Tanesco! Tanesco! Kitanda msichokilalia hamjui kunguni wake....! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco! Tanesco! Kitanda msichokilalia hamjui kunguni wake....!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jan 3, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  Asalaam aleykum kwa ndugu zangu walio waislamu, tumsifu Yesu Kristo kwa ndugu zangu walio wakristu, shikamooni wakubwa zangu na habari za saa hizi au mambo vipi kwa wale wa rika langu.

  leo sina mengi ila kutaka mchango wa mawazo japo mawili matatu kwa kero hii inayo wasibu waTanzania wengi na labda hata wana wa Africa kwa ujumla, ila sitoangaza mbali kuliongelelea tatizo hili kwa undani ila ndani ya mipaka ya inchi yangu ambayo bila shaka ninao uhuru wa kuyasema mawazo yangu kama ilivyo kwa mujibu wa katiba yetu ambayo tunaizingatia kuwa ndio sheria mama.
  kukaa kimya NA MAWAZO YALIO SAHII au mawazo bunifu sio kuyatatua matatizo bali kukuza na kuyafanya matatizo kuwa sugu, ila kulisema jambo ambalo linatatiza ndio suluu inayoweza kuleta mwafaka wa jambo lililo tata, nina yasema haya ili tuweze kupeana mawazo ambayo yanaweza kutatua na hata kupunguza dukuduku ulilonalo kuhusu jambo fulani ambalo linakughasi na unadhani muafaka wake upo ila labda wahusika hawaja kaa chini kulitafakari kwa kina labda kwa sababu wameridhika na vyeo na majina makubwa (kuwa wanahusika na maslahi ya watu wao) au labda hawapatwi na masahibu haya yanayotukumba sisi siku hadi siku, sio machache yapo kadha wa kadha katika taifa letu najamii kiujumla amakweli kuna ukweli ndani yake katika ile medhali ya kale kuwa KITANDA USICHOKILALIA HUJUI KUNGUNI WAKE basi sisi tunao wajua tushirikiane. hebu tuangazie hili la TANESCO

  tumekuwa tukipata hasara kula kukicha na kuingia gharama ambazo zipo inje ya mipango yetu kila kukicha labda kwa kukosa umeme na hivyo kulazimika kuingia gharama za vibatari vya mafuta ya taa, chemli na hata wakati mwingine mishumaa ambayo huwa inaweza kusababisha madhara makubwa pale uzembe kidogo unapotokea, bado mamia kwa maelfu ya watu huimgia hasara kwa shoti zinazojitokeza mara kwa mara labda kwa ongezeko la umeme ambalo maranyingine husababisha kuungua kwa vifaa mbalimbali vya umeme na hata kusababisha maafa makubwa kama moto kutokana na ongezeko la nguvu hiyo, ambapo ni wachache au hakuna kabisa wanaolipwa fidia kwa kutokana na hasara hizo ambazo shirika hili tegemeo husababisha.
  sasa je tulichukulieje shirika hili ambalo kwa kifupi linatutia shaka kwa utendaji kazi wake na hata kwa historia yake yakitaifa iliyotingisha na kuendelea kutingisha kwa mikataba mibovu (RICHMOND) ambayo ilikuwa na ahadi zakuridhisha ambayo ndio matarajio yakila mtanzania kuishi bila giza (BATILI), sasa chakukera zaidi ni kuhusu mgao, migao hii inayopelekea shughuli nyingi za watu kufikia kikomo kwa kukosekana kwa umeme sasa wengine wetu ni watu wa kawaida hatuna majenereta, na sasa je fridge zetu zilizosheheni mapochopocho yakubana matumizi tufanyeje?


  SULUHU ipo wala isiwe balaa kwetu kwani kwa ratiba ya TANESCO ya migao hii ya umeme huwa ndio ratiba za wezi na vijizi vya mtaani kwetu wavunje nyumba gani leo au wachane nyavu ipi ya dirisha walambe kisuruali ulicho vaa jana ukaacha walet,
  nakumbuka miaka ya nyuma tulikuwa na kampuni moja ya soda nayo ilitoa huduma kwa hali ya taratibu sana hata kutofikia watu sehemu za vijijini na baadhi ya mikoa, ila baada ya shirika lingine kuja kuwekeza aaah kumekuwa na ushindani na ongezeko la bidhaa hiyo ya kila ladha na ujazo wa gharama tofauti bila kusahau kuweko kwa ongezeko la ajira kupitia kupanuka kwa usambazaji wa huduma na kuanzishwa kwa kampuni hizo, vile vile kwenye mitandao ya simu pia kumbuka miaka ya nyuma vocha ilikuwako ya bei gani______?

  Sasa ifike pahala serikali yetu itafute wawekezaji waje hapa nchini kuwekeza katika swala zima la UMEME ili tuweze kujikwamua na balaa hili la kupata umeme usioweza kuwasha hata taa ukaokota kalamu kisa line moja inatumiwa na nusu mtaa, pia itapunguza kiburi chao cha kutupangisha foleni kwenye vituo vya mafuta huku tunamanoti yetu mkononi yani huduma zenye kero kabisa vituo vyakuhesabika quality ya umeme wenyewe hafifu, pia italeta huduma bora zakumjali mteja iwapo zitaongezeka kampuni zitakazo gawa huduma hizi , pia kutakuwa na uwezekano wa wateja kulipwa fidia iwapo kutakuwa na hasara itakayosababishwa na shirika kwa mteja na hata gharama zitapungua kutokana na ushindani baina yao kama zilivyo kampuni za simu hivi sasa miaka mitano iliyo pita ulidhani ingekuwa hivi?

  Tunautambua utendaji kazi wa serikali yetu lakini kwa hili nilakuangaliwa kwa kina
   
Loading...