TANESCO: Taarifa ya kukosekana kwa umeme katika baadhi ya maeneo katika mkoa wa Kinondoni Kaskazini

THEBLACKPEARL

Member
Jun 11, 2015
69
46
TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA UMEME KWA BAADHI YA MAENEO YA MKOA WA KINONDONI KASKAZINI

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kuwa leo asubuhi Machi 10, 2016 kama walivyotangaziwa kwenye vyombo vya habari,
Njia inayounganisha vituo vya kupoozea umeme vya Mikocheni na Viwanda ilizimwa ili kuruhusu mkandarasi afanye kazi ya kutoa line ya juu na kuweka line ya chini eneo la karibu na Kituo cha Kupoozea umeme cha Mikocheni.

Maeneo yanakayokosa umeme ni Mikocheni, Mwenge, Survey, Sinza, Kawe Beach na Kijitonyama.

Umeme utarejeshwa saa 10 jioni.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu.
 
Tafadhali tunaomba mrudishe muda huohuo au mapema zaidi kama mlivyoahidi, kazi njema
 
Back
Top Bottom