TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

nimeomba luku ilala mkoani ya kuongeza kwenye duka leo mwezi moja na nusu sijapata hata conrol nambar inakuwaje
 
TANESCO munatutesa sisi huku Mtoni Kijichi Mgeninani. Tangu jana umeme mumekata hamujarejesha kwenye line yetu.
Sijui mumetusahau au vipi?

Tukipiga simu zenu hazipatikani jamani

Tuhurumieni mweeeeee
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
Wilaya Temeke
Eneo Mtoni Kijichi Mgeninani
Tatizo kukosa huduma ya umeme
Toka jana asubuhi

Na ya simu 0686526225

Hatuna namba ya taarifa hamupokei simu
 
Kwenu Tanesco Kibaha mkoa wa pwani.
Kumekua na ukatikaji wa umeme eneo la Kongowe kuanzia Kongowe mashine ya maji Hadi Kigelo kwenye barabara ya Kongowe-Soga Kila inyeshapo mvua. Hata muda huu hakuna umeme tangu Ile mvua ya Leo ilipoanza kunyesha. Nadhani tatizo mnalijua maana linajirudia Mara kwa Mara. Jana umeme umerudi kwenye saa nne za usiju. Wakazi wa eneo hili wanaomba mrekebishe hili tatizo.
Natanguliza shukrani.
Wenu katika ujenzi wa taifa.
 
TANESCO NYIE NI MATAKATAKA KABISAA....NA MNAKERA VIBAYA MNO,DAWA YENU NI KUWATAFUTIA MSHINDANI.

HAIWEZEKANI MKATE UMEME TOKA SAA TATU KARIBIA JIJI ZIMA LA DAR ALAFU.MPAKA MUDA HUU SAA MBILI NA MADAKIKA BADO HAMJARUDISHA NA MKO KIMYA BILA UFAFANUZI WOWOTE ULE.

TAKATAKA KABISA NYIE.
 
Et Wanasema wanafanya service 😅 tuwe wapole.....service gani mwezi mzima? Laiti yule Baba angelikuwepoooo
 
Wanadhani waTanzania ni wajinga Sana wakati wao ndo wajinga na mazwazwa....yaani mpaka muda huu inaelekea saa nne usiku mhna UMEME toka saa tatu asubuhi.....huu mshirika umejaa mapuuzi tu.

Hizo service wakati wa yule baba zilikuwa hazifanyiki au???

Rubii huo uwongo wao wala usiusikilize dear.
 
nimeomba luku ilala mkoani ya kuongeza kwenye duka leo mwezi moja na nusu sijapata hata conrol nambar inakuwaje
Mimi nimeomba kuwa na luku separate eneo la biashara. Toka mwezi wa 9 mpaka Leo sijapata control number. Piga simu, fuatilia .... Ni danadana mtindo mmoja 😭 TANESCO
 
Wanadhani waTanzania ni wajinga Sana wakati wao ndo wajinga na mazwazwa....yaani mpaka muda huu inaelekea saa nne usiku mhna UMEME toka saa tatu asubuhi.....huu mshirika umejaa mapuuzi tu.

Hizo service wakati wa yule baba zilikuwa hazifanyiki au???

Rubii huo uwongo wao wala usiusikilize dear.
Naona TANESCO wameshatuona sisi watz ni wajinga, Sasa huu ndio wakati muafaka wa kulikataa hili shirika Kwa kuandaa maandamano nchi nzima kushinikiza hili shirika livunjwe ili yaje makampuni mbali mbali kutoa huduma ya umeme kama wanavyofanya kwenye simu
 
Kabisaa chief....hawa jamaa wanatuchukulia poa sana
 
Hivi TANESCO ubaguzi huu mtauacha lini? Yaani watu tunaomba umeme miaka nenda miaka rudi lakini hamtaki kutupa umeme...hii nchi yetu sote inauma sana...
 
Hivi sisi wakazi wa mwanza tumewakosea Nini TANESCO???
Huu ni mgao au mgawano??
Tuanze na wilaya ya ilemela kata ya kirumba kuanzia Jana saa5 usiku mpaka Sasa alfajir hii hakuna Umeme...Ukipiga simu EMERGENCY hawapokei...TUNAPIGA Tena simu emergency ya makao makuu vile vile sim haipokelewi..
Vile vile juzi kuamkia Jana wilaya ya nyamagana Maeneo ya Nyakato Nundu umeme ulikatika siku nzima...
Hivi tumewakosea Nini???ukiwapata mfundi lazma uwatangazie posho ndio waje waanze kufatilia chanzo....
Kwakweli Mama yetu SSH alikosea saana kumtoa Mh KALIMANI ktk hio wizara ya NISHATI
 
Hivi sisi wakazi wa mwanza tumewakosea Nini TANESCO???
Huu ni mgao au mgawano??
Tuanze na wilaya ya ilemela kata ya kirumba kuanzia Jana saa5 usiku mpaka Sasa alfajir hii hakuna Umeme...Ukipiga simu EMERGENCY hawapokei...TUNAPIGA Tena simu emergency ya makao makuu vile vile sim haipokelewi..
Vile vile juzi kuamkia Jana wilaya ya nyamagana Maeneo ya Nyakato Nundu umeme ulikatika siku nzima...
Hivi tumewakosea Nini???ukiwapata mfundi lazma uwatangazie posho ndio waje waanze kufatilia chanzo....
Kwakweli Mama yetu SSH alikosea saana kumtoa Mh KALIMANI ktk hio wizara ya NISHATI
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
 
Hivi TANESCO ubaguzi huu mtauacha lini? Yaani watu tunaomba umeme miaka nenda miaka rudi lakini hamtaki kutupa umeme...hii nchi yetu sote inauma sana...
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
 
86 Reactions
Reply
Back
Top Bottom