TANESCO yakalia fidia ya wananchi miaka mitano

rushesheka

New Member
May 13, 2021
4
45
Fedha za fidia ya wananchi wanaopisha ujenzi wa njia ya mradi wa umeme kutoka bwawa la Mwl Nyerere za kwama Tanesco fedha hizi zilidhinishwa na bunge la bajeti la 2015/2016 kwa ajili ya malipo ya fidia kwa kusimamiwa na Tanesco mpaka leo 2021hakuna taarifa yoyote rasimi kwamba fedha hizi zinalipwa lini? Ila wana kauli mbiu yao kila mara usema 'HAZINA HAWAJALETA HELA' Kingine cha kushangaza na kusikitisha hakuna mdai yeyote anayejua anadai kiasi gani cha fedha, tunadai tusichokijua. Hii ni siri inayotia mashaka makubwa sana.

Hatujui kama endapo wataamua kulipa watalipa kwa kuzingatia principal au formula hipi ? Mradi wenyewe ni kutoka Kinyerezi kupitia Chalinze kuelekea Tanga na Arusha ukiitwa North East grid KV400 ulifanyiwa tathimini mwaka 2015 na baadaye 2018 ukauhishwa na kuitwa Bwawa la Mwl Nyerere hadi Chalinze Dodoma na Dar es salaam sasa ni 2021 hapa kumbuka kisheri kuna haki ya kulipwa pamoja na riba ya miaka mitano kulingana na viwango vya Benki Kuu.

Sasa swali kwa kuwa muhathilika wa mradi hajui kiasi anchopaswa kufidiwa si nirahisi kudanganywa kuwa kiasi atakacholipwa mtu kimejumlishwa na riba ya ucheleweshaji? Hapa kunatakiwa Tanesco wawe wazi kila mtu ajue kiasi anacho stahili kulipwa na riba ni kiasi gani?

Kama matakwa ya kisheria yatatimizwa hata wakikaa miaka mingine mitano kila mtu atakuwa anajua haki yake kisheria iko wapi . Mh Waziri wa ardhi na makazi tunakutegemea sana katika hili busara zako zinaepusha migogoro mingi sana hisiyo ya lazima. Mh Mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan ametamka mwenyewe kwa kauli yake amesema hataki mtu adhulumiwe wala serikali yake isidhulumu mtu, hataki hataki kabisa.

TANESCO lini mnalipa watu fidia zao pamoja riba yao? Hilo ndio swali la msingi. Umeme kwa maendeleo yetu , lakini haki itendeke.
 

chaliko

Senior Member
Apr 1, 2019
180
1,000
TANESCO ni genge la Wahuni, kule DODOMA eneo la KIKOMBO na MSALATO tangu 2018 wametwaa Ardhi ya Wananchi na leo hii hawajawalipa.

Wanakuja na Mbwebwe nyingi kuwa FEDHA ipo kumbe hamna kitu.

Narudia tena TANESCO ni WAHUNI.
 

sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,208
2,000
Achaneni na mambo ya kubembelezana fanyeni mambo kisheria, wafikisheni TANESCO mahakamani. Jana majaji 25 wa Mahakama kuu wameapishwa na Mheshimiwa Rais Samia, mpaka sasa hawana kesi, fungueni na kesi yenu wapewe itasikilizwa muda mfupi tu na mkajua kile mnachostahili kupata.

Kisheria hesabu ya fidia inafanywa kwa njia mbili, kwa uthamini wa mali iliyopo eneo linalochukuliwa au kwa mfidiwa kutaja kiwango anachotaka kulipwa. Sasa kama hapo kwenu hakuna uthamini uliofanyika au uthamini ulifanyika bila ninyi kushirikishwa (kusaini idadi ya mali pamoja na thamani yake) basi fidia sahihi inakuwa ni ile mliyotaka kulipwa kwa kujitajia nyie wenyewe.

Kama hapajabomolewa basi uthamini unaweza kufanywa upya ili utoke na thamani halisia ya wakati huu ila kama walishabomoa na hakuna cha kukifanyia uthamini, mtalipwa kile kiwango mlichokuwa mmekitaka nyie.

Msipoteze muda, jikusanyeni pamoja muende mahakamani muweke mambo kisheria ama sivyo mtapoteza kabisa kama mtaendelea kubembelezana.​
 

rushesheka

New Member
May 13, 2021
4
45
Fedha za fidia ya wananchi wanaopisha ujenzi wa njia ya mradi wa umeme kutoka bwawa la Mwl Nyerere za kwama Tanesco, fedha hizi zilidhinishwa na bunge la bajeti la 2015/2016 kwa ajili ya malipo ya fidia kwa kusimamiwa na Tanesco, mpaka leo 2021hakuna taarifa yoyote rasimi kwamba fedha hizi zinalipwa lini?

Ila wana kauli mbiu yao kila mara usema 'HAZINA HAWAJALETA HELA' Kingine cha kushangaza na kusikitisha hakuna mdai yeyote anayejua anadai kiasi gani cha fedha, Hii ni siri inayotia mashaka makubwa sana, hatujui kama endapo wataamua kulipa watalipa kwa kuzingatia principal au formula hipi?

Mradi wenyewe ni kutoka Kinyerezi kupitia Chalinze kuelekea Tanga na Arusha wakati huo ukiitwa North East grid KV400 na ulifanyiwa tathimini mwaka 2015 na baadae 2018 ukauhishwa na kuitwa Bwawa la Mwl Nyerere hadi Chalinze mpaka Dodoma na Dar es Salaam.

Sasa ni 2021 hapa kumbuka kisheri kuna haki ya kulipwa pamoja na riba ya uchelewesho kwa miaka mitano kulingana na viwango vya benki kuu. Sasa swali kwa kuwa muhathilika wa mradi hajui kiasi anchopaswa kufidiwa si ni rahisi kudanganywa kuwa kiasi atakacholipwa kimejumlishwa na riba ya ucheleweshaji?

Hapa kunatakiwa Tanesco wawe wazi kila mtu ajue kiasi anacho stahili kulipwa na riba ni kiasi gani? Endapo matakwa ya sheria yakitimizwa hata wakikaa bila kulipa miaka mingine mitano kila mtu atakuwa anajua haki yake kisheria iko wapi.

Mh Waziri wa ardhi na maendeleo ya makazi kwa pamoja na Waziri wa nishati tunawategemea sana busara zanu ili kuondoa migogoro mingi sana hisiyo ya lazima.

Mh Mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan ametamka mwenyewe kwa kauli yake amesema hataki mtu adhulumiwe wala serikali yake isidhulumu mtu ,hataki hataki kabisa. TANESCO lini mnalipa watu fidia zao pamoja riba yao?

Hilo ndio swali la msingi. Umeme kwa maendeleo yetu, lakini haki itendeke.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom