufu wa maji kwenye vituo vya kuzalisha umeme vya Kihansi na Pangani.

  Hatua hiyo ya TANESCO imekuja miezi michache tu baada ya Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Dk. Idris Rashid, kuonya kuwa taifa litaingia gizani iwapo mitambo ya Kampuni ya Dowans yenye uwezo wa kuzalisha megawati 100 haitanunuliwa.

  TANESCO ilikuwa na mpango wa kununua mitambo ya Dowans ambayo ilirithi mkataba kutoka Kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond iliyobainika kutokuwa na uwezo wa kuzalisha nishati hiyo.

  Dhamira hiyo ya shirika hilo ilikumbana na upinzani mkali kutoka kwa wanasiasa mbalimbali, hususan Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyo chini ya Mbunge wa Bumbuli, William Shellukindo, ambaye alisema kuinunua mitambo hiyo ni kukiuka sheria ya manunuzi ya umma pamoja na kukiuka maagizo ya Bunge.

  Kutokana na upinzani huo, TANESCO ililazimika kuondoa mpango wake huo huku Dk. Idris akionya kuwa kuna kila dalili kuanzia Septemba mwaka huu taifa likakabiliwa na mgawo wa umeme kama ule wa mwaka 2006.

  Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa TANESCO, Dk. Idris Rashid, imesema kumekuwapo na upungufu wa uzalishaji wa umeme kwenye gridi ya taifa, ambao kwa kiasi kikubwa umesababishwa na uhaba wa maji katika vituo vya Kihansi na Pangani, kutokana na ukame katika kipindi hiki cha kiangazi.

  Sababu nyingine iliyotolewa na shirika hilo ni kuharibika kwa mtambo wa Songas UGT1 (20 MW), kuharibika kwa mtambo wa Kihansi (60 MW) na kuharibika kwa mtambo wa Hale (8 MW).

  Dk. Rashid amesema athari za upungufu huo zimelisababishia shirika kufanya mgawo wa 65MW kwa maeneo mbalimbali kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa tano usiku.

  Aidha, amesema ili kukabiliana na tatizo hilo, TANESCO inajitahidi kukamilisha ujenzi wa mtambo mpya wa Tegeta 45 MW ili ikiwezekana uanze kazi mwezi ujao na kuharakisha matengenezo ya mtambo wa Songas unit 1 (20 MW) kabla ya mwisho wa mwezi huu.

  Jitihada nyingine zinazofanywa na shirika hilo ni kuharakisha matengenezo ya mtambo wa Kihansi unit 1 (60 MW) ili yaweze kukamilika katikati ya mwezi Desemba mwaka huu.

  Aidha, Dk. Rashid alisema katika kipindi hicho cha magwo wanatarajia mvua za vuli zitaanza kunyesha mwezi ujao, hali itakayosaidia kuboresha hali ya uzalishaji umeme kwa kutumia maji.

  Aliongeza kuwa, pamoja na sababu hizo, TANESCO itaendelea kushirikiana na serikali kuanza maandalizi ya ununuzi wa mitambo mingine ya kuzalisha umeme ili kukidhi mahitaji ya umeme kwa mwaka ujao na siku za baadaye.

  Hatua hii ya TANESCO kutangaza mgawo wa saa 12 itaathiri shughuli mbalimbali kwa wananchi pamoja na uchumi, ambao katika siku za hivi karibuni umekuwa katika mdororo.
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa nini tusione kuwa huu ni uzembe wa tanesco? Walishajua kuwa kutakuwa na hali kama hii, kwa nini hawakuchukua tahadhari? Mimi naamini wameacha kuchukua tahadhari makusudi ili siasa zao zionekane kuwa ni za kweli
   
 3. n

  nyakyegi Member

  #3
  Oct 4, 2009
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  As usual ''management by crisis''
   
 4. DALA

  DALA JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 874
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 80
  Nchi hii kila mmoja anataka kila akisemacho kifanyiwe kazi isipofanyiwa kazi basi adhabu inatupwa kwa wananchi walipa kodi! Kwanini Tanesco wameshindwa kujiwekea mikakati ya kuhakikisha kwamba umeme unapatikana bila tatizo? Umeme wenyewe unawafikia watu sio zaidi ya milioni 10 tu alafu wanashindwa sasa nchi mzima itapata umeme mwaka gani! Huu ni uzembe wa hali ya juu na hatuwezi kukubali! tanesco wafanye kazi sio siasa!
   
