TANESCO, Wizara ya Nishati zachunguzwa na PPRA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANESCO, Wizara ya Nishati zachunguzwa na PPRA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Aug 6, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,039
  Likes Received: 37,823
  Trophy Points: 280
  Mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya umma PPRA imeanza kufanyia uchunguzi mchakato wa zabuni wa kununua mafuta mazito uliosababisha mvutano kati ya TANESCO na wizara ya Nishati na Madini.

  PPRA itachunguza mchakato uliotumiwa na wizara ya nishati na madini kuipatia kampuni ya PUMA zabuni ya kusambaza mafuta mazito wakati mchakato wa zabuni hiyo ulikwisha kamilika.

  Lakini PPRA pia itachunguza utaratibu uliotumiwa na TANESCO kuipatia zabuni kampuni ya Oryx.Afisa mmoja wa PPRA amesema wizara nayo lazima ichunguzwe ni kwanini ilikubali kuipa zabuni kampuni ya PUMA nje ya taratibu zilizoanishwa kisheria.Afisa huyo alisema kuwa ktk swala la zabuni kuna taratibu na wao PPRA kinachowafanya waichunguze wizara ni kutaka kuona huyu mzabuni(PUMA) aliyekuja nyuma kushawishi ni taratibu gani zilitumika kumpa zabuni.

  Vyanzo vya habari kutoka ndani ya mamlaka hiyo vinatilia shaka uadilifu wa kampuni hiyo ya PUMA ambayo seriali ina ubia kutokana na hatua yake ya awali kugoma kuuza mafuta kwa bei ambayo iliwekwa na serikali.

  Source:Gazeti la habari leo la tarehe 06/08/2012.
   
 2. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  hana jipya hapo! La msingi ni kufukuza CCM madarakani. tutachunguza sana!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 3. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Another Bongo Movie! Let's wait and see.
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  Hao PPRA walikuwa wapi kuichunguza TANESCO wakati Umeme unakatika katika bila sababu za kuridhisha yaani

  Wanasubiri mpaka wanapewa Mwelekeo wapi pa kwenda? Sasa hapo si kubeba Per DM za kuiba? sababu BUNGE

  Wanafanya Uchunguzi; Takuhuru wanafanya Uchunguzi; CAG wanauchunguzi; Tanesco Wanauchuguzi wa Ndani

  POLISI wanafanya Uchunguzi... Sasa na Hao PPRA ... HUU NI ULAJI WA STYLE... PER DM's...

  NI KUFILISI TANGANYIKA... WOTE HAO MATUMBO MAKUBWA...
   
 5. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,039
  Likes Received: 37,823
  Trophy Points: 280
  Sina imani kabisa na uchunguzi wa bunge kwenye hili sakata.Lile bunge liko kisiasa zaidi na linaweza kupotosha ukweli kulinda watu wachache.Jiulize ile taarifa ya kamati ya bunge ya huduma za jamii kuhusu mgomo wa madaktari imeishia wapi?
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Hivyo Vyombo Vyote Vya Uchunguzi havifai kama waka serious walete Interpol... Itasema Ukweli Kabisaaa
   
Loading...