Tanesco watimuliwa na wafuasi wa kanisa la full gospel bible fellowship. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco watimuliwa na wafuasi wa kanisa la full gospel bible fellowship.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kitomai, Feb 18, 2010.

 1. Kitomai

  Kitomai JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,058
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Leo asubuhi watumishi wa shirika la umeme Tanesco walifika katika mbele ya kanisa la Full Gospel Bible Fellowship kwa nia na madhumni kuendeleza zoezi la kusimika nguzo kwa ajili ya umeme. Mara baada ya kufika hapo walikutana na kigingi cha waumini ambao idadi yao inaaminika kufikia mia mbili.
  Muda mchache baada ya kutimuliwa jeshi la polisi lilikaingia. Haikujulikana mapema ni nani aliyetoa taarifa hizo kwa jeshi hilo.

  Kiongozi wa kipolisi aliyeambatana na jeshi hilo aliingia ndani kwenda kufanya mazungumzo na uongozi wa kanisa akiwapo askofu Mkuu Zakary Kakobe.

  Baada ya hayo mazungumzo Akofu Mkuu Zakary Kakobe alijitokeza nje na kuanza kuhojiwa na jopo la waandishi wa habari waliokuwapo hapo kwa ajili ya kushuhudia zoezi hilo. Wakati anahojiwa na waandishi polisi waliokuwa katika magari maarufa kama ‘’defender’’ na wale waendesha pikipiki maarufu kama ‘’tigo’’waling’oa nanga kuodoka katika eneo hil.


  Askofu Mkuu Zakary Kakobe alianza kwa kusema‘’ Mazungumzo bado yanaendelea baina yetu sisi na serikali, sisi tunaamini serikali haiwezi kuwa chanzo cha vurugu, ni jambo la uzuni sana kuona kuna kikundi kidogo cha watu wachache, sasa tunataka kuja hilo kundi la watu wachache ni hakina nani hao”.
  Akiongea kuhusu madhara ya huo mradi Askofu Zakary Kakobe alisema, ‘’Mradi huu una heath hazard, una madhara kwa afya ya binadamu, nguzo hizi zinatakiwa kupitishwa umbali wa mita 7.5 kutoka katika makaazi ya watu’’.

  ‘’ Athari za huu umeme kupita karibu na makaazi ya watu, ni pamoja na wanaume wanaweza kupoteza nguvu za kiume, na wanawake mamba zinaweza kutoka ’’

  Akiongea kwa ufasaha kuhusu uhalali wa mradi wenyewe, Askofu alisema, ‘’ kisheria umma lazima ushirikishwe katika hatua za awali kitu ambacho hakikufanyika, mimi kama msomi nalijua hilo na nina pambana nao kisomi’’.

  Kuhusiana na idadi ya watu waume kwa wake wanaokuwepo hapo masaa 24/7 ambao idadi yao inakadiriwa kufikia 200, kuhusiana mustakabari wa kutokuwa na kazi za kufanya, na ni nani anawalipa kwa kufanya hiyo kazi. Askofu alikuwa na haya ya kusema’’ Hawa wana kazi zao za kufanya, kanisa hili lina waumini 10,000. Hapa wanafanya kazi kwa kujitolea, kuna shift 6 A, B, na C. Wapo hapa kwa ajili ya kulinda maslahi yao, tayari tuna mradi wa runinga, wameshachanga million 800, mradi huu sasa umekwama kwa kitisho na chokochoko za Tanesco’’.

  Hiyo ndiyo habari kwa ufupi.
   
 2. l

  libaba PM Senior Member

  #2
  Feb 18, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  UMOJA wao ndio silaha yao , utengano wao ndio maangamizo yao. na hili liwe somo na kwawengine wote kuwa tunapaswa kutetea haki zetu hata kwa nguvu, maana serikali hii imethibitika kuwa haijali afya zetu
   
 3. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 925
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  Hii ni breaking news, au ndiyo habari yenyewe!
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,231
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Whatever you may take it to be Kyachakiche!..(nimemaliza na wewe)!

  Ni kweli maendeleo ya nishati yanahitajika, lakini kitendo cha kutaka kutumia ubabe kwa mtu ambaye anaendesha shughuli yake, in this case kanisa, kihalali , ni mbaya sana.