 5. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #5
  Oct 4, 2009
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  Duh,

  Ndo maana tangu juzi umeme hatupati? Kazi kwelikweli. Hapa nilipo tayari ushakatika
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160


  Hayo maandalizi yalisubiri mashine zinaharibike na maji yakosekane si ndio? Au wenye meno wanaona uchaguzi umekaribia, na bingo yao haijatimia?

  Inakuwa vigumu sana kuelewa pale kampuni ya kuuza umeme inaposhindwa kuuza umeme. Inasikitisha kuwa ni only in Tz kuwa unaweza kuwa demand ya bidhaa muhimu kabisa kama umeme ipo, lakini hakuna service provider wa maana. Inashangaza, na watu wanafanya kazi kwenye hii kampuni na kila siku wanaamka asubuhi 'kwenda kazini'..lol

   
 7. s

  shabanimzungu Senior Member

  #7
  Oct 4, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  these bureacrats are fools....these people cannot even agree on how to sort TANESCO........tz bongo people are just gulliblke and blackmailed by TANESCO....................In any other contryt here would be riots..
   
 8. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ni yale yale yanaongelewa kila mwaka. Inaelekea hao huko TANESCO hawawezi kazi. Wawajibishwe na apewe mtu mwingine hii kazi. Sio kila mwaka tunakabiliwa na tatizo lile lile tu! Analilia Dowans, kwani wana share huko Dowans? Kweli umaskini wa fikra unatumaliza!!!
   
 9. O

  Ogah JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Piga chini Waziri na uongozi wote wa Tanesco..........damn!
   
 10. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mimi nashindwa kujua hivi sisi tuna wadudu gani kichwani kwetu?? Hivi baada ya haya madudu yote mpaka serikali kujiuzulu mpk leo kuna matatizo ya umeme?? Jamani ndugu zangu Taifa letu nani anweza kufanya kweli kwa ajili ya kizazi hiki, inatia uchungu sana
   
 11. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #11
  Oct 4, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ndugu unapozungumzia kuwa huu ni uzembe wa Tanesco angalia vizuri usije kuwa hujui unachokiongelea. Wewe na wenzio waliotangulia nadhani hamjafanyia uchunguzi yakinifu nini kizuizi au tatizo la tanesco.

  Let me give some few details. Nilisomaga raia mwema last week kuhusu crisis ya Dk Idris na mabosi wake nikagundua Tanesco ina matatizo makuu matatu.
  a. Uongozi mbovu wa wakurugenzi ambao wamekalia bodi kwa ajili ya matumbo yao na sio umma. Wewe umesikia wapi Chairman wa bodi eti anapewa nyumba ofisi na gari la shirika (This is non-sense kabisa!!!) kwasababu kwanza yeye ni chairman wa bodi ya shirika la umma amewekeza kiasi gani ndani ya Tanesco???? Pili hata kama amewekeza kiasi mambo ya shirika la umma na shughuli zake binafsi haviendani hata kidogo hii ni ubadhirifu wa pesa za umma na hili ni tatizo.

  b. Dk Idrisa aliwaagiza watu wakakate umeme Tanga Cement kwasababu walikuwa wadaiwa sugu (To me this was right kabisa) akatoka bosi mmoja serikali akaandika kimemo eti warudishiwe umeme kwakuwa ni watu muhimu (This is again is non-sense kabisa!!!) kwasababu kama mteja ni mdaiwa sugu utamuachia vp aendeleee kukuumiza. Chukulieni mfano nyie mnafanya biashara zenu binafsi halafu watu kila siku wanakopa kulipa hawalipi unategemea biashara itakuwa????.

  c. Tanesco ina majengo kibao inayo dar ambayo yanaweza kuwa ni mtaji wa tanesco kujikwamua kipesa but uliza ni kina nani wanakaa katika majengo hayo zaidi ya mashirika ya serikali na wizara zao unategemea kweli tanesco itapata wapi pesa za kujiendesha????

  d. Mikataba mibovu ya richmond, IPTL ambayo imeingiza shirika hasara ya mamilioni unadhani Tanesco itaenda mbele.

  Binafsi hakuna mmoja wetu hata leo akipewa uongozi pale Tanesco anaweza kufanya maajabu. Haya haya yanayoiua Tanesco ndio yameuia NBC, Benki ya nyumba (THB) etc ambazo viongozi na wasaidizi wake wanaabuse their powers. Isitoshe serikali yenyewe impliedly inaua hayo mashirika unadhani Tanesco ingelikuwa chini ya mtu binafsi hivi vingelitokea sidhani!!!. Ndio matunda hayo jamani tuvumilie tu badala kunyoosha kidole kimoja Tanesco vengine vinne vinatuangalia sie!!!!
   
 12. M

  Magezi JF-Expert Member

  #12
  Oct 4, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kweli kwa mtu mwenye akili ukijiuliza unashindwa kuelewa. Ni nini kinatendeka pale tanesco, miaka yote wapo wahandisi, wanansheria, mameneja, mafundi wazuri tu lakini ni aibu tupu.

  Lakini chanzo cha yote ni serikali kuingilia maamuza ya menejimenti za tanesco kwa muda mrefu. Kesi ya IPTL ni serikali, richmond ni serikali, songas japo wanajikongoja lakini ni serikali kwa hiyo ni lazima tufike mahali siasa ikae pembeni.

  Mimi kila mara namuuliza ngeleja, ni kwa nini asitangaze wafanyabiashara/makampuni makubwa yaje yawekeze mitambo yao ya kuzalisha na kusambaza umeme wenyewe na walipe kodi kama ktk biashara nyingine!!! Lakini ni kimya tu, oh... mara tunamikakati...oh mara tuna mgao utakuwa historia......na upuuzi mwingine mwingi.

  Hata kama hii ni justification ya kununua mitambo ya Dowans, still siyo suluhisho la matatizo ya umeme tanzania. Niliwahi kutoa mfano kwamba mtu/kampuni inaweza ikapewa wilaya au hata mkoa mzima izalishe na isambaze umeme na kukusanya mapato kutoka kwa watumiaji, then ilipe kodi serikalini. Sijui viongozi wa serikali wana nini kichwani, alafu mtu anakurupuka anasema Ngeleja ni waziri kijana?? kijana gani hana vision??
   
 13. M

  Magezi JF-Expert Member

  #13
  Oct 4, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hapo bado hujaeleza chochote in details kama ulivyo tanguliza. Watanzania wengi wanajua hayo uliyo yaeleza na yote yana fall kwenye uzembe wa mamagement ya tanesco hata kama inaingiliwa na serikali/mafisadi. Wote ni wazembe na wezi tu tanesco na serikali yao.
   
 14. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #14
  Oct 4, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Sheria ya Umeme ya mwaka 2007 (tuliipitisha bungeni 2008) inaruhusu makampuni ya binafsi kuzalisha umeme na kusambaza umeme (upande wa kuzalisha tayari IPTL na Songas wanashiriki).

  Tatizo la umeme wa Tanzania ni Transmission. Uwezo wetu wa kusambaza umeme ni mdogo sana na tuna gridi moja tu. Uwekezaji katika gridi hauwezi kuwa kwa sekta binafsi (serikali ilitika kuliberalise transmission pia, nakumbuka mimi na mzee cheyo tulikataa kata kata na tukafanikiwa). Serikali ilipaswa kuwa imejenga gridi mpya ya North-West gridi ili kusafirisha umeme kwenda kanda ya Ziwa mikoa ya Kigoma, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Kagera na Mara. Mahitaji ya umeme wa mikoa hii kwa sasa kama migodi yote ikipata umeme wa gridi ni 240MW. Kwa sasa ni mgodi mmoja tu wa Bulyanhulu ndio unapata umeme wa gridi na usio na uhakika. Hii inapelekea serikali kupaata hasara mbili.
  1. TANESCO wanakosa soko la uhakika la zaidi ya 120 MW ambapo wangeweza kuingiza zaidi ya 120bn usd kwa mwaka na hivyo kupata fedha za kusambaza umeme vijijini na mijini. Pia hii inakosesha uchumi faida ya backward linkages kati ya sekta ya nishati na sekta ya madini (backward linkage is such that a sector that gets a lot of inputs from within the country will have strong backward linkages relative to sectors that import most of their inputs from oversees). Madhara haya tunayaona hapa chini kwenye hasara ya pili;
  2. Serikali inatoa misamaha ya kodi ya mafuta kwa kampuni za madini ili zizalishe umeme wake wenyewe (importing inputs). Kwa mujibu wa ripoti ya Bomani Tanzania ilisamehe jumla ya 191bn Tshs katika kipindi cha 2005/06 - 2007/08. Hii pia ina madhara katika urari wa biashara na hata thamani ya shilingi ya Tanzania pale uzalishaji unapokuwa unaongezeka katika sekta ya madini.
  Uwekezaji wa transmission line ni uwekezaji mkubwa sana lakini unawezekana. Zinahitajika kama 700m usd kujenga grid hii mpya. Hapa serikali ndipo inapotakiwa kufanya kazi sawasawa.

  Lakini kuna hatua za dharura zilizotakiwa kufanywa. Mojawapo ni kuwa na mtambo wa 60MW Mwanza ambao utapunguza mzigo kwenye gridi. Zabuni zilitangazwa na TANESCO toka mwezi Aprili na wazabuni kujitokeza lakini mtambo huu utaweza kufungwa na kuanza kazi mwaka 2011. Hii inatokana na taratibu za ujenzi wa mitambo kwenye viwanda. Baada ya kupata mzabuni, itabidi kuanza sasa ujenzi wa mitambo nk.

  Kwa mwono wangu, matatizo ya sasa ya mgawo hayatachukua muda mrefu sana kwani mvua zitanyesha na mitambo kurekebishwa. Hata hivyo bado tutakuwa na tatizo kubwa la kanda ya Ziwa maana hata mabwawa yazalishe at 100%, kama gridi imezidiwa haitaweza kusafirisha umeme kwenda huko. Mtambo wa 60MW Mwanza ndipo unapopata umuhimu wake kwa sasa.

  Kuwalaumu TANESCO sidhani kama ni sawa. Hili ni Shirika ambalo limeharibiwa sana na mikataba mibovu ambayo sio TANESCO wenyewe waliingia. Hili ni Shirika ambalo NetGroup Solution waliliingiza kaburini na ndio kwanza limetoka.

  TANESCO wamejitahidi sana kwa kadiri ya uwezo wao kushugulikia suala hili kwani wao wenyewe wanajua kuwa wanapaswa kufanya kazi kwa bidii kwani wanatakiwa kubreak even mwaka 2010 ili waweze kuanza kulipa mkopo waliochukua katika taasisi za fedha. Hivyo migawo hii inawaumiza na ninajua wanaumia.

  Tatizo ni commitment ya serikali katika suala hili. TANESCO waliomba 312bn kwenye bajeti ili kushughulikia masuala haya ya umeme hawakupewa kitu. Tuzingatie kuwa tuna nakisi ya 155MW za umeme kutokana na IPTL kusimama kuzalisha mpaka kesi iishe na kesi bado haijaisha.

  Suala la umeme lapaswa kuangaliwa katika mapana sana. Ni kweli kuwa asilimia 12 tu ya nyumba ndio zina umeme, lakini umeme sio kwa jili ya kuwasha nyumbani tu. Umeme kwenye uzalishaji wa uchumi ni muhimu sana ili walaji wa kawaida waweze kufidiwa kwa kupata umeme wa gharama nafuu.

  Ninaamini kabisa kuwa kama tukiamua kuisaidia TANESCO tunaweza kulifanya Shirika hili 'champion' wa nchi yetu. Potential zote zipo. Dhamira hakuna.
   
 15. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #15
  Oct 4, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Vile vile Management in crisis
   
 16. M

  Magezi JF-Expert Member

  #16
  Oct 4, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nashukuru sana Zitto kwa mchango wako ambao ume-summarize mengi ambayo tumeandika hapo juu lakini mimi naomba maelezo kidogo, hivi zile pesa za vitambulisho vya taifa (UD$200m approx.) kama zikiwekwa huko tanesco haziwezi kusaidia kitu?? Kwa nini law makers wetu hamlioni/hamkuliona hilo mpaka sasa tunaanza kuumizana?

  Serikali ingeanza kujenga hiyo gridi kwa interval...kila mwaka kipande mpaka leo si ingekuwa tayari?? Mbona nyumba tunajenga hado hado na zina isha?? Kama ulivyosema Zitto, we have all the resources we need problem ni dhamira hakuna.
   
 17. c

  care4all Senior Member

  #17
  Oct 4, 2009
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wabongo bwana wanapenda kupindisha kila kitu ili ionekane kuwa kuna uzembe au ilipangwa... hapa Tanesco wametoa taa**** ya kiufundi na time frame za kufix hilo tatizo....kama mitambo inafanya kazi 24hrs bila kupumzishwa hutegemei kuwa kuna siku itaharibika? tulitakiwa tumewe na mitambo ya ziada (standby)....lakini siku hizi wabongo suala la kiuhandisi au ufundi wanaweka siasa..watu wanavamia taaluma za watu...
   
 18. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #18
  Oct 4, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Sio kwamba fedha za vitambulisho zipo zimekaa zinasubiri mradi. Hapana. Nadhani unafahamu kuwa kuwa mradi unapangwa kisha fedha zinatafutwa - ama kupitia TRA au misaada kutoka nje. Hivi sana hakuna fedha hizo za vitambulisho vya Taifa. Isipokuwa mradi unatarajiwa kugharamia 200bn.

  Ni kweli tunaweza kujenga gridi kidogo kidogo. Tatizo kubwa Tanzania ndugu yangu ni, je tunajua matatizo yetu? Je tunajua kipi kianze na kipi kifuate? (prioritization and sequencing). Mimi nadhani, hisia zangu tu, viongozi na hata wananchi wenyewe hatujui kwa kina matatizo yetu na kipi kianze. Tena katika eneo la nishati - ukiachana na kelele zetu za mikataba - watu wachache sana wanajua kwa undani kabisa changamoto tulizonazo katika nishati na mahusiano yake na sekta nyigine za uchumi.

  Lakini tutajua tu, tunakua!
   
 19. M

  Magezi JF-Expert Member

  #19
  Oct 4, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Tunacho hoji siyo yanayotokea leo..... ni uzembe wa muda mrefu. Wewe kama unafikiri unaelewa zaidi mambo ya uendeshaji wa mashirika kama ilivyo tanesco...nadhani unakosea na wala hujui taaluma za kila member wa JF. Unasema mitambo inafanya kazi 24hrs bila kupumzishwa.......mitambo za ziada (standby..),....who should do that? Kazi ya tanesco ni nini?

  Unasema wabongo wanapenda kupindisha mambo.....kk mjadala huu ni nini kimepindishwa?? Jaribu kutumia akili kabla huja bandika ujinga wako humu.
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Oct 4, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Miafrika bana! Sometimes they make you laugh...
   
Loading...