Tanesco yadai... Mgawo wa umeme umesitishwa...........

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,620
2,000
Mgawo wa umeme wasitishwa

Imeandikwa na Halima Mlacha, Morogoro; Tarehe: 8th December 2010 @ 23:59

NgelejaUmeme%281%29.jpg


ANGALAU Watanzania wanaotumia nishati ya umeme watakuwa na ahueni sasa baada
ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutangaza kusitisha mgawo wa umeme uliodumu kwa zaidi ya wiki mbili.

Mkoa wa Dar es Salaam ulianza na mgawo huo kabla ya kuikumba mikoa mingine yote inayopata umeme kutoka Gridi ya Taifa, hali ambayo iliyafanya maisha ya Watanzania wengi kuwa katika hali mbaya.

Lakini jana Tanesco imetangaza kusitisha mgawo huo wa umeme ikieleza hali hiyo imetokana na mvua kuanza kunyesha na maji kuongezeka kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme ya Kidatu, Mtera na Kihansi katika mikoa ya Morogoro na Iringa.

Umeme wa Tanzania kwa kiasi kikubwa unazalishwa kwa kutegemea maji. Lakini pia Tanesco imesema inasitisha mgawo huo baada ya mashine moja kati ya nne zilizoharibika za Songas kupona.

Akizungumza na waandishi wa habari walioko katika ziara ya kuzungukia mitambo ya Kihansi na Mtera, Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud, alisema kwa sasa hali ya uzalishaji umeme inatia matumaini.

Badra alisema tatizo la mgawo wa umeme pamoja na kuharibika kwa mashine nne, lilisababisha kiwango cha maji katika mabwawa hayo kupungua kutokana na ukame.

"Hali ya uzalishaji umeme kwa sasa inaendelea vizuri, mvua kubwa zimenyesha na
mabwawa yetu ya Kihansi, Mtera na Kidatu yameingia maji ingawa si mengi, lakini yanatosheleza kusitisha mgawo uliodumu kwa takribani wiki mbili sasa," alifafanua Badra.

Hata hivyo, alisema pamoja na Tanesco kusitisha mgawo huo, hali inaweza kubadilika
wakati wowote na mgawo kurudi kama mabwawa hayo yasipoingiza maji ya kutosha.

Naye Kaimu Meneja wa Mtambo wa Kihansi, Patrick Lwesya, alisema awali maji katika bwawa la Kihansi, maji yalipungua na kufikia matumizi yake yashuke hadi lita za ujazo 8.8 kwa sekunde katika uzalishaji umeme.

"Kwa kawaida mtambo wa Kihansi huzalisha umeme kwa kutumia lita za ujazo 16.2 kutokana na mvua za leo (jana) zimeongezeka na kufikia lita za ujazo 10.27," alisema Lwesya.

Alisema hali ya uzalishaji katika mtambo huo unaochangia asilimia 25 katika Gridi ya Umeme ya Taifa mara nyingi hutegemea kiwango cha maji kinachokuwepo.

Alisema kwa sasa mtambo wa Kihansi uko kwenye mchakato wa kuzalisha megawati 120 nyingine na hivyo kuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 300 pindi awamu ya pili ya ujenzi wa mtambo huo itakapokamilika.

Alisema ujenzi huo wa awamu ya pili utahusishwa na uwekaji wa transfoma mbili ambapo moja tayari imeshawekwa ili kuongeza nguvu ya umeme huo.

Mgawo wa umeme ulianza wiki mbili zilizopita baada ya kupungua kwa maji katika mabwawa ya New Pangani na Kihansi sambamba na kuharibika mashine nne ikiwamo ya Songas inayozalisha megawati 35.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja amesema kupatikana kwa umeme wa uhakika kunategemea kukamilishwa kwa matengenezo ya mitambo iliyoharibika.

Ngeleja alisema hayo Dar es Salaam jana baada ya kutembelea mitambo ya kuzalisha umeme kwa lengo la kujua hali yake na jinsi ambavyo inaweza kupunguza mgawo wa umeme nchini.

Mitambo aliyotembelea ni pamoja na Songas, Kituo cha kuzalisha umeme cha Tanesco Ubungo, IPTL na Tegeta.

Akizungumza baada ya ziara hiyo, Ngeleja alisema mgawo wa umeme ulioanza takriban wiki mbili zilizopita, ulisababishwa na uharibifu wa mitambo kadhaa nchini ikiwemo ule wa Songas wa kuzalisha megawati 35, Kipawa wa megawati 32, mtambo mmoja wa Ubungo na upungufu wa maji.

Kuhusu mtambo wa Songas, alisema mtambo namba tatu ulioharibika tayari wamefunga mwingine ambao umeanza kuzalisha umeme, ila kuna mtambo mwingine wenye uwezo wa
kuzalisha megawati 35 ambao upo katika matengenezo ya kawaida.

"Mtambo unatakiwa kufanyiwa matengenezo ya kawaida kwa kuwa ulifanya kazi kwa muda mrefu na kwa mujibu wa vifaa hivyo usipofanyiwa matengenezo hayo unaweza kulipuka," alisema Ngeleja.

Hata hivyo, aliwataka watendaji wa Songas kufanya kazi kwa saa 24 wakishirikiana na wataalamu kutoka Kampuni ya Marekani ya General Electric ili kukamilisha kazi hiyo kesho ambapo watendaji hao walikiri kukamilisha kazi hiyo kwa muda huo.

Kwa upande wa IPTL, alisema hadi jana walikuwa wakiingiza umeme megawati 70, hivyo kuchangia kusitishwa kwa mgawo wa umeme.

"Tatizo kubwa kwa IPTL ni kukosa mafuta ya kutosha kwa wakati unaotakiwa wa kuendesha mitambo hiyo, ambapo kwa siku malori 17 humwaga mafuta huku upakuaji wa lori moja kuchukua saa mbili," alisema.

Kuhusu ongezeko la maji alisema kwa mabwawa ya Kidatu na Mtera kutokana na mvua
iliyonyesha juzi iliongeza kiwango cha mita 1.3 ya maji.
 

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
1,195
Hakuna kitu kama hiyo hizo ni propaganda tu mkuu, hivi ninavyoandika reply hii wameshauchukua zamaniiiiii kurudi mpaka jioni au usiku watakapoamua wenyewe. Natafuta safari nikirudi iwe usiku mkubwa nikute umeme umesharudi maana bila umeme hakukaliki kibaya sijawahi kupiga pasi!
 

mams

JF-Expert Member
Jul 19, 2009
614
195
Inawezekana kubinafisisha shirika la umeme likawa chini ya uangalizi wa regulatory authority na tukahakikishiwa umeme. Hatuwezi kuendelea kwa kutumia maji ya mvua ndiyo tupate umeme. Vinginevyo ingekuwa maji ya mvua basi nchi za jangwa wangekuwa na matatizo ya ajabu kinyume chake wao ndiyo wana umeme wa uhakika kuliko sisi!
 

Henge

JF-Expert Member
May 14, 2009
6,934
2,000
hakuna kitu kama hiyo hizo ni propaganda tu mkuu, hivi ninavyoandika reply hii wameshauchukua zamaniiiiii kurudi mpaka jioni au usiku watakapoamua wenyewe. Natafuta safari nikirudi iwe usiku mkubwa nikute umeme umesharudi maana bila umeme hakukaliki kibaya sijawahi kupiga pasi!
sokomoko leo ndo nimekuona unaongea! Upo kwenye ukweli zaidi!
 

bensonlifua92

Member
Dec 9, 2010
84
125
Umeme wa kudumu yaani maisha bila umeme wa mgao Tanzania inawezekana endapo tu wahusika wataacha kuwa na mtizamo wa kufisadi nchi yetu kupitia matatizo ya umeme. Wapo watu (na hao ni baadhi ya vigogo tu) wanafaidika na hali hii. Na pia baadhi ya wafanya biashara nao wanafaidika sana kwa kuuza majenereta, mafuta ya hayo majenereta, mishumaa, n.k. Napendekeza NGUVU YA UMMA kutumika ili kudai suluhisho la kudumu la umeme wa uhakika. Vinginevyo hawa jamaa wataendelea na visingizio vya maji kupungua ili waweze kutimiza malengo yao ya kujinufaisha
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,620
2,000
More electricity flows into national grid
By Correspondent9th December 2010
NgelejaUmeme%281%29.jpg

Energy and Minerals minister, William Ngeleja (L), on a working tour of power plants in Dar es Salaam yesterday, listens as Songas` plant manager, Robert Hosky briefs him on progress in fixing the machine breakdown at the plant.


The government has increased the supply of heavy fuel to Independent Power, Tanzania Ltd (IPTL) enabling it to pump more electricity, easing rationing.
This was said yesterday by the Energy and Minerals Minister, William Ngeleja during his visit at the Independent Power, Tanzania Ltd (IPTL).
He said the government had increased supply of heavy fuel to the IPTL boosting the plant's power production from 10 megawatts to 70 megawatts as of yesterday. IPTL pumps electricity to the national grid.
"IPTL has been short of heavy fuel for power production because of financial constraints on the part of the government. But with increased heavy fuel, it is now producing more electricity. I believe, this will help to mitigate the power crisis," said Ngeleja.
But he warned: "Ongoing power rationing would end after Tanesco' technicians complete repairing faulty machines at Songas gas plant and the Kipawa power transformer," he told reporters at the plant compound.
According to the minister, the latest power crisis, which forced Tanesco to embark on a countrywide load-shedding, was caused by technical problems that faced Songas, Ubungo gas plans, New Pangani Falls plant and decreased inflow of water at Kihansi and Kidatu hydro-power plants, fuel shortage at IPTL, defective power transformer.
"But yesterday there was no rationing because IPTL electricity production increased, and the volume of water increased by almost 1.3 metres at Kidatu hydro-power plant."
Repairs to defective machines at Songas gas plant had been completed and would add 32 megawatts to the grid, according to the minister.
Tanesco technicians in collaboration with experts from the US were still working on another defective 32 megawatt power plant, Ngeleja said, noting that the work is expected to be concluded on Friday.
"I am sure by Saturday, power crisis in the country would be resolved to a great extent," said the minister.
Reacting to a planned private motion of no confidence in him, for failure to oversee effective and efficient implementation of the country's power-master plan, minister Ngeleja said his resignation was not a solution to the power woes in the country.
The Kigoma-South MP (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, recently announced that he was planning to present a private motion in the Parliament to press for the resignation of the energy minister for failure to supervise power master-plan, a situation which has plunged the nation into darkness several times.
"That is his (Kafulila) opinion…I cannot prevent him from expressing his views. But I should insist that my resignation would not be a solution to power crisis in Tanzania," he said.
Asked about the ruling on the Tanesco-Dowans case, the minister said the issue was now in the hands of the Attorney General.
"The file of the controversial issue is now being worked on by the Attorney General…," said Ngeleja.SOURCE: THE GUARDIAN
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,620
2,000
Mtera yawahakikishia Watanzania


na Salehe Mohamed, Mtera


amka2.gif
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limewahakikishia Watanzania kuwa lina uwezo wa kutosha wa kuzalisha umeme katika bwawa la Mtera kwa muda wa miezi miwili hata kama mvua haitonyesha.
Hakikisho hilo lilitolewa jana katika bwawa la Mtera na Kaimu Meneja wa Mtera, Julius Chomola, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambao wanafanya ziara katika mabwawa ya kuzalisha umeme ya Kihansi na Mtera.
Alisema Mtera ndilo bwawa kubwa mbalo linahifadhi maji kwa kiwango kikubwa na hivi sasa lina maji ya kutosha kwa muda wa miezi miwili, bila kutegemea maji ya mvua.
Alibainisha kuwa bwawa hilo licha ya kuzalisha umeme asilimia 7.98 katika gridi ya taifa, pia ndilo linalotegemewa kuhifadhi maji ambayo hutumiwa na mitambo ya kuzalishia umeme wa maji ya Kidatu mkoani Morogoro; Kidatu huchangia umeme wa asilimia 20 katika gridi ya taifa.
Wakati huo huo, wakazi wa maeneo jirani na maeneo hayo jana walikuwa na furaha kubwa na walifanya tambiko baada ya kuonekana kwa mnyama aina ya Kakakuona ambaye inaaminika kuonekana kwake kunaashiria neema.
Wakizungumza na waandishi wa habari katika eneo lilipofanyika tambiko hilo, wazee wa Kigogo na Kihehe, walisema mnyama huyo ni nadra kuonekana na kila anapoonekana huweka vitu fulani ili aweze kutabiri mwenendo wa nchi au eneo fulani.
Mmoja wa wazee waliofanya tambiko hilo, Daniel Magomba, alisema Kakakuona huyo alitabiri uwepo wa mvua katika maeneo hayo jambo ambalo linawafanya wakazi wa maeneo hayo kuwa na uhakika wa kulima pamoja na uwepo wa maji katika bwawa la Mtera ambalo husaidia kuzalisha umeme.
Alisema kuwa hii ni mara ya tatu kwa eneo hilo kumuona Kakuona ambapo katika miaka hiyo mitatu waliweza kuwa na mvua nzuri zilizozalisha umeme pamoja na wakazi hao kupata mazao mengi.
Mazoea Nyalinde, alisema baada ya kuonekana kwa Kakakuona huyo walimuwekea kitambaa cheusi, unga, maji na mafuta ya kondoo ambavyo vyote kwa pamoja kila kimoja kina umuhimu wake.h.sep3.gif

 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom