Narudia tena,TANESCO mvua hizi zinanyesha,na bado hatutaki umeme ukatike.Ndio maana mnalipwa mishahara kuhakikisha huduma hii ipo muda wote.Acheni huu ujinga wa kukata umeme na kusingizia hitilafu zisizo na kichwa wala miguu.Rudisheni umeme na hakikisheni haukatiki,period.
 
Tanesco hivi sisi watu wa Moshi-Kobosho meneo ya Shule ya Msingi Marawa tumewakosea nini? Inaenda wiki ya pili sasa hatuna umeme,Nimetoa taarifa kwenye Tanesco App mara kadhaa,Nikipiga simu hampokei.Chaajabu jirani yangu mwenye line ingine yeye kwake umeme upo! Kama ni hela semeni tuwape ili tupate umeme,Tumechoka na hii adha.
 
Tunashukuru sana REA kwa kutuwekea nguzo hali inayotutia moyo kuwa huduma ipo karibu!! Haya ni matunda ya uchapakazi wa viongozi wa awamu hii.

Tunaomba basi muweze kulimalizia zoezi lenu hili mkoa huu wa Pwani mtuwekee nyaya na kutuwekea umeme sisi wananchi.
 
Tanesco hivi sisi watu wa Moshi-Kobosho meneo ya Shule ya Msingi Marawa tumewakosea nini? Inaenda wiki ya pili sasa hatuna umeme,Nimetoa taarifa kwenye Tanesco App mara kadhaa,Nikipiga simu hampokei.Chaajabu jirani yangu mwenye line ingine yeye kwake umeme upo! Kama ni hela semeni tuwape ili tupate umeme,Tumechoka na hii adha.
Tafadhali tupatie namba yako ya taarifa na namba ya simu kwa hatua zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona Tanesco mnapanic hivyo,,mimi nina uthbtsho wotee juu yenu ninyi kuomba rushwa nikiamua kuzivujisha thbtsho zote sidhani kama mnaweza pona hapo ofisini kwenu,uthbtsho wa video,sound,n.k zote ninazo ila tu nimekaa kimyaa kulinda uongozi mzima hapo,maana Tanzania bila rushwa inawezekana lakini sio kwa asilimia 100.

Kwahyo ndugu admin usichukie kwahili wewe kubali tu kuwa hapo kwenu rushwa ipo sanaaa tu,siku zote penye mamba wengi kenge huwa hawakosi,kwahyo be cool tu,
System ipo na inafanya kazi.
Taratibu zote hizo zipo kwenye mkataba wa huduma kwa wateja je wewe umeomba umeme lini? Wilaya na namba yako ya simu? Je kuna mahali tumekuomba rushwa? Kama ndio nenda TAKUKURU ili sheria ichukue mkondo wake au leta taarifa kamili kwa viongozi wa shirika kwa hatua zaidi badala ya kuchafua taswira yetu bila ushahidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe toa tu hela ya soda maana hela ya soda au ya kiwi ya viatu haina shida kwa surveyor wa Tanesco nguzo yako itakuja fasta tu ohooooo,,
Wewe zubaa tu utaletewa mpaka mwakani 2021.
Binafsi nicho ona Voda ongozi wa Tanesco muangalie na kufuatilia kwa makini kero znazotolewa humu, maana wanaochafua taswira ya Tanesco ni baadhi ya watumishi sio wote,mfano unakuta unaenda Tanesco lkn kitendo cha kutatua tatizo linachukua muda mrefu sana,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni luku mkuu na sio nguzo,nguzo zinaweza zikawa zangu naweza nunua hata kwa qwihaya pale mafinga tanesco wakazitumia kuniwekea.

Qwihaya anawauzia tanesco 30,000/= na zaidi ya hapo haifk 40,000/= kwa nguzo moja semeni hili walitolee ufafanuzi wao wanauzia wananchi shngapi???? Nahitaji Tanesco waje hapa.
Ile nguzo ni mali ya shirika na sio mteja, ni kama ardhi unayomiliki ila sio yakwako
 
Napendekeza Tanesco wawalazimishe kwa kutoa notisi ya miezi sita wenye nyumba hasa Dar es Salaam kubadilisha wiring za nyumba zao maana hazifai.

Pia Tanesco watoe pendekezo kwa wizara husika inayoshughulika na makazi kupitisha utaratibu kwa nyumba za kupangisha kufungwa vifaa vya kuhesabu unit kwa kila chumba cha kupanga ili kuboresha matumizi sahihi na malipo sahihi kulingana na mahitaji ya wateja (watumiaji) na sio kumhesabu tu mwenye nyumba kama mteja wa Tanesco wakati hawajali ata kufanya ukarabati wa mifumo ya umeme kwenye nyumba zao matokeo yake wapanganji ndio wanapata tabu.
 
TANESCO hii line ya umeme ya Mavurunza ina tatizo gani?mbona mnakata sana umeme?Mavurunza,Matangini,Korogwe,Kam College,Kimara Mwisho,Michungwani,kulekea Baruti na Ubungo kwa line hii ya upande wa pili wa barabara,ni line inayoishia Kimara mwisho.
Inakatika mno umeme hivi sasa.Inasumbua sana.
 
Mamlaka ya maji Dar es Salaam dawasco
Kwa sasa wanajitahidi sana
Maji yapo kila kona na ikitokea dharura wanatoa taarifa mapema tu kwa wateja

Lakini nyie TANESCO kwa sasa kuhusu umeme Dar es Salaam ishakuwa kero

Nakumbuka kale kawimbo umeme na maji Tanzania ishakuwa kero¶¶¶,, kerooo,, ¶¶¶kerooo

Nipo Tabata dampo wilaya ya ilala
Mkoa wa Dar es Salaam
Umeme ni kero Tangia jana
Mnakata asubuhi unarudi jioni
Tatizo ni nini?
Si mlisema mgao wa umeme itakuwa ni historia leo tunakwenda miaka 5 ya utawala awamu ya 5
Mgao wa umeme upo pale pale lakini kinyemela hamsemi kama kuna mgao Lah.. Upo kimya wananchi tunapata hasara... Nyie mnapata mishahara huu si uungwana hata kidogo toeni taarifa babu acheni uchawi..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu mji ulitangazwa kuwa jiji takriban mwaka mmoja sasa. Hata hivyo, huduma nyingi hazijaboreshwa zikiwemo huduma za umeme.

Kwa siku za karibuni kumekuwa na ukatikaji wa umeme tena kwa muda mrefu bila taarifa yoyote Kwa umma hasa eneo la kisasa Nyumba 300. Hii siyo Sawa na mnaondoa hadhi ya mji wenu kupewa hadhi ya jiji au mlitangazwa jiji kisiasa wakati hamjajiandaa kifikra na miundombinu. BADILIKENI kama wenzenu wa miji mingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kibaya zaidi hakuna hata taarifa inayotolewa baada ya umeme kurudishwa. Mfano leo alfajiri saa 10:45 umeme ulikosekana kwa takriban dakika 30.
 
Back
Top Bottom