TANESCO yasema haina mpango wa kuongeza bei za umeme kwa watumiaji wadogo

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,961
Shirika la umeme nchini TANESCO limesema halina mpango wa kupandisha bei za umeme kwa watumiaji wadogo na badala yake mpango huo upo kwa watumiaji wakubwa.
 
Kwahiyo wataongeza kwa wenye viwanda ili bidhaa zipande?.....

Hoja ni kwamba kwa nini upandishe umeme wakati gesi ipo ?......

Kwanini tuliambiwa baada ya gesi umeme utashuka?.....

Muhongo ndiye aliwaambia watu akiwa wizara hiyo hiyo 2014 kuwa umeme utashuka kwa kasi baada ya kuanza kutumia gesi........
 
Watumiaji wadogo ndio tunaendesha kampuni ya Tanesco. Mkoani kama Songwe mtumiaji mkubwa wa Umeme ni nani zaidi ya tembo cement?
hujui maana ya mtumiaji mdogo,unaweza ukajihisi wewe ni mtumiaji mdogo kumbe sivyo.Kama unatumia zaidi ya unit 75 kwa mwezi basi wewe si mtumiaji mdogo.Pigo hili linaenda kulamba zaidi ya asilimia 75 ya watumiaji wa sasa wa umeme
 
Tusidanganyane. Bei ikipanda, uzalishaji wa bidhaa utapanda na bei ya huduma itapanda na mlipaji wa mwisho ni mlaji ambaye ni huyu mwananchi wa chini. Hata ukiwapandishia wenye viwanda tu, mwananchi wa chini ndiye atakayeumia.
 
Ukiongeza umeme kwa watumiaji wakubwa mfano viwanda inamaanisha umepandisha inflation...waache danganya toto.
 
hujui maana ya mtumiaji mdogo,unaweza ukajihisi wewe ni mtumiaji mdogo kumbe sivyo.Kama unatumia zaidi ya unit 75 kwa mwezi basi wewe si mtumiaji mdogo.Pigo hili linaenda kulamba zaidi ya asilimia 75 ya watumiaji wa sasa wa umeme
Masikini sisi, tuko kama wakiwa, hatuna mtetezi, tunabanwa kila kona, kule kwenye mafao hakuna wakututetea, kwenye kodi za vimshahara vyetu hakuna wakututetea, hawa wa vyama vya wafanyakazi ni simba wa maboksi hawezi kuuma. Sasa ndo wanakuja huku kwenye umeme, gesi ndo bado anasa, mkaaa ndo usiseme, mafta taa nayo ndo hivyo, eeeeeeeeeh. Powa tu lakini, Mungu anaona.
 
Hii haingii akilini. Ni sawa na kusema bei ya mafuta ya taa haitapanda kwa kuwa watumiaji ni wananchi wa hali ya chini. Wakati huo huo ukipandisha bei ya petroli bila kujali athari za usafirishaji wa bidhaa na usafiri wa umma(Daladala) kwa ujumla! Tanesco jipangeni upya.
 
Mambo ya kifala nchi hii yataendelea mpaka tutakapo kubali kuzitumia akili zetu ipasavyo katika uchumi kunakitu kinaitwa cheni kuongeza bei ya umm kwa namna yoyote inaua uchumi na inamwasiri MTU wa chini zaidi
 
Shirika la umeme nchini TANESCO limesema halina mpango wa kupandisha bei za umeme kwa watumiaji wadogo na badala yake mpango huo upo kwa watumiaji wakubwa.

Jambo lolote kinyume na kushusha bei ya umeme kwa 50% litakuwa upuuzi na kichefuchefu tu
 
JF kama kawaida watapotosha tu ..... ..... sikio la kufa halina dawa. JF tubadilike.
 
Bogus.

Shusha umeme kwa wafanya biashara ili wawekeze zaidi, wananchi wapate ajira na serikali ikusanye kodi.

Kuongeza bei ya umeme ni kuuwa uchumi.

Hii ndiyo mijitu iliyosomea ujinga shule.
 
Hili swala ni kama yale ya VAT kuwa mlipaji ni mtoa huduma wakati anakuja kulipa mtumiaji
 
Nilitype bonge la tusi nikakumbuka sina mil 7.
Kweny VAT ya ATM na miamala ya simu walitudanganya hivohivo, mwisho wa siku tunakatwa hiv watanzania tunachukuliwaje???
Kweli tongotongo la zege limetanda machoni mwetu hatuwezi ona.
 
Tulitegemea aseme, "Kwa kuwa bomba la gesi sasa limefika Kinyerezi na kwa kuwa sasa tumefunga majenereta yetu yasiyo na capacity charge, tunakusudia kuteremsha bei ya umeme kwa asilimia 35%" Tuliahidiwa hivyo na Muhongo na wanasiasa wengine kuwa ingekuwa hivyo gesi ikifika Dar!!
 
Tanesco ni jipu linalotoa usaa unaonuka nusura yake halijapata mkamuaji mpaka leo
 
Back
Top Bottom