Tanesco wanaendesha mitambo ya IPTL kwa tsh bilioni 15 kwa siku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco wanaendesha mitambo ya IPTL kwa tsh bilioni 15 kwa siku

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Observer2010, Mar 25, 2011.

 1. Observer2010

  Observer2010 Senior Member

  #1
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hii imenishangaza sana inakuwaje mitambo iendeshwe kwa gharama kubwa hivi ? Au hela zingine wanailipa Dowans kisilisili.

  Hebu angalia mahesabu rahisi.

  Tsh Bilioni 15 kwa siku zidisha na siku 365 kwa mwaka unapata Tsh Trilioni 5.475.

  Hivyo basi Tanesco wanaendesha mitambo ya Dowans kwa TSH Trilioni 5.475 kwa mwaka. Ukiangalia bajeti ya Tanzania mwaka 2010/2011 ni around TSH Trilioni 11.

  Hii hela ni nusu ya bajeti ya nchi nzima !!!
  :behindsofa::behindsofa::behindsofa:
   
 2. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hiyo hela hawana ya kuchezea kwa kiwango hicho
   
 3. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Mkuu, tunaomba chanzo cha habari hii tafadhali!
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Whaaat!!!
   
 5. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Maybe the guy has the key to basic info.. Can you prove that negro?
   
 6. Observer2010

  Observer2010 Senior Member

  #6
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hamjaikamata hii wadau ? Hizi ni habari toka TANESCO, nimesikia kwenye taarifa ya habari jana. Kwani hamjaona kamgao kidogo kamepungua ? Hii gharama inainclude ununuaji wa mafuta mazito ya kuendeshea hiyo mitambo.
   
 7. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mi binafsi sijaiona hiyo taarifa; yaani unamaanisha kabisa Sh 15 bln au walimaanisha Shs 15 mln! Duh! Tz ipo njia panda; kushoto simba kulia chui mbele nyoka na nyuma kuna mamba
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  chanzo kipi wakati mimashine ya IPTL inaunguruma na mgao umekwisha...sasa unataka source ya nini?
   
 9. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #9
  Apr 7, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  April 6th, 2011

  Wastani wa Bilioni 15.62 hutumika kwa kila mwezi kwa ajili ya kununulia mafuta ya kuendeshea mitambo ya IPTL ili kuzalisha umeme nchini.


  Akijibu swali bungeni leo Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alisema fedha hizo ni kwa ajili ya ununuzi wa tani zaidi ya 12,000 za mafuta mazito kwa mwezi.

  "Kiasi cha Sh bilioni 46.4 au wastani wa shilingi bilioni 15.62 kwa kila mwezi zinalihitajika kwa kugharamia ununuzi wa tani 36,800 za mafuta mazito (HFO) kwa kipindi cha miezi mitatu."Alisema.

  Alisema matumizi hayo yalitumika kuanzia Novemba 15, 2010 hadi Februari 14, 2011 ambayo ni sawa na tani 400 kwa siku.

  Alisema Kampuni ambazo serikali imekuqwa ikinunua mafuta hayo kutoka kwao ni Oryx na Total kwa kuwa ndizo kampuni pekee zinazofanya biashara ya mafuta mazito nchini.

  Alisema utaratibu uliotumika kupata kampuni za Oryx na Total ni kwa njia ya "Restricted Tendering" ambapo kampuni za mafuta zilitakiwa kufikisha mafuta maghala ya IPTL mwezi Novemba 2010.

  "Katika hali ngumu kama hiyo maamuzi ya serikali yalihitajika kufanyika haraka ili kupunguza ukali wa mgawo wa umeme kwenye mfumo wa gridi ya Taifa," alisema Ngeleja.

  Alisema fedha za kununua mafuta ya kuendeshea mitambo hiyo zimetoka kwenye mfuko mkuu wa Serikali.

  Aidha alisema mpango wa kubadilisha mitambo ya IPTL ili iweze kutumia gesi asilia badala ya mafuta alisema serikali haiwezi kufanyika kwa sasa kutoakana na kuwepo kwa kesi mahakamani.

  Alisema mara baada ya kumalika kwa kesi hiyo mahakamani serikali itafanya hivyo ili kuweza kupunguza gharama za uendeshaji.

  Alikuwa akijibu swali la Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini Chadema) aliyetaka kujua kiasi cha mafuta kinachonunuliwa kila mwezi kwa ajili ya kuendeshea mitambo ya IPTL.

   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,681
  Likes Received: 82,533
  Trophy Points: 280
  06 April 2011

  By Mkinga Mk§inga
  The Citizen Reporter


  The government has spent Sh46.4 billion from November last year to last February in buying furnace oil for the Independent Power Tanzania Limited. The average expenditure of Sh15.62 billion a month (Mhhhh! this is equivalent to T Sh 187.44 bilion a year!) had to be spent by the government in efforts to solve power shortage problems.

  This was revealed yesterday by the minister for Energy and Minerals, Mr William Ngeleja, in response to a question by the Kigoma North Member of Parliament, Mr Zitto Kabwe (Chadema). He said the money was used to buy 36,800 tonnes of furnace oil and the plant was using about 400 tonnes a day.

  Minister Ngeleja said funds to buy the furnace oil were sourced from the government. However, Mr Ngeleja asked for more time to get details as asked by the MP in his supplementary question.

  He said the cost was high because the plant used furnace oil. The government has been striving to make sure that the mechanism of the plant is changed to allow use of gas, he said, lamenting:

  “We could have switched to using gas but there has been a case in court…this conflict is costing the government.”

  Mr Zitto said the government was embracing IPTL projects on since there might be people benefiting from the problem.
   
 11. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #11
  Apr 7, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  na hapo hujajumlisha na capacity and other manadatory charges!! sasa hizo hela hadi mkataba wao wa miaka 20 utakapomalizika zisingetosha kujenga hata mabwawa zaidi ya maji kwa kuzalisha umeme?

  kama vichwa vya serikalini ndiyo hivi? hii nchi bora tu wakoloni wasingeng'olewa enzi za mwalimu
   
 12. m

  macinkus JF-Expert Member

  #12
  Apr 7, 2011
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 260
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  kwa bilioni 46 tungenunua majenereta mangapi?

  macinkus
   
 13. d

  donmzushi Member

  #13
  Apr 7, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  majenereta ya nini tutengeneze umeme wa upepo na solar tuu tuachane na mafuta and all energy ambazo tunanunua upepo ni bure na jua ni bure jamani na hivyo vyote tumejaaliwa sana haopa Tanzania.
   
 14. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #14
  Apr 7, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwa lugha rahisi ni kuwa mafuta ya kuendeshea mitambo ya IPTL yananunuliwa na serikali na baadaye serikali inauziwa umeme unaozaliswa kwa mafuta ya serikali. Je, kampuni ya IPTL imefanya jukumu gani? na je, bei ya kuuzia umeme ikoje?
   
 15. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #15
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Another bad news!!!!
   
 16. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #16
  May 5, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Vigogo wabanwa ufisadi mpya IPTL

  * Zitto awatuhumu kupata mabilioni
  *Takukuru yaanza kuchunguza

  Na Waandishi Wetu

  KUNA taarifa ya kuwa kuna kashfa mpya ya ufisadi inayonukia kuhusu mafuta ya mitambo ya umeme ya kampuni ya Independent Power Limited (IPTL) inayoweza kuwa inawahusisha vigogo serikalini.

  Kashfa hiyo ambayo tayari vyombo vya dola vimeanza kufuatilia kwa karibu, inahusisha matumizi yenye utata ya Sh bilioni 15 kila mwezi, fedha zinazotolewa serikalini kabla ya kuingia katika mfuko mkuu wa Hazina.

  Tayari Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) Zitto Kabwe, ameliomba Bunge kupitia Kamati ya Nishati na Madini, kufanya uchunguzi wa kashfa hiyo kwa kushirikiana na vyombo vya dola na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG).

  Wakati Zitto akitaka Bunge liunde kamati ya kuchunguza suala hilo, Raia Mwema limefahamishwa kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imekwisha kuanza kuchunguza suala hilo kwa kina.


  Imeelezwa kwamba TAKUKURU inachunguza taarifa za kwamba baadhi ya vigogo wakiwamo wanasiasa na watendaji serikalini wananufaika na mradi huo ambapo baadhi wanatajwa kupata bakshish ya fedha zinazotolewa kila mwezi na serikali kwenda IPTL.


  Vyanzo vya habari ndani ya Bunge vimeliambia Raia Mwema kwamba Zitto ameandika barua hiyo Aprili 11 mwaka huu, kwenda kwa Spika akipendekeza Bunge kuunda kamati teule kuchunguza suala hilo.

  Kumbukumbu za Bunge (Hansard) zinaonyesha kwamba suala hilo lilianzia Bungeni ambapo katika Mkutano wa tatu wa Bunge, Aprili 6, 2011, Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja alilithibitishia Bunge kwamba Serikali ilitumia zaidi ya Shilingi Bilioni 46 kununua mafuta ya kuendeshea mitambo ya IPTL tangu Novemba 2010 hadi Februari 2011.

  Katika barua yake kwa Spika Zitto alisema;

  "Waziri alikiri kwamba serikali ilitumia mfumo wa zabuni dharura na hivyo kuyapa makumpuni mawili ya
  Oryx na Total Zabuni ya kuagiza Mafuta mazito kwa ajili ya kuendesha mitambo ya IPTL. Fedha hii ni wastani wa Tsh 15bn kila Mwezi.

  "Kumekuwa na Manung'uniko kuhusiana na zabuni hii na hata kuletea hisia za rushwa miongoni mwa Maafisa wa Wizara ya Nishati na Madini na Kabidhi wasii Mkuu aliyeko Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) **ambaye ndiye msimamizi wa IPTL kwa sasa kufuatia amri ya Mahakama. Inawezekana kabisa kwamba kuna watumishi wa Umma ambao wanafaidika na tatizo la mgawo wa umeme kwa kuhongwa kutokana na zabuni hii ya mafuta mazito kwa ajili ya mitambo ya IPTL."

  Mtendaji Mkuu wa RITA Philip Saliboko, ameliambia Raia Mwema jana kwamba hana taarifa za kuwapo uchunguzi unaofanywa na TAKUKURU, pamoja na kuwa wakala unahusika katika mchakato wa kuisimamia IPTL.

  Saliboko alisema pamoja na RITA kusimamia IPTL, hawana mamlaka na wala fedha zinazotolewa na serikali hazipitii katika kwao na kwamba hata taratibu za ununuzi na maamuzi yote mazito hufanywa na serikali kuu moja kwa moja baada ya wao kutoa taarifa za upungufu wa mafuta katika mitambo ya kuzalisha umeme.

  Katika maelezo yake Zitto alisema kuna mashaka kuhusiana na utaratibu wa zabuni kama ulifuata sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004.

  "Ninaleta kwako ombi kwamba Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ifanye uchunguzi maalumu kuhusu zabuni ya uagizaji mafuta ya kuendesha mitambo ya IPTL. Uchunguzi huo, pamoja na mambo mengine, uzingatie malipo yote ambayo Kampuni za Oryx na Total zinafanya kwa watu mbalimbali kuhusiana na biashara hii. Malipo yote ya Kampuni hizi ya ndani ya nchi na nje ya nchi yachunguzwe na Maafisa wa TRA na CAG wakisaidiwa na PCCB (Takukuru)," inaeleza sehemu ya barua ya Zitto kwa Spika wa Bunge.

  Katika maelezo yake bungeni, Waziri Ngeleja alisema shilingi bilioni 46.4 au wastani wa shilingi bilioni 15.62 kwa kila mwezi zilihitajika kwa ajili ya kugharamia ununuzi wa tani 36,800 za mafuta mazito kwa kipindi cha miezi mitatu, kuanzia 15 Novemba, 2010 hadi 14 Februari, 2011 sawa na tani 400 kwa siku.

  Alisema kampuni mbili za Oryx na Total ndizo pekee zinazofanya biashara ya mafuta mazito nchini na ndizo zilizoombwa kushiriki katika mchakato wa ununuzi wa mafuta hayo, kauli ambayo imepingwa na baadhin ya wadau wa mafuta wakizitaja kampuni nyinginezo zinazofanya biashara ya mafuta hayo na kampuni za madini zinazoendesha mitambo ya umeme wa mafuta.

  "Utaratibu uliotumika kupata kampuni za Oryx na Total ni kwa restricted tendering ambapo, kampuni za mafuta zilitakiwa kufikisha mafuta katika maghala ya IPTL mwezi Novemba, 2010. katika hali ngumu kama hiyo, maamuzi ya Serikali yalihitajia kufanyika haraka ili kupunguza ukali wa mgawo wa umeme kwenye mfumo wa grid ya TAIFA. Fedha za kununua mafuta ya kuendeshea mitambo ya IPTL zimetoka kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali," alisema Ngeleja.

  Hata hivyo, Raia Mwema limethibitishiwa kwamba fedha hizo hutolewa katika akaunti ya makusanyo hata kabla ya kuingia katika mfuko mkuu, jambo ambalo linazidi kuibua utata kutokana na fedha hizo kutofuata taratibu za fedha za serikali na kuwapo ugumu wa kufanyiwa ukaguzi.

  Katika swali la nyongeza, Zitto alihoji; "Ni dhahiri kwamba shilingi bilioni 15 kwa mwezi ni fedha nyingi sana. Wakati tunapitisha bajeti ya Serikali mwaka 2010/2011 hapakuwa na provision yoyote ya bajeti kwa ajili ya mafuta kwa mitambo hii. Waziri alithibitishie Bunge ni katika vote gani na kama ni ya Wizara yake au Wizara nyingine yoyote ambayo tunapata fedha (mabilioni) haya kwa ajili ya kulipia mafuta haya?"

  Zitto alisema kila mwezi Tanesco wanalipa capacity charge ya zaidi ya* shilingi bilioni 3.6 kwa IPTL, fedha ambazo zinawekwa kwenye ESCO Account ambapo zimefikia zaidi ya shilingi bilioni 160.

  "Kumekuwa na malalamiko na maombi na hoja mbalimbali za kutaka mitambo hii igeuzwe kuwa gas na imilikiwe na* Serikali. Lakini mpaka sasa hakuna lolote ambalo limefanyika. Waziri haoni kwamba kuendelea mitambo hii kutumia mafuta kama hivi na bila utaratibu ambao labda mitambo hii imilikiwa na Serikali ni kuwa ni mradi wa watu wachache ambao wanafaidika na mafuta haya?" alihoji Zitto.

  Katika majibu yake, Waziri Ngeleja hakuwa na maelezo ya kutosha kuhusu zinakotoka fedha hizo na badala yake alisema, "nimuombe Zitto Kabwe kama anavyofahamu vizuri ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge suala hili ni la takwimu tunayo ofisi inayosimamia mambo yote ya Fedha, chini ya Wizara ya Fedha mimi na yeye tukutane baada ya kikao hiki ili tupeane taarifa kupitia Wizara ya Fedha."

  Ngeleja alisema kwa utaratibu uliopo fedha inayopaswa kulipwa kwa IPTL inalipwa kwenye akaunti maalum ESCO kwa sababu ya kuwapo mgogoro wa kisheria mahakamani na kwamba ni lazima kuwe na utaratibu maalum hadi hapo mgogoro utakapokuwa umekwisha.

  "Kwa nini hatujaweza kufanikisha azma ya Serikali ya kubadili ile mitambo kutoka kwa kutumia mafuta mazito kutumia gesi asili kilichotuchelewesha hapa ni huo mgogoro ulioko mahakamani kwa sababu ya mgogoro hatuwezi kuendelea zoezi hilo linahitaji kufanywa baada ya kupatikana hatma ya mambo ambayo yanabishaniwa mahakamani," alisema Ngeleja.

  Sekta ya nishati nchini imekuwa ikigubikwa na kashfa za mara kwa mara na mradi wa IPTL ndio mkubwa wa kwanza kuhusishwa na ufisadi ambao hadi sasa hakuna maelezo wala hatua zilizowahi kuchukuliwa dhidi ya wahusika kabla ya kuibuka kashfa nyingine katika miradi kama hiyo ikihusisha kampuni za Richmond Develepoment LLC na Dowans Holding Limited.
   
 17. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #17
  May 5, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Hapo ndipo Takukuru wanaponinogea....hawaanzi kazi mpaka wanasiasa wachokonoe!!theze shit* are in deep sleep!!
   
 18. M

  Mbwazoba Member

  #18
  May 5, 2011
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ufisi wo ni aibu kwa taifa,but oneday tutawaona mwisho waooooooo
   
 19. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #19
  May 5, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Takukuru walianza uuchunguzi kabla ya Zitto kusema ndio maana Zitto ametaka Bunge liwashirikishe katika uchunguzi pamoja na CAG
   
 20. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #20
  May 5, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Eh! kutumia hela ambazo hazijawekwa katika Rekodi ya hazina?Huu ni uzembe wa hali ya juu,hakuna dharura yoyote inayoweza kuhalalisha uzembe kama huu.Hili linahitaji uchunguzi makini.There is a sequence of Irresponsibility

  Corruption has grown to become a pampered monster in Tanzania. And rather than lead the way to moral rebirth, the government appears too eager to be seen condoning and even championing corruption. Several of its officials continue to be indicted daily for unethical conducts without any attempt on its part to initiate their probe and trial in an open court.

  What the government does at best is to merely disengage them, and watch them depart happily with their loot intact. In a country so wanting in transparency and honesty on the part of its elite and officials, many Tanzanians have been seduced by widespread bad examples in high places into the belief that sharp practices have become an acceptable route to survival.

  While grinding poverty squeezes the life out of millions of Tanzanians due to the administrative irresponsibility of those in the helm of affairs. Our political rulers, their families and cronies flamboyantly parade their ill-gotten wealth before the hungry masses as they swim in ostentatious profligacy.


  Ant-Graft bureau(PCCB) Or Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) failed us Miserably.They played a stumbling block role and failed to spearhead Tanzania's attempts to combat Corruption.Shame!
   
Loading...