Tanesco wamekaa kikao kuandaa waraka wa kuwalipa dowans.

Mtaka Haki

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
492
149
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya mwanakikao. Zinasema uongozi wa TANESCO wako leo wamekaa kikao wanaandaa waraka wa kuwalipa DOWANS. Ni Mungu tu aingilie kati hali ya nchi hii. Saa chache zilizopita bado walikuwa ndani ya kikao hicho.
 
yawezekana DOWANS washachukua hela yao zamani sana.... kikao cha nini sasa.... kuandika cheque au ....
 
Kwa hiyo TANESCO ndo wanalipa? kesi imeshaandikishwa mahakama kuu?
Waraka unaandaliwa kwenye kikao?...........waraka ni nini?
 
Nimesikia kuwa mkulu anataka hela hizo zilipwe kabla ya bunge kuanza kikao chake Februari ili Dowans isiwe issue tena.
 
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya mwanakikao. Zinasema uongozi wa TANESCO wako leo wamekaa kikao wanaandaa waraka wa kuwalipa DOWANS. Ni Mungu tu aingilie kati hali ya nchi hii. Saa chache zilizopita bado walikuwa ndani ya kikao hicho.

pesa yenyewe wanayo?kila mwezi wanavuta ruzuku
 
watu watafungwa ooooohhh ngojeni Bunge lianze, nani katoa mamlaka ya kulipa? Mkulo alisema wazi hazina haina fedha ya kulipa, meaning
alijua BUNGE likija hali ni mbaya, wait
 
Sijui TANESCO wameona nini huko. IPTL, RICHMOND, DOWANS nk. Sasa Riz 1 through some people na Sixtelecoms wanataka tenda za mradi wa kuuza vocha za LUKU na hao wengine kuuza umeme wa upepo (hewa?).
 
Nimesikia kuwa mkulu anataka hela hizo zilipwe kabla ya bunge kuanza kikao chake Februari ili Dowans isiwe issue tena.

JKK, a member in the LIST OF SHAME.
Good in pressurizing "fraudulence business'? IPTL? Bulyanhulu? Richmond (T) Ltd? Loliondo? Ruaha National Park? ...aaakhh NO!
 
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya mwanakikao. Zinasema uongozi wa TANESCO wako leo wamekaa kikao wanaandaa waraka wa kuwalipa DOWANS. Ni Mungu tu aingilie kati hali ya nchi hii. Saa chache zilizopita bado walikuwa ndani ya kikao hicho.

Huu ni wizi wa mchana peupe, kwa nini wasingoje bunge likae?????????? Wanalipa kwa budget ipi, imeidhinishwa na nani????????? Wote watakao husika wapelekwe mahakamani, bila kujali wamepewa amri na nani, watatajana huko mbele ya sheria. Sheria gani inaruhusu kutumia fungu kubwa la fedha bila kupitia bungeni au baraza la mawaziri??????????? CHADEMA nawaomba wainitiate vote of no confidence kwa huyo aliye toa amri, hata kama ni mkuu wa nchi he should be imperched. Si dhani kama CCM wote ni wezi wa aina hii, bila shaka kuna watakao suport hiyo motion. Bandugu twafa tugangamale!!!!!!!!!
 
Huu ni usaliti kwa wananchi maskini wa Taifa hili,hata kama(kufanyika malipo) yakihairishwa mpaka Bunge linalokuja bado sioni ahueni kwa jinsi Bunge lilivyojaa ndiyo mzee wa ccm,watatishwa na watapitisha hayo malipo..,Labda ingesaidia kujua nani yuko upande upi..
 
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya mwanakikao. Zinasema uongozi wa TANESCO wako leo wamekaa kikao wanaandaa waraka wa kuwalipa DOWANS. Ni Mungu tu aingilie kati hali ya nchi hii. Saa chache zilizopita bado walikuwa ndani ya kikao hicho.

Jamani, huu waraka wa kulipwa ni waraka gani huu?
Kwani mahakama kuu imeshasajili hiyo award?
Hapa ndipo ninapojua tunaibiwa..nilikuwa na mashaka kidogo ya kuibiwa, ila sasa sina mashaka, nimeamini tunaibiwa...

KIKWETE MWIZIIIIIIIIII!!!!!!!!!!!!!
KAMATA PIGA JIZI HILOOOO!!!!!
 
politics inafanya watu washindwe kufikiria kwa akili walizopewa. Unashangaa mtu msomi na mwenye akili timamu akipewa 10% (hata ikiwa milion 2 tu) utashangaa reasoning yote inakuwa impaired na anaanza kushabikia ujinga ulio wazi. Mmmmmmh
 
Huu ni wizi wa mchana peupe, kwa nini wasingoje bunge likae?????????? Wanalipa kwa budget ipi, imeidhinishwa na nani????????? Wote watakao husika wapelekwe mahakamani, bila kujali wamepewa amri na nani, watatajana huko mbele ya sheria. Sheria gani inaruhusu kutumia fungu kubwa la fedha bila kupitia bungeni au baraza la mawaziri??????????? CHADEMA nawaomba wainitiate vote of no confidence kwa huyo aliye toa amri, hata kama ni mkuu wa nchi he should be imperched. Si dhani kama CCM wote ni wezi wa aina hii, bila shaka kuna watakao suport hiyo motion. Bandugu twafa tugangamale!!!!!!!!!
kufuatana na kauli ya waziri wa nishati tanesco ndio wana takiwa kulipa, hivyo transaction hii haipiti kwenye vitabu vya serikali, hivyo hoja ya kupitishwa budget serikali haipo.
 
Kwa hiyo TANESCO ndo wanalipa? kesi imeshaandikishwa mahakama kuu?
Waraka unaandaliwa kwenye kikao?...........waraka ni nini?

Mwanzoni TANESCO walikuwa wamekataa kulipa wakisema serikali ndio inapaswa kulipa kwani wao walitoa ushauri wa kitaalamu serikali ikatumia wanasiasa kushinikiza mkataba. Inaonekana sasa suala la malipo limerudishwa TANESCO. Sielewi waliofungua kesi kama hakuomba hati ya dharura kuomba malipo yasifanyike hadi kesi hiyo isikilizwe?
 
Ohoooo!!! Naona wanafanya fasta ili kikao cha Bunge kinachoaanza Februari hii ishu iwe imeisha kabisa wala isifike huko, hivi sasa Tanesco kuna kitu ambacho sielewi waraka wa malipo kwani wao Tanesco ndio wanalipa hilo deni au wanataka kutufanya sisi hatuelewi hivi mtu anayekudai huwa anaandaliwa waraka wa malipo???
 
Back
Top Bottom