TANESCO Yapongezwa kwa Kuzalisha, Kusafirisha na Kusambaza Umeme Nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,781
898
TANESCO YAPONGEZWA KWA KUZALISHA, KUSAFIRISHA NA KUSAMBAZA UMEME NCHINI.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imepongeza uongozi wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kwa jitihada zake za uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme nchini.

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dunstan Kitandula ametoa pongezi hizo Jijini Dodoma wakati Kamati hiyo ilipokuwa katika semina ya kujengewa uwezo katika masuala ya umeme, mafuta na gesi, Machi 25 hadi 26, 2023.

‘’Sisi Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini tunaipongeza Wizara ya Nishati na Shirika la umeme Tanzania kwa juhudi wanazofanya katika uzalishaji, usafirishaji na usambazaji umeme nchini, jambo ambalo linaongeza ukuaji wa uchumi wa Taifa letu kwa kasi,” amesema Kitandula.

Akizungumza na wajumbe wa Kamati hiyo, Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato amesema kuwa lengo la semina hiyo ilikuwa ni kutoa uelewa sawa kwa wajumbe wapya na kuwaongezea uelewa wale waliokuwepo katika kamati hiyo.

Amesema semina hiyo imeandaliwa na Wizara ya Nishati kupitia TANESCO pamoja na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ili kuendelea kuwaimarisha wajumbe wa kamati hiyo kwa kuwa ndio wanaoishauri serikali katika sekta ya umeme, mafuta na gesi.

Wakati akifunga semina hiyo, Kitandula ameipongeza Wizara na taasisi hizo mbili kwa kuandaa mafunzo hayo yaliyokuwa na lengo la kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo ya Bunge.

Baadhi ya waliohudhuria semina hiyo ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athumani Selemani Mbuttuka, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Maharage Chande, Mkurugenzi wa TPDC, Mussa Makame pamoja na watendaji wengine wa Wizara na taasisi hizo.

Maelezo ya Picha

Moja.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Dunstan Kitandula akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa sawa kwa wajumbe wapya na kuwaongezea uelewa wale waliokuwepo katika sekta ya Umeme, Mafuta na Gesi.

Mbili.
Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato akiwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uelewa sawa wajumbe wapya wa kamati hiyo na kuwaongezea uelewa wale waliokuwepo katika sekta ya Umeme, Mafuta na Gesi

Tatu.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athumani Selemani Mbuttuka akiwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uelewa sawa wajumbe wapya wa kamati hiyo na kuwaongezea uelewa wale waliokuwepo katika sekta ya Umeme, Mafuta na Gesi.

Nne.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, Maharage Chande, akiwasilisha mada kwenye mafunzo ya kuwajengea uelewa sawa wajumbe wapya wa kamati hiyo na kuwaongezea uelewa wale waliokuwepo katika sekta ya Umeme nchini.

Tano.
Mkurugenzi wa Shirika la Petroli Tanzania, Mussa Makame, akiwasilisha mada kwenye mafunzo ya kuwajengea uelewa sawa wa wajumbe wapya wa kamati hiyo na kuwaongezea uelewa wale waliokuwepo katika sekta ya Mafuta na Gesi nchini.

Sita.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wakiwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uelewa sawa wajumbe wapya wa kamati hiyo na kuwaongezea uelewa wale waliokuwepo katika sekta ya Nishati Umeme, Mafuta na Gesi.

Saba.
Watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la umeme Tanzania pamoja na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, wakiwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uelewa sawa wa wajumbe wapya wa kamati ya Nishati na Madini na kuwaongezea uelewa wale waliokuwepo katika kamati hiyo, katika sekta ya Umeme, Mafuta na Gesi.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-03-27 at 00.56.13.jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-27 at 00.56.13.jpeg
    123.8 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-03-27 at 00.56.14.jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-27 at 00.56.14.jpeg
    106.6 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-03-27 at 00.56.15.jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-27 at 00.56.15.jpeg
    96.1 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-03-27 at 00.56.15(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-27 at 00.56.15(1).jpeg
    72.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-03-27 at 00.56.16.jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-27 at 00.56.16.jpeg
    66.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-03-27 at 00.56.16(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-27 at 00.56.16(1).jpeg
    114.7 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-03-27 at 00.56.16(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-27 at 00.56.16(2).jpeg
    132.5 KB · Views: 2
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom