TANESCO yaingia mkataba wa kukodi software kutoka India kwa USD 30M

Watanzania naona tulisahau kabisa ajenda ya ufisadi wakati wa Magufuli, mpaka sasa kuna ufisadi umefanyika fasta fasta bila ya watu hata kushtuka.

Mkataba uliosainiwa baina ya Serikali ya Tanzania (kupitia TANESCO) na kampuni ya Tech Mahindra ya India wenye thamani ya dola milioni 30 ni wa kukodisha software ya Enterprise Resources Planning (ERP) - ambayo wahindi hawa wenyewe wanaiita Corporate Management System (CMS), kama inavyosomeka kwenye bango pichani chini.

Software ya aina hii huwa inaunganisha vitengo vyote vya taasisi katika software moja kwa ajili ya urahisi wa kuendesha taasisi. Hivyo basi kwa lugha nyingine ni kwamba Wahindi hawa watafunguliwa milango ya kuingia kila mahali ndani ya TANESCO, na hivyo kuwa na siri zote za mfumo wetu wa umeme.

Jambo kama hili ni hatari sana kwa usalama wa taifa. Hakuna njia rahisi ya kuiangusha nchi bila ya kufyatua hata kombora moja kama kuangusha mfumo wa nchi wa umeme.

Software kama hizi serikali inatakiwa iwawezeshe wataalam wa ndani kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao kutengeneza, kama vile mfumo wa malipo serikalini ulivyotengenezwa na wataalam wetu wa ndani kwa kuwezeshwa na serikali.

Zabuni ya kukodisha software hii ilianzaga kwenye dakika za lala salama za utawala wa Kikwete. Hivyo basi kitendo cha zabuni hii kukaa benchi kwa miaka mitano ya Magufuli kinaonesha kuwa hakuwa amekubaliana nayo. Baada ya Magufuli kufa naona wadau wa zabuni hii wameiendeleza na kuimwagia wino fasta, kama wanavyotaka kufanya kuhusu bandari ya Bagamoyo.

img-618a884f193e3.jpg
Hii kitu kimeniumeza akili sana kwa kweli kipindi cha magufulia ndo tumeona wataalam wetu wa IT wakipewa kipaumbele kwa kutengeneza mifumo yetu sisi wenyewe kama Gepg , NHIF , GotTHoMis. Plan Rep FASS. Umhm wa wataalam wetu kutumika kwenye mifumo mhim ya uendeshaji wa nchi ni mkubww Sana kwa usalama wa nchi na vile vile low cost ukilinganisha na gharama za kuwalipia watu kwa dollars na perdiem
 
Sioengelei hizi software zinazotengenezwa na makajanja anayekuambia anatoa app kwa 30,000 au kila siku yeye ana punguzo kuna watu wakongwe wapo wamefanya mambo makubwa na hakuna longolongo na wapo wanaoamini zimetengenezwa na wazungu ila ukiambiwa historia yake ndio utaelewa. Tatizo ni watu wamevamia fani na kumekosekana regulation ya maana ya nani ni nani ndio maana wengi mnakuwa na hiyo perception. Unafikiri hakuna software zilozochukuliwa kutoka nje ambazo zimeflop pia ? ukiambiwa ndio utashangaa zaidi gharama zilizoingiwa
Kizuri Cha jiuza kama zingekuwepo hizo software zilizotengenezwa kutoka Tanzania tungezijua
 
Mnaolalamika tengenezeni software zenu halafu mkawauzie Tanesco kwa bei nafuu kama mnaona ni kazi nyepesi. Kwa nini mnataka kuandikia mate wakati wino upo? Changamkeni fanyeni kazi andikeni hizo software halafu mkauzie hayo mashirika ya umma.
 
Hio ndo point yangu wanazingua sana
 
30 Million Dollars = 69 Billion Tanzania Shillings aisee tuache utani, hiyo software ina nini cha ziada, ni license ya muda gani ?

Serikali ingeweza kuunda timu ya kuunda huo mfumo na kuna uwezekano ungekuwa ni chini ya nusu ya gharama na ungemilikiwa 100% na serikali sio haya mambo ya kukodi. Mbona GepG imeundwa na wataalamu wa ndani na inafanya kazi bila matatizo yoyote...unafikiri serikali ingeamua kukodi mfumo wa malipo ya nchi nzima wangetumia gharama kiasi gani ?
Wapigaji kazi yao ni kuwaza ku outsource nje kila kitu ili wapate ten per cent. Ni watu waovu sana maana kwanza wanakubali bei kubwa ili per cent yao iwe kubwa.
Maendeleo ya nchi ni kujenga uwezo wa kujitegemea kwa hiyo wapigaji wala hawastahili kabisa uongozi nchini kama tunataka maendeleo.
 
Watanzania naona tulisahau kabisa ajenda ya ufisadi wakati wa Magufuli, mpaka sasa kuna ufisadi umefanyika fasta fasta bila ya watu hata kushtuka.

Mkataba uliosainiwa baina ya Serikali ya Tanzania (kupitia TANESCO) na kampuni ya Tech Mahindra ya India wenye thamani ya dola milioni 30 ni wa kukodisha software ya Enterprise Resources Planning (ERP) - ambayo wahindi hawa wenyewe wanaiita Corporate Management System (CMS), kama inavyosomeka kwenye bango pichani chini.

