kitokololoo
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 704
- 813
Kaya nyingi hapa mbalizi hazina Umeme tamko toka tanesco mkoa wa mbeya kupitia viongozi wa vitongoji walisema Tusuke umeme kaya zote ambazo hazina umeme na tukapewa na fomu kabisa na watendaji na wenyeviti wa vitongoji watu wakakopa mpk hela kusuka umeme haraka haraka ili umeme ukija uingizwe bila tatizo.
Yapata miaka 3 sasa Hakuna kinachoendelea kby zaidi unashangaa Mtu analetea Nguzo mbili ukimuuliza anakwambia nimetoa laki 7 ndyo wameleta hzo nguzo na ushahidi ninao nilipiga picha ile fomu mliyomlipisha hzo hela.
Wewe mnyonge ukienda pale tanesco mbeya unaambiwa Serikali haijaleta nguzo wala mita sasa swali hzo nguzo na mita mnazouza laki 7 mnatoa wapi?
Kitongoji cha Nsalala Mbeya Vijijini tunawaona uhuni mnaoufanya kila siku kwa kuuza nguzo kwa wenye pesa wkt serikali imetoa tamko ni bure nchi nzima.
Tukumbukeni sisi wanyonge wa nchi hii.