TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
TANESCO kuna tatizo gani ambalo limetokea na kupelekea maeneo Mbezi Beach 'B' kukosa umeme toka usiku wa manane mpaka muda huu? Najaribu kupiga namba za simu za ofisi yenu lakini zinaonekana zipo 'busy"?
 
TANESCO kuna tatizo gani ambalo limetokea na kupelekea maeneo Mbezi Beach 'B' kukosa umeme toka usiku wa manane mpaka muda huu? Najaribu kupiga namba za simu za ofisi yenu lakini zinaonekana zipo 'busy"?
Tumepokea taarifa kwa hatua zaidi tafadhali
 
Mmekata umeme last week jtatu,jnne,jtano,jmosi siku nzima no working!wiki hii jana jtatu mmekata saa moja asubuhi mpaka saa nne usiku eneo kubwa kuanzia Manzese mpaka Kimara,almost wilaya nzima ya Ubungo.Na leo naamka asubuhi hapa Kimara hakuna umeme,umeshakatika.Hebu tuambieni wakuu wa nchi hii tunaishi vipi kwa hali hii?!
Tumepokea taarifa kwa hatua zaidi tafadhali
 
Tanesco Rukwa mnaua viwanda vidogo vya vijana walioamua kuwa wajasiliamali kwenye welding, fisheries, milling n.k

Mnakata umeme kwa zaidi ya saa 15/24 kitu ambacho kinafanya watu washindwe kufanya kazi
Sababu zenu kuwa transformer yenu kubwa inayounga umeme kutoka Zambia ina matatizo, ,tunaona ni ya uongo maana sumbawanga mjini mnawapa umeme saa nyingi kuliko wilaya zingine km kalambo, dc na nkasi

Tanesco, acheni kuwarudisha watu nyuma, acheni kuua ajira za vijana.
Leo watu hawana uhakika wa kazi zao kisa umeme.
Inauma sana, chukueni hatua
 
Unakata umeme mchana kutwa nzima, ,alafu unarudisha usiku wa manane, kisha unakata tena alfajiri!!!

Kutwa nzima umeme hakuna! Hizo kazi zitafanywa usiku??

Watu watasaga usiku? Watatengeneza milango, madirisha, vitanda n.k usiku?

Mnawaingizia wajasiliamali wa usindikaji wa samaki gharama kubwa za kutumia generator, na bado serikali inapandisha Bei ya mafuta!!!!

Hiyo maintenance itachukua muda gani? Mbona mnaturudisha kwenye hali iliyotufanya tushindwe kujiajiri!!??

TANESCO
 
Naona TANESCO wameshatuona sisi watz ni wajinga, Sasa huu ndio wakati muafaka wa kulikataa hili shirika Kwa kuandaa maandamano nchi nzima kushinikiza hili shirika livunjwe ili yaje makampuni mbali mbali kutoa huduma ya umeme kama wanavyofanya kwenye simu
Hii nakubaliana nawewe

Bora yaletwe makampuni mengine tu

Umeme imekua shida mno siku hizi

Tafikiri wanatufanyia hisani yaan kama wanatupa bure
 
Hivi sisi wakazi wa mwanza tumewakosea Nini TANESCO???
Huu ni mgao au mgawano??
Tuanze na wilaya ya ilemela kata ya kirumba kuanzia Jana saa5 usiku mpaka Sasa alfajir hii hakuna Umeme...Ukipiga simu EMERGENCY hawapokei...TUNAPIGA Tena simu emergency ya makao makuu vile vile sim haipokelewi..
Vile vile juzi kuamkia Jana wilaya ya nyamagana Maeneo ya Nyakato Nundu umeme ulikatika siku nzima...
Hivi tumewakosea Nini???ukiwapata mfundi lazma uwatangazie posho ndio waje waanze kufatilia chanzo....
Kwakweli Mama yetu SSH alikosea saana kumtoa Mh KALIMANI ktk hio wizara ya NISHATI
Sio mwanza tu hili tatizo ni karbu kila mkoa watu wanalalamika
 
Mmekata umeme last week jtatu,jnne,jtano,jmosi siku nzima no working!wiki hii jana jtatu mmekata saa moja asubuhi mpaka saa nne usiku eneo kubwa kuanzia Manzese mpaka Kimara,almost wilaya nzima ya Ubungo.Na leo naamka asubuhi hapa Kimara hakuna umeme,umeshakatika.Hebu tuambieni wakuu wa nchi hii tunaishi vipi kwa hali hii?!
Sijui tutaishije sisi ambao biashara zetu mostly zinategemea umeme

Yaani mtu kama una mtaji mkubwa unafunga limtambo la solar likubwa
 
TANESCO ivi sisi wafanya biashara was hapa kimara mwisho njia ya bonyokwa tumewakosea nini? Jana mlikata umeme kuanzia saa 8:30 aubuhi mkarejesha saa 07:48 usiku, sasa I've mmeka tena umeme , Kila siku huu mtaa mnakata umeme ..shida ni Nini ?
 
TANESCO ivi sisi wafanya biashara was hapa kimara mwisho njia ya bonyokwa tumewakosea nini? Jana mlikata umeme kuanzia saa 8:30 aubuhi mkarejesha saa 07:48 usiku, sasa I've mmeka tena umeme , Kila siku huu mtaa mnakata umeme ..shida ni Nini ?
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
Eneo mwananyamala


Wilaya ya kinondoni


Namba ya 0717505745

Tatizo ni nyaya ya neutral kupitisha umeme

tatizo limeanza toka jumatatu ya 29/11/2021 baada ya umeme kukatika na kurudi

tumejaribu kuwatafuta kwa namba za simu both emergency na tanesco office hawapokei simu
 
Nimenunua umeme a/c no
54 1722 4342 7 mpaka sasa sijapata token. Tatizo ni nini?
Halotel wanasema pesa imeshatumwa Tanesco.
 
Magu alisema mtanikumbuka sio kwa mabaya bali kwa mazuri

Yani siku hizi Tanesco mnajiamulia tu kukata kata umeme

Jana hapa Chamazi mlikata umeme sa 1 usiku mkarudisha sa 6 usiku na Leo tena sa 1 hii mmeshakata sijui mtarudisha sa ngapi

Muheshiwa waziri mkuu Majaliwa ebu mtumbue huyu meneja wa tanesco kanda ya mbagala
 
Maana nasikia huwa wanapewa mzigo mameneja ili umeme upelekwe viwandani

Mgao gani kila siku kuanzia SAA 1 hadi usiku wa manane
 
@Ncherry1 bora wewe ndugu yangu umelipia mwezi wa 10 wenzako tumelipia mwezi wa 9 mwanzoni kabisa hadi leo hakuna dalili ya kufungiwa umeme huko mwisho wa reli, jibu ni hilo hilo kila mara hakuna mita, ila kinachoshangaza wengine wanafungiwa sijui mita zinatoka wapi.
Nimelipa wa Tisa had Leo Sina umeme jiran yangu kalipa wa nane Hadi leo kimya

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Tanesco- Dodoma jiji ni Janga...,Eti wamesimamisha kutoa control number/malipo kwa wateja ambao connection ina involve nguzo 1.....,NA HAILEWEKI WAMESIMAMISHA MPAKA LINI.....??!. [ENZI ZA MAGUFULI HAYAKUWEPO HAYA]
Shirika la Umeme Tanzania - (Tanzania Electric Supply Company Limited - TANESCO), Tunaomba mtupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri kupitia huu uzi nasi tutawajibu.

Tunawaomba mzingatie yafuatayo ili kurahisisha ufafanuzi na ufumbuzi wa tatizo au taarifa husika;

1. ENEO HUSIKA

(Mnaweza kuwa eneo moja lakini mnahudumiwa na transfoma au njia ya kusambaza umeme (feeder) tofauti)

2. NAMBA YA SIMU

(Wakati mwingine umeme upo kote isipokuwa kwako hivyo na rahisi kuwasiliana na wewe)

3. KARIBU NA NINI

(Kuna alama vitu au watu mashuhuri karibu na eneo lako mfano ofisi ya Serikali ya Mtaa, Mahakama, Kituo cha Polisi nk)

4. JINSI YA KUFIKA MAKAZI YAKO

(Toa ufafanuzi wa jinsi ya kufika makazi yako,chukulia unamuelekeza mtu ambaya hajawahi kufika kabisa)

5. MKOA,WILAYA NA KITONGOJI/KIJIJI

(Taarifa hii ni muhimu sana kusaidia kubaini eneo husika lipo wapi kwani yapo maeneo yanayofanana kwa majina lakini yapo Mikoa tofauti mfano Magomeni ipo Dar es Salaam na Mkoa wa Mtwara pia.)