  Kakobe, tumia machinery yoyote unayoweza, ili at least haki na usawa vitendeke juu ya eneo lako unalomiliki kihalali na kulilipia!

  Richmond imewashinda 'miserably' hawa!
  Full support from the masses!
   
 5. Kitomai

  Kitomai JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,058
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Ndiyo habari yenyewe. Imetokea leo asubuhi. Cha msingi hapo ni hizo hoja zinazotolewa na kanisa. Hiyo hoja ya mita 7.5 kutoka katika makaazi ya watu na madhara ya kupitisha umeme mkubwa katika makaazi ya watu kinyume na utaalamu unaopaswa kuzingatiwa. Hapo kuna mambo ya mipango miji. Je, ni lini serikali iliuweka huo mpango na wadau walishirikishwa vipi.
  Matharani ukiangalia masta plan ya jiji la Dar es Salaam ya mwaka 1978 utaona pametengwa maeneo 80 kama open space kwa ajili shughuli mbalimbali za kimaendeleo na michezo. Kwa mujibu wa ripoti ya rushwa ya tume ya Jaji Warioba ya 1994, tayari maeneo 70 yalikuwa yamechukuliwa yapo mikononi mwa miliki ya watu binafsi, yakimilikiwa kisheria kwa maana yana hati miliki. Nani wakulaumiwa hapa serikali au wananchi?
   
 6. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 17,559
  Likes Received: 5,123
  Trophy Points: 280
  Kati ya wanaolinda maeneo yale, wapo ambao nguzo kama zile zinapita majumbani mwao.....................
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 42,021
  Likes Received: 37,327
  Trophy Points: 280
  Hivi nani kashika mpini?
  Tanesco au serikali?
  Mwamuzi wa kweli ni muda tu.
  time will tell
   
 8. Kitomai

  Kitomai JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,058
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Tunahitaji watalaamu wa afya mazingira watuelimishe juu ya hili. kama kweli hayo madai yanayotolewa na hilo kanisa yana ukweli iweje sehemu nyingine wamekaa kimya. Tuseme nini, wamekubali kwa kwa shingo upande au hawana ubavu wa kupambana na serikali hata kwa njia ya kutumia mahakam?
  Mimi ni mpenda maendeleo maoni yangu serikali ingeweka hadharani faida na hasara za huo mradi kwa manufaa ya wadau wote.
   
 9. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,834
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 180
  I'm simply tired!

  TANESCO why don't you call OFF this entire Project and let be what may be?

  Richmond came and "passed away" so is Kakobe - Why worry?

  Acheni Kakobe aweke TV station na nyie mkatie umeme for 6 months - akiwauliza mwambie umeme wa kukupatia hatuna kwa maana ulituzia kukuletea umeme - BASI
   
 10. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 30,307
  Likes Received: 29,018
  Trophy Points: 280
  nafikiri kakobe anajua yuko right ndio maana anajiamini na serikali haiwezi kufanya chochote bali kunegotiate,hii ni changamoto kwa watu wengine kutetea haki na maslahi yao,kuna watu wanakubali kuweka minara ya simu(tigo,voda etc) kwenye nyumba zao bila kujali long term health hazard they expose themselves to.
   
 11. M

  Mundu JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,720
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi kwa mfano ikienda ile gari yenye maji ya washa washa, afu ikanyunyiza maji aste aste. Hao jamaa watagangamala hivyo hivyo kweli? Au wana test zali?
   
 12. Kitomai

  Kitomai JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,058
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Mamlaka ya nchi, Bunge na Mahakama ndiyo vyombo vikuu vitatu vya juu vilivyoshika mpini. Si umeona hivi majuzi Bunge kwa kuzingatia hoja ya serikali likatunga sheria ya kumkataza mgombea binafsi. Lakini Mahama ikayabatirisha maamuzi ya Bunge na Serikali na mpaka sasa serikali ipo mtegoni kama si kikaangoni
   
 13. Kitomai

  Kitomai JF-Expert Member

  #13
  Feb 18, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,058
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Hauitajiki kuwa mnajimu kujua kitu gani kinaweza kutokea pale. Mimi nimeshuhudia live mori walionao wale jamaa. Wenzako wanaamini ukiwauwa wakati wakiwa katika hizo harakati wanakwenda peponi.
  Kazi itabaki kwa wale waliotoa maagizo kuandaa ripoti itakao waridhisha wanasiasa ili wasitolewe kafara.
  Lile ni jeshi la watu 10,000 unatakiwa kuwa mwangalifu sana unaposhughulikia suala kama hilo. Tumia busara zaidi kuliko nguvu siku zote. Matumizi ya nguvu wakati mwingine yanaashiria ni kwa kiwango gani una IQ ndogo.
   
