TANESCO yaingia mkataba wa kukodi software kutoka India kwa USD 30M

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
587
1,000
TAtizo la mtoa Uzi ni mshamba, mill 30 kwa software ni ya kawaida kwa kampuni kubwa kama TANESCO

Mmezoea kutumia software za uwizi unafikiri kampuni kubwa kama TANESCO nao watatumia hapana
Mkuu uwe unasoma nakuelewa basi unaambiwa $ wewe unatamka milion 30 kama shilingi! Upo meza kuu nini
 

UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
13,162
2,000
Wanawake wa Tanzania wamepiga hatua hadi kufikia nafasi ya urais na nafikiri hili ndiyo jambo kubwa kwa Samia kwamba yeye mwanamke kutambulika kuwa ni kiongozi wa juu kabisa katika nchi, sasa hayo ya sijui ni vp huyo mwanamke anaiongoza hii nchi sio la kuliangalia sana sasa hivi muhimu ni kufurahia hii hatua ambayo wanawake wameweza kuifikia basi.
 

Janjaweed

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
12,297
2,000
Watanzania naona tulisahau kabisa ajenda ya ufisadi wakati wa Magufuli, mpaka sasa kuna ufisadi umefanyika fasta fasta bila ya watu hata kushtuka.

Mkataba uliosainiwa baina ya Serikali ya Tanzania (kupitia TANESCO) na kampuni ya Tech Mahindra ya India wenye thamani ya dola milioni 30 ni wa kukodisha software ya Enterprise Resources Planning (ERP) - ambayo wahindi hawa wenyewe wanaiita Corporate Management System (CMS), kama inavyosomeka kwenye bango pichani chini.

Software ya aina hii huwa inaunganisha vitengo vyote vya taasisi katika software moja kwa ajili ya urahisi wa kuendesha taasisi. Hivyo basi kwa lugha nyingine ni kwamba Wahindi hawa watafunguliwa milango ya kuingia kila mahali ndani ya TANESCO, na hivyo kuwa na siri zote za mfumo wetu wa umeme.

Jambo kama hili ni hatari sana kwa usalama wa taifa. Hakuna njia rahisi ya kuiangusha nchi bila ya kufyatua hata kombora moja kama kuangusha mfumo wa nchi wa umeme.

Software kama hizi serikali inatakiwa iwawezeshe wataalam wa ndani kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao kutengeneza, kama vile mfumo wa malipo serikalini ulivyotengenezwa na wataalam wetu wa ndani kwa kuwezeshwa na serikali.

Zabuni ya kukodisha software hii ilianzaga kwenye dakika za lala salama za utawala wa Kikwete. Hivyo basi kitendo cha zabuni hii kukaa benchi kwa miaka mitano ya Magufuli kinaonesha kuwa hakuwa amekubaliana nayo. Baada ya Magufuli kufa naona wadau wa zabuni hii wameiendeleza na kuimwagia wino fasta, kama wanavyotaka kufanya kuhusu bandari ya Bagamoyo.

img-618a884f193e3.jpg
At Some point

I was made to believe kwamba EGA ndio atakua msimamizi mkuu wa haya mambo na tutajitahidi kuwa tunatengeneza software zetu Kwa ajili ya haya mambo
 

Wamabere

JF-Expert Member
Jul 19, 2016
1,103
2,000
Hili tatizo linaanzia kule juu kabisa, unapokuwa na kiongozi asietaka kushughulisha akili yake kwa chochote zaidi ya kusubiri kuletewa taarifa na wasaidizi wake huyo ndie chanzo.

Wasaidizi wake wanaweza kumpelekea mawazo ya hovyo yenye malengo ya "kutupiga", na kwasababu kiongozi mwenyewe hawezi kuhoji chochote anayakubali tu mawazo hayo kutokana na namna pumba anazolishwa zitakavyokuwa zimepangiliwa.

Matokeo yake ndio haya, unaona habari ya kukodi software ya $ 30 milion, baada ya kutoka kule kwenye mradi wa LNG ambao nao naamini alipigwa sound akaukubali bila kujua chochote, wala asijue hao anaowatuma ndio wajanja wenyewe, anachofanya Rais ni sawa na kumkabidhi fisi bucha sasa tunavuna tulichopanda.
Jamani nchi yetu na Wahindi ! Jumamosi iliyopita nilisafiri na treni kutoka Dar mpaka Arusha. Tulipoondoka Dar nilikuwa naongea na staff mmoja fundi wa TRC nae alikuwa anasafiri tulipopita pale Ilala yard akanionyesha akasema mle ndani ya workshop kuna vile vichwa vya treni 12 vilvyoibuliwa na JPM pale bandarini kutoka India ambapo mwenye mali hajajitokeza mpaka leo na vichwa vimeegeshwa tu. Tunaambiwa ile ni dili ya viongozi wawili mmoja alishaondoka zake sijui kama serikali ililipia hivyo vichwa au la. Ninachosema hapa wahindi kwa magendo!!!!! hongereni na kukodisha software kumbe ile juhudi ya Kalemani kumalizia vijiji vyote kupata umeme ilikuwa inazuia dili za watu.....
 

Ligaba

JF-Expert Member
Oct 12, 2018
1,031
2,000
Sio kwamba ufisadi ulikufa wakati wa Dikteta Magufuli, tatizo hapakuwa na vyanzo vya habari kuelezea mambo ya serikali.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom