TANESCO walitukatia umeme tukisubiri mwongozo wa jeshi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANESCO walitukatia umeme tukisubiri mwongozo wa jeshi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sinkala, Feb 19, 2011.

 1. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nimesikitika sana na uamuzi wa TANESCO kukata umeme huku mimi na familia yangu tukisubiri tamko au mwongozo wa haraka haraka kutoka kwa uongozi wa JWTZ au wataalamu wa mabomu ili tuweze kujua nini cha kufanya wakati milipuko ikiendelea. Akili yangu ya haraka ilikuwa ni kufungua redio na televisheni ya taifa lakini cha kusikitisha umeme ulikatwa. Kwa muda huo sikujua ipi ni hatua salama, kukimbiza familia nje ya nyumba au kutulia ndani. Kwanza niliwaambia tutoke nje, lakini baada ya muda mfupi nikawaambia vipande vitatukata, turudi ndani. Baada ya milipuko kutulia ndipo umeme ulirudishwa, na hakuna aliyekuwa na hamu tena ya kusikiliza/kutazama TV/redio. Wote tulienda kulala huku nyumba ikiwa na nyufa. Asubuhi nilipotaka kujua nini kinachoendelea, umeme ulikatwa tena. Niliishia kusikiliza uvumi tu kwamba mabomu yaliyosalia yatalipuliwa saa sita, wengine saa saba na wengine saa tisa. Ndipo nilipoanza purukushani za maandalizi ya kukimbiza family. Bahati nzuri kuna kiredio kidogo nilishakitosa muda mrefu, nikakitafuta na ndipo nikasikia kuwa Amiri Jeshi mkuu aamewataka watu wasihame. lakini kwa kuwa tayari nilishajiandaa kuondoka, ilibidi kuitoa kwa muda family pale ili wasahau mambo ya jana ya sauti za milipuko na hasa mivumo ya mabomu iliyokuwa inapita juu ya anga la paa letu. Jana nilimsikia Prof. Lipumba akisema kuwa ni vyema watu wakaelimishwa mapema hatua zipi ni sahihi kuchukua inapotokea hali hii, nampongeza kwa hilo. Lakini hawa TANESCO wangetuvumilia kidogo ili tuwe informed nini cha kufanya, nadhani watu wengi wasingehangaika kuhama ile siku ya pili. Kama walikata kwa sababu za kiufundi, sina sababu za kuwalaumu, ila kama walikata kama sehemu ya mgao wa umeme, hakika wao ni wakatili.
   
 2. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #2
  Feb 19, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ...I suspect walikata kwa sababu za kiufundi, kwani hata mvua kubwa na radi zikiwa zinapiga huwa wanakata.

  ...Kilichokosekana ni kitu kinachoitwa Crisis Management. Vyombo vyote vya habari na mawasiliano vilipaswa kutumiwa vizuri kuelimisha wananchi nini cha kufanya na kwa wakati gani. Tume ya maafa bado inahitaji kujipanga vizuri. Nataka kuamini wana miongozo ya kazi inayobainisha likitokea janga la namna fulani wanatakiwa kufanya nini, kwa kushirikiana na kina nani.
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Poleni sana!
   
 4. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #4
  Feb 19, 2011
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  hivi walishindwaje kutumia mitandao ya simu kutuma ujumbe kama walivyofanya kipindi cha kapeni???????????????
   
 5. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #5
  Feb 19, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nani awape taarifa? bado mnadhani kuwa viongozi wa nchi wanawajali raia wao? Walisema yale ya Mbagala hayatatokea tena, hatimaye ya Gongo la Mboto hayatatokea tena. Baadaye tutasikia yaliyotokea Lugalo hayatatokea tena.

  Waliunda tume kuchunguza suala la milipuko ya mabomu kule Mbagala lakini ripoti yake hadi leo siijui, tutasubiri ya Gongo la Mboto nayo hatutaijua. Yote hayo pengine ni kwa sababu za kiusalama lakini bado maisha yetu hayapo salama.

  Kwa yote hayo yanayotokea wananchi tunapaswa kuwa wa kwanza kujilaumu kwani inasadikika kuwa viongozi wanaotuongoza tuliwachagua. Kama tulikosea katika kuchagua basi tuwe na ujasiri wa kuwaambia mjiuzulu haraka msisubiri hadi miaka mitano iishe. Tusipofanya hivyo tutaendelea kukoma ubishi.

  Haiingii akilini kama serikali inanunua mabomu kwa ajili ya kulinda raia lakini kumbe ndiyo inaua raia. Walipoyanunua hawakujua namna na mahali pa kuhifadhi?
   
 6. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #6
  Feb 21, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  poleni sana, hili ni tatizo la nchi yetu hatuna elimu ya kukabiliana na majanga makubwa kama haya,kukata umeme ni sawa na kuwaambia mfe kwa sababu hamjui kinachoendelea au ufanye lipi,kibaya zaidi hata simu walikata,fire sasa hivi nao wamekuwa wakusanya pesa za magari barabarani,kweli wanamda wa kufikiria au kusoma kitu kipya kwa ajili ya kukabiliana na majanga kama haya?
   
Loading...