Ndugu mpendwa mteja wetu
Tunaomba utapatie swali ambalo halijajibiwa tulifanyie kazi.Tupo kukuhudumia wewe muda wote

Kuna eneo la Mtaa wa Kigogo Kati wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salam liliwekwa nguzo zenye taa miaka takriban mitano iliyopita! Jambo la kushangaza ni kwamba umeme uliwashwa siku moja tu kwa majaribio na tangu wakati huo haujawashwa tena, hadi baadhi ya nguzo zimeanza kuoza na zitaanguka wakati wowote!
Tatizo ni nini? Kwa nini umeme haujawahi kuwashwa kwa kipindi chote hicho? Ina maana hamna kitengo cha Survey kugundua dosari?
 
Nampemda huyu kijana wa TANESCO anavyojibu maswali as if ni auto answer au 🤖 robot 😂.

Ila akizidiwa na maswali anazima data anasepa 😂 hahahaaaaa...
 
Habari za Leo.naomba kujua ni kwanini Tanesco wameniongezea gharama za unit za umeme ,awali nilikuwa nikinunua umeme wa sh5000 napata unit 24, lakini kwasasa nikinunua umeme wa sh 5000 napata unit 14.1 yaani being zimeongezeka Mara 2 kimyakimya .
Serikali ya viwanda na gharama hizi tutafika kweli???!!
Inaelekea wamebadili ule utaratibu wa WATUMIAJI UMEME WADOGO. Nami nilikuwa nanunua hivyo hivyo, na matumizi yangu kwa mwezi, ni unit 50. Bila taarifa, naona nashindwa kununua kwa mpesa. Napewa namba nipige ili nipewe namba za kubadirishia mfumo wa kununulia.
Kama wameamua kufuta ule utaratibu, kwa nini kimya kimya?
 
Tunaomba namba yako ya simu tufatilia swala hili mpendwa mteja wetu
 
Habari za Leo.naomba kujua ni kwanini Tanesco wameniongezea gharama za unit za umeme ,awali nilikuwa nikinunua umeme wa sh5000 napata unit 24, lakini kwasasa nikinunua umeme wa sh 5000 napata unit 14.1 yaani being zimeongezeka Mara 2 kimyakimya .
Serikali ya viwanda na gharama hizi tutafika kweli???!!
Matumizi yako ni makubwa ndio maana tumekuongezea. Umevuka kwenye matumizi ya kimaskini umeingia kwenye matumizi ya kitajiri. Hongera kwa hilo
 
Jamani tanesco VP?nilienda oficin mbezi kubadili tariff, nikajaza form ,nilaambiwa nitajuzwa,,ilikuwa no mwezi was tatu mpaka Leo sijapigiwa simu ..tatizo nini? Au mnatufukuza kwa kutuambia tujaze form?
Naona hamtaki kujibu
 
Tunaomba namba yako ya simu tufatilia swala hili mpendwa mteja wetu

Namba ya simu niiweke hadharani? Kwanini nisikuelekeze tu?

Kuna stand maarufu kwa jina la Randa Bar pale kwenye Transformer lenu kuelekea barabara ya kushoto - KIBIA STREET!
 
Hii wizara itawasumbua sana, ,,,, huongo wa kwenye vyombo vya habari kujinasibu kuwa wanamove forward kumbe hakuna kitu,,,, Ndugu Sospeter Muhongo ndio alikuwa anatekeleza kauri mbiu ya kuangaza maisha yetu. .... ila huyu hamna kitu Tanesco limekuwa miongoni mwa mashirika mabovu Tanzania kuwahi kutokea, ,,, kumtoa Muhongo ilikuwa ni kuruka mkojo na kukanyaga kinyesi, ,,,,,,,
 
Uongozi wàTanesco kwanini kuunganisha umeme kwa kujenga Nguzo 1 ichukue muda wa siku 60 wakati ni kazi ya masaa 3 tu?
 
Separation meter .

Ninauliza huu utaratibu wa saparation meter ninayotaka kuweka kwenye vibanda vya biashara.

Nimeenda kuulizia utaratibu wa kuwekewa hiki kifaa nikashangazwa na maelezo niliyopewa na staff wa Tanesco!

Nimeambiwa baada ya kufanya wirering natakiwa kulipia takribani laki3 na ushee ili niunganishiwe!

Hii bei imekaaje kuwa sawa na anayeanza kabisa mchakato (beginner)?

Compound ni moja, kuongeza mita ya pili ninapewa gharama ya kuvuta umeme sawa kabisa na mtu anayeanza?

Ninaomba ufafanuzi wenu Tanesco hili limekaaje? Je limekaa sahihi ki mantiki au linafanywa kwa mazoea?
 
Kuweka mita ya pili gharama ni sawa na mita ya kwanza kwa vifaa vitakavyotumika kukufungia umeme ni sawa na vile vilivyotumika hapo awali
 
TANESCO kuna shida gani katika mradi wa REA Moshi vijijini eneo la SHABAHA wamesimika nguzo na kutandaza waya baadhi ya maeneo ila ni zaidi ya mwez sasa hakuna kinachoendelea. Nini kinakwamisha kuunganishia watu umeme tuendeshe viwanda vyetu?
 
Back
Top Bottom