Tanesco tumewachoka sasa

mwankuga

JF-Expert Member
Aug 30, 2010
334
120
Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikikereka na tatizo la umeme katika nchi hii.Tatizo la ukosefu wa nishati hii muhimu limekuwa tatizo kubwa sana tangu enzi na enzi huku viongozi wa TANESCO na serikali kwa ujumla wakiwa wakitupa ahadi na matumaini yasiyozaa matunda.Kumekuwa na gharama kubwa sana za kuingiza umeme katika nyumba hasa kwa sisi ambao vipato vyetu ni vya chini,na pia ni gharama sana kulipia ankara za umeme amb azo kwa kiasi kikubwa zinapikwa.

Mbali na hilo,bado shirika hilo linaongoza kwa kuingia mikataba tata na makampuni mengine kama vile IPTL.AGGREKO,SONGAS,RICHMOND,DOWNS N.K.Inaposainiwa mikataba mbwembwe zinakuwa nyingi lakini mwisho wake ni mbaya.Leo tunaambiwa TANESCO inatakiwa kuilipa DOWANS BILIONI 185,baada ya muda mfupi TANESCO inatangaza mgao wa umeme,huku waziri mhusika anatangazia umma kuwa mgao wa umeme Tanzania itakuwa historia.

Najua sisi Watanzania ni waoga sana,lakini ubabaishaji umefika kikomo,umefikia sehemu ambayo hatuwezi kujifunga mikanda tena.Tumenyamaza kwa muda mrefu sana tukiwa na imani kuwa ipo siku moja mambo yatakuwa safi.Rai yangu,nawaomba Watanzania wenzangu tujitokeze katika maandamano yatakayoitishwa na CHADEMA NA VIKUNDI VINGINE kupinga udhalimu wa serikali yetu.Maandamani ni hatua ya kwanza kuonyesha kuwa hatulidhiki na hali hiyo,halafu tuone kama kilio chetu kama kitasikilizwa,kama hatutasikilizwa tuchukue hatua ngumu zaidi.Nawatakia Krismasi njema huko mjini
 
Back
Top Bottom