TANESCO yasimamisha kuunganisha umeme tangu Mei | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANESCO yasimamisha kuunganisha umeme tangu Mei

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Faru Kabula, Sep 13, 2010.

 1. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,875
  Trophy Points: 280
  Kuna habari kwamba shirika la umeme nchini (TANESCO) limesimamisha kuunganishia wateja wake wapya huduma hiyo muhimu. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari hii toka ndani ya shirika hilo, sababu kubwa inayotolewa na shirika hilo ni kukosekana kwa nyaya za kuunganisha kutoka kwenye mlingoti kwenda katika jengo (service line) na kwamba mteja wa mwisho kupata huduma hiyo katika mkoa wa Ilala (wa TANESCO) aliwekewa mwezi wa Mei 2010. Kama kuna ukweli wa habari hii, maana yake ni kwamba iwapo ataonekana mteja ameunganishiwa umeme hivi karibuni, basi huyo atakuwa ametoa rushwa au amepita njia za 'panya' na anatakiwa aripotiwe TAKUKURU ili wachunguze ni nani amemuwekea umeme na ametoa wapi nyaya wakati inajulikana kwamba nchi nzima hakuna nyaya na huduma ilishasimamishwa. Naona MD mpya amekuja na mikosi. Karibuni jamvini ...

  NB: Naombeni msaada wa kisheria kwani nataka niwashitaki TANESCO kwa kukiuka mkataba wa kuniwekea umeme ndani ya siku 60 baada ya kufanya malipo halali.
   
 2. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Inawezekana kabisa na mimi nipo mmojawapo nitatoa ushahidi hadi leo sijapata umeme tokea nilipiae Mwezi wa Sita.
   
 3. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
   
 4. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,875
  Trophy Points: 280
  Naendelea kukusanya maoni ili niwaburuze hawa jamaa mahakamani.
   
 5. T

  Teko JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2010
  Joined: Jul 3, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  mimi nililipia mei wakahaidi kuja tarehe 30 june,lakini hiyo tarehe ikapita hawakuonekana.Nilipoona muda unazidi kwenda nikaenda kuwauliza mbona muda umepita waliohaidi,wakasema hawana mita za luku.Wiki iliyopita nilifuatilia tena, wanadai hadi baada ya uchaguzi.
   
 6. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Huko Iringa sasa hawapokei hata pesa ya kuunganishja umeme kwa madai hayohayo-hawana nyaya! Sasa kama huko Dar ni huku mikoani tumekwisha.

  Kwa mujibu wa sheria wamefanya kosa kwa kushindwa kukuunganishia umeme baada ya kupokea malipo yako, nenda EWURA kawashitaki na kabla ya hayo anza kuwalima barua ya notisi kwanza kwa Meneja wao.
   
 7. BrainPower

  BrainPower Senior Member

  #7
  Sep 15, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Duu ! Hii ni dhambi jamani. Sasa kama wameshindwa umeme , na maji ndio shida - hivi internet wataiweza kweli ?
   
Loading...