TANESCO wasipandishe viwango vya bei ya umeme

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,480
30,152
Hivi karibuni TANESCO walieleza azma yao ya kutaka kupandisha bei ya umeme, kwa asilimia 67, kutoka shilingi 195 kwa uniti moja hadi 332 kwa uniti moja.

Kitu kimoja ambacho kiko wazi ni kuwa,wakati wowote, panapotokea upandishwaji wa bei ya umeme, maana yake huduma mbalimbali na bidhaa zote zinazozalishwa viwandani,huwa vinapanda bei.

Hebu tuangalie sababu zinazotolewa na TANESCO na Wizara ya Nishati, kuhusu upandishwaji huo, sababu kubwa wanayotoa, ni gharama kubwa wanazozipata TANESCO, katika kugharimikia kununua umeme kutoka kwenye mitambo ya kukodi, ambayo inaendeshwa kwa kutumia gesi na mafuta mazito.

Tulimsikia waziri mdogo wa Nishati,George Simbachawene, majuzi alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha mapambazuko cha radio one, akidai, kupandishwa kwa viwango hivyo ni lazima, kwa kuwa gharama za uendeshaji za shirika la umeme la TANESCO, zimekuwa kubwa sana, na akadiriki hata kuwakashifu watanzania kuwa, yeyote atakayeshindwa kumudu gharama hizo, ni bora akajiwashia kibatari, au akaamua kukaa gizani!!

Waziri huyo Simbachawene, alikitumia kipindi hicho kuwadanganya watanzania, kuwa gharama za umeme za Tanzania zipo chini, kuliko nchi yoyote barani Afrika!!

Huo ni uwongo wa dhahiri, kwa kuwa inafahamika wazi kuwa zipo nchi kadhaa barani Afrika, ambazo zinatoza viwango vya chini sana, ukilinganisha na nchi yetu.

Nitazitaja baadhi ya nchi hizo, ambazo ni Afrika ya kusini, Botswana, Namibia, Mauritius, Ghana na Libya.

Unajua tatizo kubwa la viongozi wetu, badala ya kueleza ukweli kuhusu tatizo la sekta ya umeme, huwa wanatafuta sababu za kuchomeka chomeka. Siyo siri tena kuwa tatizo la hali ya umeme hapa nchini huwa "inatengenezwa" na watawala wetu kwa manufaa yao binafsi.

Kwani nani hajui kuwa mitambo mingi ya umeme wa kukodi, wanaomiliki mitambo hiyo, ni hao hao vigogo wa serikali ya CCM. Kwa kuwa hatujasahau wakati ilipotokea kashfa ya Richmond, hadi kupelekea mawaziri wanne, kujiuzulu, akiwemo aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowassa.

Vile vile bado waTZ, hatujasahau namna JK alivyojitahidi kuwakana Richmond/Dowans kuwa hawajui wamiliki wake, hadi pale alipoumbuliwa na "best" wake, mzee wa mamvi, alipomwambia LIVE kwenye kikao cha NEC, akanushe ikiwa kuna jambo lolote alilokuwa akilifanya kama PM, kama kuna jambo lolote, hakuwa hi kumhusisha JK, akiwa kama mkuu wa nchi!!

Hivi watz, tujaribu kujiuliza, inakuwaje kwa mfano nchi yetu imejaaliwa na Mwenyezi Mungu, kuwa na makaa mengi ya mkaa ya mawe, hapo hapo mtambo wa umma, wa Kiwira, wenye uwezo wa kuzalisha umeme wa megaweati 400, ukawa umetelekezwa kabisa?!!!

Ni dhahiri basi watawala wetu mara nyingi, huwa wanatutengenezea "artificial shortage" ya umeme, ili waungurumishe mitambo "yao" ya umeme ili wazidi kutukamua waTz.

Kwani si tunakumbuka namna mtambo wa Richmond, ambao baadaye ulijigeuza jina na kuitwa Dowans, na hivi sasa unaitwa mtambo wa Symbion, namna wakati ule,walipa kodi wa nchi hii, tulivyokuwa tunawalipa, shilingi milioni 150 kwa siku, hata kama siku hiyo hawajawazalishia TANESCO hata uniti moja!!

Kwa hiyo ni muhimu watanzania wote tuamke, na kuwakatalia watawala wetu, njia zao za ujanja ujanja, za kutaka "kutuibia"

Watanzania tunapaswa kuiga mfano wa wananchi wa Zambia, ambao wao, hata ikitokea nyongeza ya shilingi 100, kwenye unga wa sembe au mkate, huwa wanafanya maandamano, hadi serikali yao, huwa inasalimu amri na kushusha bei ya bidhaa hizo.

Kama wananchi wa nchi nyingine kama Zambia huwa wanaweza kuzikataa, dhuluma wanazofanyiwa na watawala wao, inakuwaje sisi watanzania tushindwe, na tukubali kukandamizwa na watawala wetu, milele na milele?!!!!
 
Mkuu,
Mimi binafsi chili jambo la Tanesco limeniuma sana,hasa kauli ya Naibu Waziri.
 
Nimefurahi pale Waziri mwenye mamlaka anaposema ukishindwa kumudu gharama "washa kibatari" natafakari kauli hii hivi wananchi wa jimboni kwake wanajisikiaje?
 
Back
Top Bottom