TANESCO wanainyanyapaa ROMBO; Kwa kuwa tulichagua wapinzani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANESCO wanainyanyapaa ROMBO; Kwa kuwa tulichagua wapinzani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tuko, Apr 29, 2011.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Apr 29, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ni takribani miezi mitano sasa TANESCO ROMBO office hawaunganishii wateja wapya umeme. Wamekuwa na visingizio mara hamna nguzo, mara hamna nyaya, mara mita n.k. na wanasema kuwa hawapati vifaa hivyo kutoka TANESCO mkoa.

  Nimewasiliana na watu waliopo wilaya nyingine kama Moshi vijijini, Same, Mwanga wanasema kuwa vifaa wanavyo tena vingi japo hawana maombi mapya.

  Imebidi nijiulize, Je, ni kwa sababu tulichagua mbunge wa Upinzani? Madiwani wamekuwa kimya na hawana majibu ya maana wanapoulizwa kuhusu tatizo hili.
  Naomba mamlaka husika zifuatilie, kwani siasa isihusishwe na maendeleo.
   
 2. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #2
  Apr 29, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ni meize mitano sasa TANESCO haiunganishi umeme kwa wateja wapya ROMBO. Wamekuwa wakitoa sababu kuwa ni ukosefu wa vifaa; mara nguzo, mara nyaya, mara mita nk.
  Kukosekana kwa vifaa ni kitu cha kawaida, lakini kinachozua mjadala ni kuwa iweje wilaya nyingine kama Moshi vijijini, Same, Mwanga wana vifaa na wanaunganisha kama kawaida kwa wanaoomba? Kama ingekuwa tatizo la kawaida, iweje lidumu kwa miezi mitano? Kinachosikitisha zaidi hata wale waliopokelewa malipo yao kuanzia mwezi wa kumi mwaka jana kabla hawajasitisha kupokea malipo, bado hawajaunganishiwa umeme.
  Hali hii imefanya watu waanze kujiuliza, Je, ilikuwa jinai kwao kuchagua mbunge wa Upinzani? Mambo ya maendeleo ya jamii yasihusishwe na siasa jama...
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Very sad kufanya mambo ya utendaji na huduma kwa wananchi kuwa za chama. Msikate tamaa, hili limewahi kuwapata watu wa Kigoma enzi hizo Ditopile mkuu wa mkoa, halafu walimchagua Kaburu wa CDM kuwa mbunge, hali ilikuwa mbaya! Hizi ndizo siasa za kizandiki zilizomea barani kwetu, tushirikiane kuwaondoa hawa.
   
 4. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  wapuuzi hao tuwazomee bdala ya kuwaunganishia wateja umeme wapate mapato wao wanaleta maringo?
  ikibidi mtaarifu mkurugenzi wa kanda uje kulikoni,jaribu kumwona pia wa wilaya rombo.
  poleni wamashati mkuu,tarakea.
   
 5. Dio

  Dio JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 1,278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wapuuzi hao
   
 6. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,348
  Likes Received: 1,145
  Trophy Points: 280
  hilo huenda ni amri ya chama cha magamba
   
 7. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,037
  Likes Received: 750
  Trophy Points: 280
  Ujinga mtupu,ndo tabu ya kuwa monopoly kwenye soko.
   
Loading...