TANESCO wakubali kubomoa jengo lao, waahidi upatikanaji wa umeme wakati wa kutekeleza agizo hilo

Kikatiba mahakama ndicho chombo pekee cha kutoa haki,siyo matamko yote ya rais ni halali.Kubomoa jengo hilo ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi.Bado uwezekano upo wa kubana zaidi upande wa wizara ya maji kukabomolewa ili kuepusha hasara zaidi.

Sent from my TECNO H5 using JamiiForums mobile app
Umenena hapo juu, mahakama ndo chombo cha kutolea haki, bila kupepesa macho hii ishu ya libomolewe au lisibomolewe ikienda mahakamani, saa mbili na robo asubuhi judge atasema toa hiyo kitu iko ndani ya hifadhi ya barabara.
 
"....ikumbukwe kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Mheshimiwa Rais katika kuleta maendeleo ya nchi yet. "

Hahahahhaha
 
Wangeomba washauri wa wataalamu wa Ujenzi jinsi ya kuepusha hasara,barabara ingeweza kujengwa hata kwa ghorofa Mbili au Tatu lengo ni kulikwepa jengo,maana kodi zetu zinauma sana hasa sie ambao kila siku lazima tulipe kodi kuchangia kupitia mafuta ya Magari,faini,nk.
Lakini mkuu kwaniwajuavyo wabongo endapo wangekwepeshatu basi huo Moto wa kulaumu serikali kuwa wanajindelea Nani angeuzima!
 
Hii ndiyo alternative mkuu! Kumbuka bila maamuzi magumu kama hayo hatutokua na miji mazuri kama kwa wenzetu, ili tujifunze lazima haya mambo yatokee.
Kwa Nn miji iwe mizuri kama kwa wenzetu?! Na isiwe mizuri kwetu ili wenzetu waige?! Kama hatuwezi kutohoa na kunyambulisha ..tunakopi tuu hatuwezi kuwa original... Kila watu wanamahitaji yao... Ndio maana unaenda Dubai ac mpk parking, na vituo vya daladala ... Ukifika marekani hawana muda na hayo..kwakuwa Hali yao haihitaji hayo mambo... Wenzetu kila nyumba ina central heating system... Dubai hawana kwakuwa hawahitaji hiyo kitu..hali yao ni joto.

Na Sie tuna mahitaji muhimu tofauti na Kenya Singapore na huko walipoziona hizo flyover... Kwahiyo ni lazima tutumie akili ya ziada kuidefine hiyo flyover in a way inatuaccomodate kwa njia ambayo ni rafiki huku tukijiepusha magharama yasiyokuwa na kichwa wala miguu.

Kama tunashindwa kumunipulate barabara kipande cha mita miatano mpk kilometer ili tutunze lile jengo ..tutaweza kurusha satellite au kubuni ndege zetu siku za usoni?! Kuanzisha vivutio vingine baada ya madini na wanyama kuwa tumewamaliza au wameisha chati?! Kweli
 
Kwanza hiyo barabara ya Morogoro ni kubomoa na kujenga tu tangu mwaka 2000. Je ni pesa kiasi gani imetumika? Ni ufisadi wa kutisha yaani kila mwaka ni kuboa na kujenga tu.

Nakwenda Zimbabwe aka (Simbawe)
 
Kwa Nn miji iwe mizuri kama kwa wenzetu?! Na isiwe mizuri kwetu ili wenzetu waige?! Kama hatuwezi kutohoa na kunyambulisha ..tunakopi tuu hatuwezi kuwa original... Kila watu wanamahitaji yao... Ndio maana unaenda Dubai ac mpk parking, na vituo vya daladala ... Ukifika marekani hawana muda na hayo..kwakuwa Hali yao haihitaji hayo mambo... Wenzetu kila nyumba ina central heating system... Dubai hawana kwakuwa hawahitaji hiyo kitu..hali yao ni joto.

Na Sie tuna mahitaji muhimu tofauti na Kenya Singapore na huko walipoziona hizo flyover... Kwahiyo ni lazima tutumie akili ya ziada kuidefine hiyo flyover in a way inatuaccomodate kwa njia ambayo ni rafiki huku tukijiepusha magharama yasiyokuwa na kichwa wala miguu.

Kama tunashindwa kumunipulate barabara kipande cha mita miatano mpk kilometer ili tutunze lile jengo ..tutaweza kurusha satellite au kubuni ndege zetu siku za usoni?! Kuanzisha vivutio vingine baada ya madini na wanyama kuwa tumewamaliza au wameisha chati?! Kweli
Kiongozi uko sawa ila mimi nilivyomuelewa mkulu, kafanya haya ili raia (wahanga) waliobomolewa wafahamu kuwa sheria ni msumeno hivyo siyo wao tu walioguswa na hili tukio.
Kuhusu ujenzi wa miji uko sawa mkuu ila wataalam Wetu bado sana tena hili suala bado kabisa.
Maoni yangu ni kwamba tukibadili mitaala ya elimu yetu kuanzia chini kabisa mpaka huko juu nahisi kila kitu kinaweza kikawa sawa kabisa.
 
Wangeomba washauri wa wataalamu wa Ujenzi jinsi ya kuepusha hasara,barabara ingeweza kujengwa hata kwa ghorofa Mbili au Tatu lengo ni kulikwepa jengo,maana kodi zetu zinauma sana hasa sie ambao kila siku lazima tulipe kodi kuchangia kupitia mafuta ya Magari,faini,nk.
Kama huyu alivyoshauri
9ba7fe462e4e744e543b04f64d99eaed.jpg
 
..kudadek!!...yani nchi hii God forbid!!.hivi nia njema ya kuleta maendeleo inatafsiriwa vipi kwa kubomoa jengo kubwa lililo makao makuu ya shirika linalosambaza umeme tz????....hii inamwingia nani akilini???.....yani unavunjaje jengo lililogharimu mabilioni alafu hapo hapo unaomba hela nje kwa wafadhili kujenga tena???huu ujuha unatafsiriwa vipi???

...kumuunga mkono rais!!my foot...yani hata rais anapokosea aungwe mkono????ama huyu rais ni malaika asiyekosea????... Hivi ikija kudhihirika hakukuwa na lazima ya kubomoa jengo hili itakuwaje litakopokuwa limevunjwa??....

..hivi anatakiwa kuvunja jengo ni Tanesco ama mmiliki wa jengo??maana tunajua tanesco ni wapangaji tu.....this is just insane....
 
Kiongozi uko sawa ila mimi nilivyomuelewa mkulu, kafanya haya ili raia (wahanga) waliobomolewa wafahamu kuwa sheria ni msumeno hivyo siyo wao tu walioguswa na hili tukio.
Kuhusu ujenzi wa miji uko sawa mkuu ila wataalam Wetu bado sana tena hili suala bado kabisa.
Maoni yangu ni kwamba tukibadili mitaala ya elimu yetu kuanzia chini kabisa mpaka huko juu nahisi kila kitu kinaweza kikawa sawa kabisa.
Ni kweli kuna shida kwenye elimu.. Tens kubwa.. Mfano wa kuwajulisha wahanga kuwa sheria ni msumeno ndio unanitia ukakasi...
Jengo ni la Tanesco/PPF. PPF/Tanesco ni mali ya serikali. Serikali ni sisi sote waliojenga katika viwanja vilivyopimwa kwa kufata taratibu na sisi tulijenga kiholela..
Pesa inatoka kwetu sote..kwa maana ya kodi.. Sasa ili kuwapoza machungu watu unaotubomolea... Unavunja jengo ambalo tunalihitaji watanzania wote..na ambalo tumelijenga kwa pesa zetu sote.. Tunaposhangilia nakosa kuelewa.. Tunajua nani anamiliki hizi Mali kweli?!
Kwa mfano kama watu wangeambiwa chuoni huwa wanakopa kiasi gani kwa mwaka wangekuwa serious sana na shule.. Vijana huwa hawajui kama mikopo ni mikubwa kwa kuwa wanachoona kinapita mikononi mwao ni meals na accommodation tu..sometimes na pesa ya vifaa na field.. Ada haioni hivyo wanachukulia poa.. Kama wangekuwa wanapewa mkononi yote wangekuwa serious na wangeappreciate HESLB ...
Najaribu kusema kwamba kama watanzania wangejua hizi ni Mali zao na namna pesa yao inavyotumika kukuyapata maofisi na barabara na vuote hivi nakuapia only the brightest wangebaki kutuongoza... Haiwezekani tubomoe jengo, ambalo itabidi tureplace, kujenga barabara tunayokopa on expense ya wananchi... Hiyo double costing nani angekubali?!

Wanasiasa wanapenda jamii iliyokufa kifikra maana ni rahisi kuipeleka... Wanaondoa vitu muhimu kama somo la siasa na Uraia.. Litawafanye wapate shida kuongoza wameliweka kando..na matokeo yake leo wanataka vijana wazalendo, na raia wema bila kuwafundisha uzalendo na kuwa RAIA mwema ni nini!? Tuna safari
 
Nchi inayomuona Dakta Shuka ni mzima wa afya si ajabu kuwq na viongozi wa sampuli za kubomoa jengo la mabilioni kupisha service road ya mamilioni
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom