TANESCO wamejipanga kupata hasara ya Tsh. Trilioni 13.34 kwa miaka mitano ijayo

Mahitaji ya umeme yataongezeka hadi kufikia megawatts 4,000 mwaka 2025 huku uwezo wa TANESCO ukiwa ni kuzalisha megwatts 1,600 kukiwa na tofauti ya Megawatts 2,400 ambayo ni Upungufu wa 60%.

WAkati huo mradi wa Mwalimu Nyerere uliotarajia kuzalisha Megawatts 2,115 ukiwa ni kizungumkuti kutokana na kukumbana na cha ngamoto ya mabadiliko ya tabia nchi , hali inayoleta mashaka kwa Tanzania kuwa na uwezekano wa kukumbana na uhaba mkali wa nishati ya umeme kwa miaka minne ijayo.

KAtika mpango mkakati wa miaka mitano ijayo TANESCO wamejipanga kutumia Tsh. Trilioni 26.17 ili kuongeza uzalishaji wa nishati ya umeme. Gharama hizi zinawasilisha hasara ya Tsh. Trilioni 13. 34 kwa kuwa jumla ya mapato wanayokadiria kukusanya kwa miaka mitano ni Tsh. Trilioni 12.83.

View attachment 2020486

Hasara inaweza kuwa kubwa zaidi kwa kuwa haijaweka gharama za uendeshaji za kila siku kama malipo ya mishahara, nishati ya maji nk, kwa kuwa hela iliyotajwa hapo ni ya kuongeza uzalishaji wa umeme tu!

TANESCO wamejipanga kupata mapato ya Trilioni 1.9 kwa mwaka wa fedha 2020/21 ambapo katika mpango mkakati wa TANESCO wanatarajia kuongeza mapato kila mwaka wa fedha. Mwaka 2021/22 wamepanga kupata mapato ya Tsh. Trilioni 2.

Katika mpango Mkakati wa 2021/22 hadi 2025/26 TANESCO itakuwa imefanikiwa kuongeza mapato kwa 25% ambapo mwaka 2025/26 watakusanya Tsh. Trilioni 2.39.
Mbona hoja yako ipo biased sana, TANESCO ikitaka kuendeshwa kibiashara mtamudu gharama? Yaani wauze Unit moja kwa bei ya zaidi ya sokoni ili wacover operating expenses zote!!?

Kingine faida ya TANESCO ni mtambuka haipimwi kwa taasisi bali kwa uchumi mzima. Mfano kwa wao kuuza umeme chini ya market value wameokoa biashara ngapi mtaani ama wamepunguza operating expenses ya viwanda vingapo Tanzania?

Taasisi za serikali ziko pale kutoa huduma ila wakisema waende kibiashara nyie nyie mtarudi hapa kulia bei kupanda.

Then upo Biased kusema mahitaji ya umeme yataongezeka ila husemi hata vyanzo vya umeme mfano kupita Gesi, upepo, Joto-Ardhi ipo kwenye mpango wa taifa wa miaka 5!?

JF tunaweza kuwa critique wazuri kama tutapunguza biasness.
 
Hii nchi ina matatizo mengi mno, na kisababishi kikubwa ni mambo ya siasa za kinafiki, siasa zetu zinaimaliza nchi hii, haiwezekani miaka 60 ya Uhuru tushindwe hata kumaliza tatizo moja kubwa la kujivunia - tuna matatizo makubwa mno yanatukabili leo.

Elimu - tumeshidwa kabisa
Maji - hamna kitu
Nishati hasa Umeme - matatizo kama hivi mnavyoyaona.
Afya - huko ndiko ni balaa

Ni kipi ndugu zangu watanzania mtajivunia ndani ya hii miaka 60 ya uhuru wetu kwamba mmekifanya vizuri na mfano wa mataifa mengine? Siasa zetu za kishabiki zinalighalimu hili taifa.
Kilimo ndo kama nchi imeumbwa Jana,

Tunachokonoa tu kama tunachimba dawa.
 
kwan hadi 2025 stiglazi itakua bado haijaanza kazi? maana ile ni power generation ambayo ni costless
 
Hii nchi ina matatizo mengi mno, na kisababishi kikubwa ni mambo ya siasa za kinafiki, siasa zetu zinaimaliza nchi hii, haiwezekani miaka 60 ya Uhuru tushindwe hata kumaliza tatizo moja kubwa la kujivunia - tuna matatizo makubwa mno yanatukabili leo.

Elimu - tumeshidwa kabisa
Maji - hamna kitu
Nishati hasa Umeme - matatizo kama hivi mnavyoyaona.
Afya - huko ndiko ni balaa

Ni kipi ndugu zangu watanzania mtajivunia ndani ya hii miaka 60 ya uhuru wetu kwamba mmekifanya vizuri na mfano wa mataifa mengine? Siasa zetu za kishabiki zinalighalimu hili taifa.
Chakujivunia ni uzinzi haswaaa mtu akipata cheo chakwanza nikuongeza mchepuko na michepuko kwa kwenda mbele!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kilimo ndo kama nchi imeumbwa Jana,

Tunachokonoa tu kama tunachimba dawa.
Ardhi nzuri ina rutuba karibu kila wilaya tumebarikiwa na muumba..sasa badala ya kuwekeza kwenye kilimo cha kimkakati ukiwahusisha vijana wa 18 - 35 kama wadau wako wakuu..wewe unaingiza pesa kwenye biashara ya airline..huku ukiacha group hili likibaki linatuuzia soksi na maji ya uhai na afya mabarabarani..na dawa za nguvu za kiume.
 
Mbona hoja yako ipo biased sana, TANESCO ikitaka kuendeshwa kibiashara mtamudu gharama? Yaani wauze Unit moja kwa bei ya zaidi ya sokoni ili wacover operating expenses zote!!?

Kingine faida ya TANESCO ni mtambuka haipimwi kwa taasisi bali kwa uchumi mzima. Mfano kwa wao kuuza umeme chini ya market value wameokoa biashara ngapi mtaani ama wamepunguza operating expenses ya viwanda vingapo Tanzania?

Taasisi za serikali ziko pale kutoa huduma ila wakisema waende kibiashara nyie nyie mtarudi hapa kulia bei kupanda.

Then upo Biased kusema mahitaji ya umeme yataongezeka ila husemi hata vyanzo vya umeme mfano kupita Gesi, upepo, Joto-Ardhi ipo kwenye mpango wa taifa wa miaka 5!?

JF tunaweza kuwa critique wazuri kama tutapunguza biasness.
Umenena!
 
Ile tozo i bet they make more than a 100B kila mwezi yani😅
Binafsi nawaza ( hizi si takwimu halisi za NBS ni mawzo tu! kwa kutumia kanuni za kihesabu) inaweza kufikia 200 bilioni kwa hesabu hii hapa chini, nitaomba wenye takwimu halisi wanikosoe.

Kwa takwimu za TCRA 2017, tulikuwa natumiaji wa simu 23 milions.

Tuchukue milioni 20 tu wanafanya kwa wastani miamala mitatu kwa wiki inayogharimu kila muamala tozo ya 1200.

Mwezi makusanyo ya tozo = watu 20,000,000 x tzs 1200/ mtu x 3 idadi ya miamala/wiki x 4 wiki/mwezi

= tzs 288,000,000,000/=

Hapo hatujagusa tozo za kibenki.
 
Hii nchi ina matatizo mengi mno, na kisababishi kikubwa ni mambo ya siasa za kinafiki, siasa zetu zinaimaliza nchi hii, haiwezekani miaka 60 ya Uhuru tushindwe hata kumaliza tatizo moja kubwa la kujivunia - tuna matatizo makubwa mno yanatukabili leo.

Elimu - tumeshidwa kabisa
Maji - hamna kitu
Nishati hasa Umeme - matatizo kama hivi mnavyoyaona.
Afya - huko ndiko ni balaa

Ni kipi ndugu zangu watanzania mtajivunia ndani ya hii miaka 60 ya uhuru wetu kwamba mmekifanya vizuri na mfano wa mataifa mengine? Siasa zetu za kishabiki zinalighalimu hili taifa.
Kiuhalisia 'tunajivunia' kuwepo kwa CCM (zamani Tanu na ASP) madarakani kwa miaka 60. Hayo ndio 'mafanikio' pekee ambayo labda taifa la mazuzu tunaweza kupongeza.

CCM oyeee!
 
Siamini kama mradi wa bwawa la Nyerere ndio unazimishwa hivyo....
Mkuu naamini hautazimwa. Tanesco wanasimamia sana ule mradi na kazi inafanyika usiku na mchana. Ila TAHADHARI NI KWAMBA KAMA ULE MRADI UTAKWAMISHWA NA WATU UKU TUNAONA TUINGIE KWENYE MAOMBI YA UKOMBOZI MAANA ITAKUWA LAANA KUBWA INAITAFUNA TAIFA LETU. NAOMBA MUNGU KILA MWENYE NIA YA KUUKWAMISHA ULE MRADI WATANGULIE JEHANAMU
 
Basi watangaze nafasi ya uwekezaji kwenye umeme waje wawekezaji kama ilivyo solar energy Ili tuchague tujiunge na umeme upi, kweli walioshika uongozi hawapo serious kuleta maendeleo ya Nchi, hivi Nchi inahitaji hela ya kuendesha serikali, maendeleo na akiba ya kizazi kijacho inaingia akilini serikali ipate wateja wa kununua bidhaa kwa wingi tena bila nguvu ya matangazo zaidi ya huduma nzuri kwa wateja alafu unazembea kuzalisha kwa wingi Ili iweje? Na hao wafanyakazi umuhimu wao utakuwa wapi? Kama hawawezi kuleta tija yoyote ya kujivunia?
 
Hii nchi ina matatizo mengi mno, na kisababishi kikubwa ni mambo ya siasa za kinafiki, siasa zetu zinaimaliza nchi hii, haiwezekani miaka 60 ya Uhuru tushindwe hata kumaliza tatizo moja kubwa la kujivunia - tuna matatizo makubwa mno yanatukabili leo.

Elimu - tumeshidwa kabisa
Maji - hamna kitu
Nishati hasa Umeme - matatizo kama hivi mnavyoyaona.
Afya - huko ndiko ni balaa

Ni kipi ndugu zangu watanzania mtajivunia ndani ya hii miaka 60 ya uhuru wetu kwamba mmekifanya vizuri na mfano wa mataifa mengine? Siasa zetu za kishabiki zinalighalimu hili taifa.
Mkuu serikali za CCM zmefeli kabsaa!!
 
Back
Top Bottom