 14. Kitomai

  Kitomai JF-Expert Member

  #14
  Feb 18, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,058
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Huo ndio ujinga kakobe na kanisa lake wanaukataa.
   
 15. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #15
  Feb 18, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,717
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Hao wanaokesha pale eti kupinga nguzo zisipite majumbani mwao mbona zmepita na hajapinga waacha ushabiki wakijinga, serikali ikiamua kufanya shughuli zake kamwe watu hamuwezi kupinga baada ya muda utasikia pale sio sehemu halali ya kakobe amejenga kimakosa kanisa ile ilikuwa open spaace kwa ajili ya watoto kucheza linaletwa likijiko kam kipawa sinema imekwisha.
  Pili naona hao watu wanaoshinda pale hawana kazi za kufanya hivi kama wangekuwa ni waajiriwa wangasubutu kwenda kshinda pale kisa wanapigania haki ya kanisa subutu yao hao wote ni majobless ndio maana wanapata muda wakwenda uza sura zao pale, na hao wakinamama hivi nao wamekosa hata kazi ya kufanya majumbani mwao kazi kushinda barabarani eti kisa kanisa watoto wanashikwa utapiamlo,kwashakoo kisa mama kaenda zamu yakulinda kanisa tanesco wasije pitisha nyaya za umeme.
   
 16. Kitomai

  Kitomai JF-Expert Member

  #16
  Feb 18, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,058
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  sina uhakika na hilo. kinachoonekana pale wale walinzi wasio na siraha wanaonekana wamevaa uniforms za kanisa
   
 17. K

  KAPONGO JF-Expert Member

  #17
  Feb 18, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,397
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kakobe anatumia kigezo cha dini kukwamisha mradi halali wenye manufaa kwa umma. Atake asitake its a matter of time umeme utapita tu katika eneo hilo na hakuna madhara yatakayowapata waumini wake....issue ya kakobe ni kuchukizwa na ukweli kuwa mabango yake mawili makubwa aliyoyasimika nje itabidi yang'olewe ili kupisha line ya umeme...si atafute mahali mbadala ili umma ufaidike na mradi unaokusudiwa.
   
 18. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #18
  Feb 18, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 429
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hivi watu wanaoshabikia kupitishwa kwa umeme wa 132kV mita chache au karibu kabisa ya majumba wanafikira madhara yake sawasawa.

  Hebu fikiria hawa "reckless" drivers wetu siku moja wakavaa hizo nguzo na huo umeme ukaangukia juu ya nyuma si itakuwa kizaa kikubwa sana. Achilia mbali madhara yanayosababishwa na strong electromagnetic field, mfano mmoja ambao nimewahi jaribu ni kuwa ukipita chini ya laini za 33kV na radio yako ay AM huwa inakata mawasiliano kabisa. Sasa imagine kuwa exposed kwenye EF ya 132kV day in day out kwa miaka kadhaa.

  Kinachoonekana ni kuwa Tanesco na Serikali hawajali kuhusu hilo kwa sababu hawatadhurika.
   
 19. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #19
  Feb 18, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160

  Hebu iangalie kwanza ile himaya ya kanisa la FGBF kwanza kisha ufanye mahesabu madogo tu, ukishapata kiasi cha unit za umeme zinazotumika na majengo ya kanisa na ukajua ni shiligi ngapi kanisa linalipa tanesco kwa ajili ya huduma ya umeme, hapo ndio utakapogundua kwamba tanesco wanaweza au hawawezi kukata umeme.

  Nijuavyo mimi kwa hali ilivyo kanisa la kakoehaliwezi kukatiwa umeme based on sababu ya huu mradi.

  Hata hivyo, kama ikitokea wale jamaa wanao uwezo wa kununua jenerator la kuwasaidia kuendesha shughuli zao kama kawaida.
   
 20. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #20
  Feb 18, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Waumini wa Kakobe waendelee na msimamo huo huo mpaka mwisho wake
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...