Tanesco yapoteza umeme wa Sh 100 bilioni kwa mwaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco yapoteza umeme wa Sh 100 bilioni kwa mwaka

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Apr 15, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Sadick Mtulya

  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Cag), Ludovick Utouh amesema kuwa upo uwezekano wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kufilisika baada ya kubaini kuwa kila mwaka linakabiliwa na upotevu wa Sh 100 bilioni.

  Alisema fedha hizo zinapotea wakati wa kusambaza nishati hiyo kutoka kwenye vyanzo vyake hadi kwa watumiaji.

  Utouh alieleza kwenye ripoti yake, ambayo gazeti hili lina nakala yake amebaini shirika hilo limepata hasara ya Sh Sh48 bilioni mwaka uliopita kutokana na ununuzi wa umeme kutoka katika kampuni binafsi, ikiwemo IPTL kufuatia mgawo mkubwa uliojitokeza Septemba na Oktoba, mwaka jana.

  Ripoti hiyo ya Cag iliyowasilishwa Aprili 6, mwaka huu katika kikao baina ya watendaji wakuu wa Tanesco na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Masharika ya Umma (Poac) kilichofanyika katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.

  Kutokana na hali hiyo, Poac iliiagiza Tanesco kuhakikisha inafanya jitihada za kujinasua katika hali hiyo.

  Akizungumza jana na Mwananchi mwenyekiti wa Poac, Zitto Kabwe alisema pamoja na mambo mengine kamati yake imeitaka Tanesco ifanye kila liwezakanalo ili iondokane na matatizo iliyo nayo.

  "Kamati yangu imeiagiza Tanesco kuhakikisha inafanya jitihada za kujinasua kutoka katika kupata hasara na itengeneze faida na si vinginevyo.

  Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini alifafanua kwamba Tanesco inapata hasara ya zaidi ya Sh100 bilioni kutokana na kupoteza asilimia 23 ya umeme wakati wa hatua ya kuusambaza kutoka katika mitambo yake ya uzalishaji hadi kwa watumiaji.

  Katika kutaka kuelezea ukubwa wa tatizo hilo, Zitto alisema "hali ya upotevu wa umeme kwa asilimia 23 ni sawa na mtambo wa kidato unaozalisha umeme wa megawati 50 kuzalisha umeme na kisha ukapotea bure yaani bila ya kutumika."

  Hata hivyo, Zitto alisema ni asilimia 77 tu ya umeme ndiyo inayowafikia wateja.

  Zitto alisema kwa kufuata utaratibu unaotakiwa Tanesco ilitakiwa kuwa na umeme wa ziada kwa asilimia 20 ambao ungesaidia kupunguza na hata kudhibiti mgawo wa umeme.

  "Kwa sasa umeme wa Tanesco haukidhi mahitaji nchini kutokana na kwamba umeme unaozalishwa na mitambo ya shirika hilo, asilimia 77 unatumia wote huku asilimia 23 hupotea wakati unaposambazwa," alisema

  Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI), Sam Nyantahe alisema jana kuwa shirikisho lake limeanza kuwashawishi watu pamoja na kampuni binafsi ili wawekeza katika uzalishaji wa umeme.

  Alisema CTI imefikia hatua hiyo kutokana na kuhitaji umeme wa uhakika na wenye kikidhi tija.

  Mwenyekiti huyo alisema kwa sasa hapa nchini kuna viwanda ambavyo vinatumia kati ya megawati 11 na 12 za umeme, hivyo imeongeza mahitaji ya nishati hiyo.

  Mgawo wa Septemba na Oktoba mwaka jana ulisababisha Rais Jakaya Kikwete kuingilia kati na kuagiza mitambo kumi ya kufua umeme wa megawati 100 ya IPTL kuwashwa.


  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=19212
   
 2. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2010
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Kitu ambacho sijaelewa ni kwamba, hiyo 23% loss kutoka kwenye mitambo hadi kwa watumiaji ni kwa sababu ya miundo mbinu mibovu, au ni nini hasa?

  And also there was a funny story about Ngeleja's statement that Tanzania will start harvesting Nuclear power in 1012.

  read the full stroy here Click here
   
Loading...