Software ya aina hii huwa inaunganisha vitengo vyote vya taasisi katika software moja kwa ajili ya urahisi wa kuendesha taasisi. Hivyo basi kwa lugha nyingine ni kwamba Wahindi hawa watafunguliwa milango ya kuingia kila mahali ndani ya TANESCO, na hivyo kuwa na siri zote za mfumo wetu wa umeme.

Jambo kama hili ni hatari sana kwa usalama wa taifa. Hakuna njia rahisi ya kuiangusha nchi bila ya kufyatua hata kombora moja kama kuangusha mfumo wa nchi wa umeme.

Software kama hizi serikali inatakiwa iwawezeshe wataalam wa ndani kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao kutengeneza, kama vile mfumo wa malipo serikalini ulivyotengenezwa na wataalam wetu wa ndani kwa kuwezeshwa na serikali.

Zabuni ya kukodisha software hii ilianzaga kwenye dakika za lala salama za utawala wa Kikwete. Hivyo basi kitendo cha zabuni hii kukaa benchi kwa miaka mitano ya Magufuli kinaonesha kuwa hakuwa amekubaliana nayo. Baada ya Magufuli kufa naona wadau wa zabuni hii wameiendeleza na kuimwagia wino fasta, kama wanavyotaka kufanya kuhusu bandari ya Bagamoyo.

img-618a884f193e3.jpg
Tamko la kwanza la Waziri January ilikuwa ni agizo kwa utawala mpya wa TANESCO (Bodi na Menejementi) kuingia "digital". Hivyo siyo ajabu kufufuliwa kwa mkataba huo feki wenye kila aina ya hatari kwa Taifa mbali na ufisadi
 
Hapo cha muhimu, ni ku train watu wetu wa humu ndani kwa nguvu zote, baada ya hapo mnawafungia vioo kimoja...

Kama nchi zilizoendelea zinavyoiba teknolojia za wengine...
 
Kuna uharaka gani wa kutengeneza huo mfumo bila kushirikisha watalaamu wa ndani ya nchi, au japo kutangaza hiyo tender?

Je, mfumo ungeleta maji au kujaza mto Ruvu au kufanya mvua inyeshe ikiwa umetengenezwa na wahindi?

Tatizo kubwa la TANESCO kwa sasa ni kutokuwepo kwa huo mfumo?

1. Nina uhakika 100% huo mfumo unatengenezwa hapa nchini Tanzania bila shida yoyote
2. Hiyo hela inayolipwa kwa wahindi ni "overwhelming"
3. Tungetumia wataalamu wetu, mfumo ungekuwa ni wetu, watalaamu au vijana wetu wangepata ajira, hela ambayo ingetumika ingekuwa ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na hiyo waliyolipwa wahindi
4. Usimamizi, usalama/ulinzi, maboresho, na matengenezo ya mfumo, vingeendelea kuwa chini ya wataalamu wetu kwa gharama ndogo
5. Tungeendelea kukua na kujitegemea katika sekta ya software

Matumizi na functionalities za huo mfumo hazitakuwa tofauti sana logically na za huu mfumo Need Human Resource Information/Management System (HRIS/HRMS) (***** - HR SERVICE na mifumo mingine iliyoelezewa hapa https://www.ega.go.tz/uploads/pressreleases/sw-1574867949-ERMS ENG.pd? Kinachotakiwa ni kuadapt tu mifumo iliyopo, kucustomize/kumodify, kuongeza modules na functionalities pale inapotakiwa. Pia Wataalamu wetu wana uwezo wa kutengeneza huo mfumo from scratch.

Huo mfumo unafanana na ipi kati ya hii The 11 Best ERP Solutions for Government and Public Sector Workers?
 
Kuna Halmashauri niliwahi kufanya kazi Idara ya Ardhi waliibia Halmashauri huku madiwani wakimwaga sifa nyingi kwa ubunifu wa ile Idara. Walidownload Google Map wakadai wamenunua software kwa gharama ya Sh 20 milioni ili kusaidia mipango mji.

Lile dude tulilibeba mpaka Maonesho ya Nane Nane kuwaonesha wananchi jinsi Halmashauri yetu ilivyopiga hatua katika Idara ya Mipango Miji. Sidhani mpaka leo kama ile Halmashauri ilishagundua iliibiwa. Tuligundua vijana wawili tu kitoka Idara nyingine ambao tulikuwa ndo tumepata ajira.

Just imagine kama Halmashauri inaibiwa kienyeji namna hiyo hali ikoje katika mambo makubwa ambayo Watanzania wengi hawana utaalam nayo?
Acha uongo

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Wanawake wa Tanzania wamepiga hatua hadi kufikia nafasi ya urais na nafikiri hili ndiyo jambo kubwa kwa Samia kwamba yeye mwanamke kutambulika kuwa ni kiongozi wa juu kabisa katika nchi, sasa hayo ya sijui ni vp huyo mwanamke anaiongoza hii nchi sio la kuliangalia sana sasa hivi muhimu ni kufurahia hii hatua ambayo wanawake wameweza kuifikia basi.
😂
 
Wizi mtupu , EGA wanafanya kazi gani , c kitengo kilichoanzishwa kwa ajili ya kudevelop software za serekali , ujinga mtupu aisee
 
Back
Top Bottom