TANESCO: Upungufu wa umeme katika gridi ya Taifa Jumamosi Novemba 18 na kesho Jumapili Novemba 19, 2017

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,556
21,487
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA TAARIFA YA KUSAFISHA NA KUUNGA BOMBA LA GESI - KINYEREZI I, MAANDALIZI YA KUUNGA KITUO CHA KINYEREZI II

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linawataarifu Wateja wake kuwa leo Jumamosi Novemba 18 na kesho Jumapili Novemba 19, 2017 kuna usafishaji na kuunga bomba kubwa la Gesi katika Mitambo ya Kinyerezi I, sambamba na zoezi hilo pia yanafanyika maandalizi ya kukiunganisha Kituo cha Kinyerezi II, kuanzia Saa:02.00 Asubuhi hadi saa 11.00 Jioni, kama tulivyowatangazia.

Kutokana na kazi hiyo kutakuwa na upungufu wa umeme katika Gridi ya Taifa, hivyo baadhi ya Wateja waliounganishwa katika Gridi ya Taifa wa maeneo mbalimbali Nchini watakosa huduma ya umeme. Zoezi hilo linaendelea kwa ufanisi mkubwa na uharaka ili kurejesha huduma ya umeme kwa wakati.

Tutaendelea kutoa taarifa zaidi za maendeleo ya kazi. TAHADHARI Kutokana na kazi hii Wananchi mnaombwa msipite karibu na eneo la Mitambo ya Kinyerezi, kutokuwasha moto, kutokufanya shughuli za uchomeleaji vyuma pamoja na shughuli nyingine yoyote yenye viashiria vya moto, ili kujikinga na madhara yanayoweza kutokea iwapo shughuli tajwa zinafanyika maeneo yaliyo karibu na Mitambo. Shirika limesha fanya taratibu zote za ki usalama katika eneo la Mitambo.

TANESCO inawaomba ushirikiano na kuwa waangalifu wakati wa zoezi hili. Kwa mawasiliano Tovuti: www.tanesco.co.tz Mitandao ya Kijamii www.facebook/tanescoyetu twitter.com/tanescoyetu

Tafadhali usisogelee, usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka Kwa taarifa za dharura kituo cha Miito ya simu namba 2194400 or 0768 985 100

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na: OFISI YA UHUSIANO, TANESCO – MAKAO MAKUU.

Novemba 18, 2017
 
Ongea vizuri mkuu, tangia hitilafu itokee kwenye grid ya taifa mpaka sasa hali ni mbaya mtaani, kuna kukatika kwa umeme mara kwa mára baadhi ya sehemu hapa Dar na Mwanza.

Ilemela juzi tangia asubuhi umeme umekatika na kurudishwa jana jioni, pia eneo la Keko na Oysterbay kuna missing of one phase kwa wale wanaotumia three phase na kusimamisha shughuli nyingi kwa wale wanaotumia vyombo vya three phase na tatizo halitatuliwa kwa muda mwafaka.

TANESCO fungukeni msaidiwe mawazo msifikiri mafundi wazuri wapo TANESCO tu maana mtaani kuna changamoto sana hasa kwa wale wanaotumia three phase, phase zinapotea sana, kuna nini huko mnachoficha.
 
Ongea vizuri mkuu, tangia hitilafu itokee kwenye grid ya taifa mpaka sasa hali ni mbaya mtaani, kuna kukatika kwa umeme mara kwa mára baadhi ya sehemu hapa Dar na Mwanza. Ilemela juzi tangia asubuhi umeme umekatika na kurudishwa jana jioni, pia eneo la Keko na Oysterbay kuna missing of one phase kwa wale wanaotumia three phase na kusimamisha shughuli nyingi kwa wale wanaotumia vyombo vya three phase na tatizo halitatuliwa kwa muda mwafaka.
TANESCO fungukeni msaidiwe mawazo msifikiri mafundi wazuri wapo TANESCO tu maana mtaani kuna changamoto sana hasa kwa wale wanaotumia three phase, phase zinapotea sana, kuna nini huko mnachoficha.
Dakar kumekuwa hakuna umeme tangu juzi- Mambo haya ni ya kawaida kwa nchi zinazoendelea kwani hata south africa ambako wana nuclear powered station bado wana matatizo kama tuliyokuwa nayo ingawa uchumi wao ni mkubwa mara 10 ya uchumi wetu.
 
Dakar kumekuwa hakuna umeme tangu juzi- Mambo haya ni ya kawaida kwa nchi zinazoendelea kwani hata south africa ambako wana nuclear powered station bado wana matatizo kama tuliyokuwa nayo ingawa uchumi wao ni mkubwa mara 10 ya uchumi wetu.
Kwa hiyo tuendelee kuiga hayo kwamba Dakar wamekoswa umeme, pia nasi tukoswe. Kama upo TANESCO ndg yangu, hilo shirika halitaendelea kamwe kwa akili hii ni bora ungetoa jibu la kisiasa kuliko kujilinganisha kwa ujinga.
 
Kwani kuna jipya hapa? Tangu lini tunao umeme wa uhakika hadi mnajihangaiasha kutoa tangazo kama hili, tushazoea kukosa umeme kila iitwapo leo
 
TAHADHARI Kutokana na kazi hii Wananchi mnaombwa msipite karibu na eneo la Mitambo ya Kinyerezi

Hivi mtu anathubutuje kupita karibu na mitambo ya Kinyerezi wakati eneo zima linazungukwa na wanajeshi wenye silaha kali kali pamoja na uzio mkubwa kulizunguka eneo hilo? :eek:

Yani pale Kinyerezi panalindwa zaidi ya kambi ya jeshi au hata kuliko makao makuu ya jeshi. Sijui pana siri gani nzito mule!
 
Kwa hiyo tuendelee kuiga hayo kwamba Dakar wamekoswa umeme, pia nasi tukoswe. Kama upo TANESCO ndg yangu, hilo shirika halitaendelea kamwe kwa akili hii ni bora ungetoa jibu la kisiasa kuliko kujilinganisha kwa ujinga.
NAONA UMEKURUPUKA, HEBU JARIBU KUSOMA NA KUANGALIA MANTIKI YA NILICHOANDIKA
 
Back
Top Bottom