TANESCO wilaya ya Kibaha ni wababaishaji sana

luangalila

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
6,325
6,866
Waziri Makamba Ukipata wasaa wa kupitia UZI huu basi usisite kutembelea hii ofisi ya TANESCO Kibaha.

Wiki mbili zilizopita nilifika ofisi ya TANESCO Kibaha nikirejesha fomu yangu ya maombi ili niweze kupangiwa Surveyor, nikiwa pale ofisini kwao nikaona Tangazo ambalo lilihusu upimaji (surveyor) kwa kata tofauti kwa nyumba ambazo zinahitaji huduma hizo, basi nikalipitia tangazo lile na niliona katika kata yangu walipanga kulitembelea Tarehe 19 ya Oktoba kwa maana ya juzi hapa.

Kufika hiyo 19 Oktoba hawa jamaa hawakuonekana ktk eneo husika , nikasema pengine kwakuwa ni sikukuu basi watakuwa wamesogeza mbele tarehe kwa maana tarehe 20, ikafika tarehe 20 hawa jamaa pia hawakufika katika eneo husika.

Ni wazi huu ni ubabaishaji wa kiwango cha juu mnoo.
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
 
Tanesco kabindi, biharamulo umeme kila Siku unakata siku nzima au usiku mzima. Kazi zetu zinafeli sna.
 
Tanesco kabindi, biharamulo umeme kila Siku unakata siku nzima au usiku mzima. Kazi zetu zinafeli sna.
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora
Teh teh shuguli inakuwaga hapa sasa

Ova
 
Makamba inabidi afumue Tanesco nzima ,wanafanya kazi kwa mazoea,waziri anasema nguzo zipo,meter zipo lakini ukishalipia hakuna kinachoendelea unaambiwa subiri zamu yako, sasa usubiri zamu gani wakati kupata control number tu inachukua zaidi ya miezi 6...Then ukipata na kulipia unaambiwa usubiri tena.

MAKAMBA MAKAMBA MAKAMBA nimekuita mara tatu, Pangua wababaishaji wa Tanesco Pangua Management ,Pangua Operations Managers wote, Pangua Zone Managers Wote, hao ndio wanaohujumu TANESCO, hao ndio wezi na wababaishaji.

Ndugu yangu alifanyiwa survey na tanesco mwezi wa pili, control number imetoka mwezi huu wa 10 yaani amesubiri miezi 8 ndiyo akapata control number, ameshalipia tena anaambiwa meter na nguzo hakuna huu ni ubabaishaji wa kiwango cha lami...Kalemani alitumiambia wana nguzo zaidi ya milioni 2 store.
 
Makamba inabidi afumue Tanesco nzima ,wanafanya kazi kwa mazoea,waziri anasema nguzo zipo,meter zipo lakini ukishalipia hakuna kinachoendelea...
Je umelipia lini? Jina Wilaya na namba ya simu? Tunaendelea kuwafungiwa wateja wetu umeme kwa mfumi wa wa kwanza kulipoa wa kwanza kufungiwa.

Aidha kumekuwa na ongezeko kubwa la wateja kutokana na kushuka kwa gharama za kuunganishia wateja umeme
 
Wabunge walishauri Tanesco isifanye kazi zote tatu peke yake ,ingependeza wa outsorce kazi wabakiwe na moja tu.

Tanesco hao hao wazalishe, wasambaze, wauze....Wajikite na kazi moja tu, wamemonopolise soko!! Ingependeza Tanesco wabakie na kazi ya Kuuza tu, Production na transimission wafanye makampuni binasfi au maruhusu makampuni mengine yaingie sokoni,yazalishe umeme kwa wingi, yazalishe meter, nguzo kwa wingi wawauzie tanesco.
 
Je umelipia lini? Jina Wilaya na namba ya simu? Tunaendelea kuwafungiwa wateja wetu umeme kwa mfumi wa wa kwanza kulipoa wa kwanza kufungiwa,Aidha kumekuwa na ongezeko kubwa la wateja kutokana na kushuka kwa gharama za kuunganishia wateja umeme

Ngoja nimpigie simu awawasiliane na nyinyi, Survey amefanyiwa mwezi wa pili ,control number imetoka mwezi wa 10 means amelipia mwanzoni mwa mwezi wa 10, sasa kama mnatumia mfumo wa FIFO(First In First Out), kama amelipia mwezi wa 10 mnapanga kumfungia umeme lini?

Kama nguzo zipo, kama meter zipo yanini mtu asubiri miezi mitatu ndio aunganishiwe kisa eti ni foleni,mpo serious kweli?

Kama hamna resources ajirini wafanyakazi wafanye kazi ya kuwaunganishia umeme kama maombi ni mengi ,ajirini watu kwa mkataba hata wa mwaka mmoja mmoja ili watu wafuunganishiwe haraka umeme...Kama maombi ni mengi outsource kazi kwa subcontractor wafanye kazi kwa wakati.

Ndio maana nikasema Makamba afukuze Operations na Zone Managers wote maana hawajui wanachokifanya,hawapo kuisaidia serikali wala kuisaidia jamii ,wewe ushaona maombi yameongezeka inabidi uwe na plan ya kuwahudumia wateja kwa uharaka.
 
Ngoja nimpigie simu awawasiliane na nyinyi,Survey amefanyiwa mwezi wa pili ,control number imetoka mwezi wa 10 means amelipia mwanzoni mwa mwezi wa 10...
Mpaka sasa haujatoa taarifa tulizoomba hivyo bado hatujui tukujibu kwa taarifa zipi haswa, tafadhalo toa ushirikiano
 
toka ofisini hapo, njoo Tanesco Chanika utajua naongelea nini
Tunawasihi wateja wetu ifike hatua tujali na kuheshimu watoa huduma, Ni vema unapoandika au kulalamika utoe ushirikiano kwa kuwa hata ukifika ofisi husika unapaswa uwe na taarifa za kuanzia.

Tunatambua Chanika ni Wilaya mpya yenye maombi ya umeme mengi sana hivyo ni kweli kabisa jitihada zinaganyika kuhakikisha wateja wote wanapatiwa huduma.

TUNAENDELEA kusisitiza utoaji wa taarifa kamili.
 
Tuma sasa tunakujibu mara moja
Tanesco nina swali
Nyumba inadaiwa umeme mil 7 mzee ndio alifanya huo uhuni na amefariki tunalipa laki moja kila mwezi ili tununue umeme je nyumba hii inaweza ikaombewa mita nyingine kwa ajili ya wapangaji huku tukiendelea kulipa hiyo laki moja ya kila mwezi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom