Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Hukumu imetolewa wiki Jana iliyoishia August 24, 2018.
Ahadi hewa za mahakama ya mafisadi mnazikumbuka?
Lini ngedere amhukumu nyani? Yaani ccm iwashitaki mafisadi wenzao waliowaweka madarakani? Na wahukumiwe? Na wafungwe?
Mafisadi wa Escrow waliteuliwa uwaziri, ni viongozi bungeni, wengine wamegombea ubunge kwa tiketi ya ccm wakashinda kwa nguvu ya dola.
Ufisadi ccm ni sawa na mwili na damu..
========================
Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) limeshindwa kwenye kesi yake IPTL -Independent Power Tanzania Limited.
Hukumu hiyo imetolewa na mahakama ya inayoshughulika na migogoro ya uwezekaji, ICSID yenye makao yake mjini Washington DC, Marekani na ipo chini ya benki ya dunia.Tanesco ilikuwa ikiwakilishwa na makampuni mawili ya wawanasheria R.K. Rweyongeza & Co. Advocates na Crax Law Partners ya Tanzania, pamoja na lile la Zurich, Kellerhals Carrard. Pesa hizo zinatakiwa kulipwa kwa Standard Chartered Bank-Hong Kong (SCB-HK).SCB-HK ililinunua deni la IPTL kwa punguzo la bei ya milioni 76.1 kutoka Danaharta Bankin ya Malaysia, August 2005 baada ya Danaharta kushindwa kuchukua mkopo wake kutoka kwa IPTL.
Hiyo ina maana kuwa SCB-HK imepata faida ya dola milioni 172. IPTL ilikopa dola milioni 100 mwaka 1998 kutoka kwenye kundi la benki za Malaysia ili kujenga mtambo umeme Tegeta wenye megawatt 100.
TANESCO ilifungua kesi ICSID baada ya kubaini kuwa imekuwa ikitozwa zaidi na IPTL. Kesi hiyo inahusiana na ripoti ya uchunguzi wa kashfa ya IPTL iliyohusisha uchotwaji wa shilingi bilioni 306 za kitanzania.
Hukumu hiyo imefikiwa mwisho wa wiki iliyopita ambapo World Bank tribunal (international centre for settlement of investment disputes.
ICSID imeamuru TANESCO kuilipa Standard Chartered Bank Hong Kong (SCB HK) kiasi cha dola za kimarekani milioni 148.40 pamoja na tozo riba.
SCB HK ndio walionunua mkopo wa IPTL kutoka bank ya Malaysia Danaharta kwa gharama ya dola za kimarekani milioni 76.1
Kutokana na gharama za riba na nyinginezo sasa TANESCO inatakiwa kulipa Bilioni 700 ZAKITANZANIA.
BILA SHAKA TANESCO WANAYAANGAZA MAISHA YETU