Tanesco yatabiriwa kufilisika siku sii nyingi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco yatabiriwa kufilisika siku sii nyingi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkombozi, Mar 23, 2011.

 1. M

  Mkombozi JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Tanesco yatabiriwa kufilisika, kutokana na Makampuni makubwa kama Twiga Cement, TBL, TCC na mengine mengi kuamua kuanzisha miradi yao mikubwa ya umeme wa uhakika basi TANESCO huenda ikakosa mapato makubwa sana yanayotaka kwenye makampuni haya. Tukumbuke kua Makampuni haya yanalipa tanesco hela yangi wastani million 300 kwa mwezi. Kiasi hiki cha makusanyo huwezi kukipata kwa watumiaji wa majumbani.

  Makampuni mengi yako kwenye harakati ya kufunga generators za kutumia gase ili kuondokana na umeme wa mgao wa Tanesco. Kitendo hiki kitaifanya Tanesco kukosa mapato na badala yake kuongeza bei ya umeme kila kukicha kwa wananchi ili kufidia mapato hayo.

  Serikali isipoliangalia hili kwa jicho la karibu sana, itakuta tanesco haitumiki tenda viwandani kutokana na umeme kuwa wa mashaka kila kukicha. Pia serikali imeshindwa kuchukua hatua za makusudi za muda mrefu za kuanzisha miradi ya umeme na kufungua milango kwa wawekezaji binafsi ili kuleta tija ya nishati nchini.

  Bei ya bidhaa inategemea sana upatikanaji wa nishati ya uhakika.
   
Loading...