TANESCO wanataka ninunue transformer

Mi nadhani utakuwa na load kubwa, nikiwa na maana unahitaji umeme mwingi na hicho ni kitu Cha kawaida kwa kwa wateja wenye uhitaji wa umeme mwingi ( high power demand) mfano viwandani, apartment s, Malls etc Mara nyingi hawa hufunga transformer zao kulingana na mahitaji yao. Cha kufanya hapo tafuta mkandarasi wa umeme anayetambulika na tanesco aje afanye tathimini ya ukubwa na specification ya transformer inayotakiwa kwa mahitaji yako na vifaa vingine (auxiliaries) vinavyoambatana na hiyo transformer itakayowekwa pamoja na kuifunga mahala pake. Baada ya hapo utaomba kuungwanishwa umeme na tanesco kupitia msongo wa juu kidogo wa usambazaji (11kV secondary distribution line)

NB: Kiufundi na kiuchumi wa usambazaji wa umeme, kwa mteja/ mtumiaji mwenye uhitaji mkubwa wa umeme itakuwa ni hasara kwa tanesco ( au Kampuni nyingine ya kusambaza umeme) kuwajibika kumfungia mteja transformer yake peke yake. Kwa hiyo mteja atawajibikia kufunga transformer yake kupitia mkaandarasi anayetambulika na tanesco.
 
Habari, Mimi ni mkazi wa Morogoro vijijini. Biashara yangu ni ya kukoboa zao(silitaji kwa sababu binafsi) ni mwaka wa tatu sasa nafuatilia kuwekewa umeme katika kiwanda hichi kidogo maana natumia diesel lakini gharama nnazopewa ni zaidi ya milioni kumi, ikiwemo na kununua transform.

Wataalam hili suala limekaaje maana nashindwa kuelewa. NINUNUE transformer kivipi wakati ni wajibu wa TANESCO kutupatia huduma kwa malipo husika ya huduma hi.. na ugumu wa kuwekewa umeme unakuja wapi jamani. MSAADA
Mkuu, hicho kiwanda chako kidogo kina LOAD ya kiasi gani?
 
Asante sana kwa ushuhuda wako, tupo kuwahudumia
Mkuu Kama tunahitaji kuvuta umeme na laini ya Umeme wenu wa Tanesco upo barabara kuu ya lami na kuuleta kwenye site yetu ni Kama 800 meters umbali toka lami, je gharama ya kuvutiwa umeme itakuwa kiasi gani, maana tuna makrasha ya kusaga mawe tunatumia diesel ambayo ni gharama ikizingatiwa mafuta yamepanda bei.
 
Kwa mfano wewe umeenda ukaambiwa kwa mdomo, je utawalazimisha wakupe barua, hakuna sehemu nimeseme KIMASHINE acha kuedit nlichosema, ndio mashine za kukoboa zinahitaji transformer.

Uso ila hujui ladha yake
 
Mkuu Kama tunahitaji kuvuta umeme na laini ya Umeme wenu wa Tanesco upo barabara kuu ya lami na kuuleta kwenye site yetu ni Kama 800 meters umbali toka lami, je gharama ya kuvutiwa umeme itakuwa kiasi gani, maana tuna makrasha ya kusaga mawe tunatumia diesel ambayo ni gharama ikizingatiwa mafuta yamepanda bei.
Hii mnashauriwa kusubiri miundimbinu ya umeme uwafikie
 
Hii mnashauriwa kusubiri miundimbinu ya umeme uwafikie

Aiseee inasikitisha sana!! Miaka zaidi ya 60 ya Uhuru bado Tanesco inasuasua kupeleka umeme ,tatizo ni monopoly,kungekuwa na kampuni nyingine ya umeme nadhani mngezinduka kutoka usingizini.
 
Aiseee inasikitisha sana!! Miaka zaidi ya 60 ya Uhuru bado Tanesco inasuasua kupeleka umeme ,tatizo ni monopoly,kungekuwa na kampuni nyingine ya umeme nadhani mngezinduka kutoka usingizini.
Utakuwa shahidi kuwa maeneo mengi nchini yamefikiwa na umeme na tunaendelea kusogeza miundombinu kwa awamu.
 
Halafu ikitokea ukalipia baadaye watawasambazia watu umeme kwa kutumia transformer uliyolipia bila kurudishiwa chochote, kuna maeneno mtu anaambiwa anunue nguzo akitaka umeme, we umenunua nguzo baadaye wanatumie nguzo hiyo kuvuta umeme kwa wengine wakati we uliyelipia nguzo hupewi chochote, utaratibu wa hovyo sana.
Naomba kujua kwamba wewe wakati unachukua umeme kwenye nguzo ya jirani uliwajibika kumlipa jirani kwakuwa yeye alisogeza umeme au wewe tu ndio unataka ulipwe kwakuwa jirani yako asiyekuwa na umeme amechukulia kwako?
 
Back
Top Bottom