6. KAMA NI TATIZO LA MITA NINI KINATOKEA UKIWEKA UMEME

(Kila mita ina ujumbe wake unaoashiria kitu fulani hivyo kubainisha ujumbe kunamsaidia mpokea taarifa kukupatia maelezo sahihi mfano mita namba 24339173921 inaonyesha error 77)

7. KAMA NI KUSHINDWA KUNUNUNUA UMEME UNAPATA UJUMBE GANI NA UNANUNUA KWA NJIA GANI

(Ujumbe huu ni muhimu sana kuweza kubaini chanzo cha tatizo pamoja na njia iliyotumika kununulia umeme mfamo Mpesa, Tigopesa, Maxcom nk)

TUNAENDELEA KUWASIHII WATEJA WETU KUZINGATIA UTOAJI WA TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA ZAIDI KUTOKA TANESCO.

ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA BORA KUTOKA TANESCO

Vilevile pitia threads hizi kupata Maelezo ya ziada;

LUKU:Mfumo wenye Tija kwa Wateja na TANESCO

Fahamu mita za LUKU zinazofungwa majumbani

Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO

Kw mawasiliano Kituo cha Miito ya Simu (+255) 22194400 or (+255) 768 985 100 Mitandao ya kijamii Tanescoyetu (@tanescoyetu) | Twitter Facebook: Tanesco Yetu

HAPA CHINI NI NAMBA ZA SIMU ZA MIKOA

Ofisi ya Mkoa wa Mbeya Simu ya Mkononi (+255) 757 529 380 ya Mezani (+255) 252 504 219

Ofisi ya Mkoa wa Ilala Simu ya Mkononi (+255) 784 768 586 ya Mezani (+255) 222 133 330

Ofisi ya Mkoa wa Kinondoni Kusini (Magomeni) Simu ya Mkononi (+255) 715 271 461/ (+255) 784 271 461

Ofisi ya Mkoa wa Kinondoni Kaskazini (Mikocheni) Simu ya Mkononi (+255) 784 768 584 / (+255) 716 768 584 ya Mezani (+255) 222 700 367/ (+255) 222 701 602 / (+255) 222 774 098

Ofisi ya Mkoa wa Temeke Simu ya Mkononi (+255) 712 052720 / (+255) 758 880155 / (+255) 732 997361

Ofisi ya Mkoa wa Pwani Simu ya Mkononi (+255) 78 5122020 / (+255) 65 7108782ya Mezani (+255) 23 2 402 386

Ofisi ya Mkoa wa Arusha Simu ya Mkononi (+255) 75 8 174 343 Mezani (+255) 272 506 110

Ofisi ya Mkoa wa Tanga Simu ya Mkononi (+255) 658 122 412/ (+255) 687 677 667 Mezani (+255) 27 2 646 779

Ofisi ya Mkoa wa Kilimanjaro Simu ya Mkononi (+255) 765 397 925/ (+255) 682 771 310 Mezani (+255) 272 755 007/8

Ofisi ya Mkoa wa Manyara Simu ya Mkononi (+255) 689 795 599 / (+255) 75 9 534 130 Mezani (+255) 272 530 590

Ofisi ya Mkoa wa Mwanza Simu ya Mkononi (+255) 759 777 786 / (+255) 687 910 202 Mezani (+255) 282 501 060 / (+255) 282 500 090

Ofisi ya Mkoa wa Geita Simu ya Mkononi (+255) 744 085 696 Mezani (+255) 28 2520330

Ofisi ya Mkoa wa Kagera Simu ya Mkononi (+255) 78 5 787 898 / (+255) 75 3 120 701 Mezani (+255) 282 220 061

Ofisi ya Mkoa wa Mara Simu ya Mkononi (+255) 762 165 087 / (+255) 732 985 672

Ofisi ya Mkoa wa Simiyu Simu ya Mezani (+255) 282 700 180

Ofisi ya Mkoa wa Dodoma Simu ya Mkononi (+255) 782 161 643 Mezani (+255) 262 321 728

Ofisi ya Mkoa wa Morogoro Simu ya Mkononi (+255) 68 4889272 / (+255) 65 4829046 Mezani (+255) 232 613 501/2

Ofisi ya Mkoa wa Singida Simu ya Mkononi (+255) 71 4 477 445 / (+255) 732 960 924 / (+255) 689 373 757 Mezani (+255) 262 502 133

Ofisi ya Mkoa wa Tabora Simu ya Mkononi (+255) 786 558 510 / (+255) 763 162 868

Ofisi ya Mkoa wa Shinyanga Simu ya Mkononi (+255) 754 521 070 Mezani (+255) 28 2762120

Ofisi ya Mkoa wa Kigoma Simu ya Mkononi (+255) 78 3720598 Mezani (+255) 28 2802668

Ofisi ya Mkoa wa Katavi Simu ya Mkononi (+255) 68 8345200

IMETOLEWA NA:- Ofisi ya Uhusiano

TANESCO Makao Makauu.

NAMBA ZA SIMU ZA MADAWATI YA DHARURA YA TANESCO MIKOA YOTE

1. Ilala

0222133330/ 0784 768586/ 0715 768586.

2.Kinondoni Kusini (Magomeni)

0784271461/ 0715271461

3. Kinondoni Kasikazini(Mikocheni)

0784 768584/ 0716 768584

4. Temeke

0222138352/ 0732 997361/ 0758881055/ 0712 052720

5. Pwani
078 5122020/065 7108782/023 2402386

6. Mbeya
0759 777781/0787 023422


7.Arusha
0758174343/
0622612501/
+255 27 2506110

8.Tanga
0658 122 412/0687 677 667/ 027 2646 779

9. Kilimanjaro
0765 397 925/0682 771 310/ (+255) 272 755 007/8

10 Manyara
0689 795 599/ 0627938951

11. Mwanza
0759 777 786/0687 910 202/
(+255) 282 501 060 / (+255) 282 500 090

12. Geita
0744 085 696/(+255) 28 2520330

13.Kagera
078 5 787 898 / 075 3 120 701/(+255) 282 220 061

14.Mara
0788 950 688/
028 262 2020/
0762 165 087

15.Simiyu
+255 282 700 180/0626383440/0745044072

16. Dodoma
0782 161 643/(+255) 262 321 728

17. Morogoro
068 4889272 /065 4829046/ (+255) 232 613 501/2

18 Singida
071 4 477 445 /0732 960 924 / 0689 373 757/(+255) 262 502 133

19. Tabora
0786 558 510 /0763 162 868

20. Shinyanga
0754 521 070/(+255) 28 2762120 /
0783 521 070

21. Kigoma
078 3720598/(+255) 2988226

22. Katavi
0688345200

23. Rukwa
0252161120/0768879813
24. Songwe
0684 611716/0763 430381.

25. Ruvuma
0252602281/0763 194 979/0787 758 986

26. Njombe
0744703988

27. Mtwara:
0789 999942/023 2333902

28. Iringa 0262702019/0739203015

29. Lindi
0752518247/0685692786


Kituo cha Miito ya simu/Call Centre Makao Makuu

0768 985 100/0222194400

Facebook
www.facebook.com/tanescoyetu

Twitter
www.twitter.com/tanescoyetu

Tovuti
www.tanesco.co.tz

Barua pepe
Customer.service@tanesco.co.tz

Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
 
Tanesco- Dodoma jiji ni Janga...,Eti wamesimamisha kutoa control number/malipo kwa wateja ambao connection ina involve nguzo 1.....,NA HAILEWEKI WAMESIMAMISHA MPAKA LINI.....??!. [ENZI ZA MAGUFULI HAYAKUWEPO HAYA]
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
 
Huu umeme mnaokatakata huku mbezi beach hata siwaelewi kabisa. Imagine asubuhi yote hii mshakata Mara tatu, hii ni tatizo. Kwa hii hasira mnayoileta kwa wananchi sitarajii kuipenda serikali hata kidogo.
 
86 Reactions
Reply
Back
Top Bottom