Tanesco mnafeli wapi kumpangia mteja matumizi ya umeme..... fanyeni kama vifurushi kwenye mitandao ya simu mtu atumie umeme tokana na pesa yake.... Tuondoeni kwenye utumwa huo.
Tunaomba maelezo zaidi ya mapendekezo yako ya nini kiboreshwe mpendwa mteja wetu
 
Habari za Leo.naomba kujua ni kwanini Tanesco wameniongezea gharama za unit za umeme ,awali nilikuwa nikinunua umeme wa sh5000 napata unit 24, lakini kwasasa nikinunua umeme wa sh 5000 napata unit 14.1 yaani being zimeongezeka Mara 2 kimyakimya .
Serikali ya viwanda na gharama hizi tutafika kweli???!!
 
Naomba kusaidiwa mzazi wangu ameomba kuunganishiwa umeme lkn sasa takribani miezi 3 imepita kila akienda tanesco ofisi ndogo ya wilaya wanamzungusha tu hawatoi maelezo yenye kuleta matumain kuwa ataweza unganishiwa huo umeme
Mara ya kwanza wamesema tusubir wabadilishe nguzo kwakuwa nguzo iliyokaribu yetu imeoza ndio watukadirie gharama
Mara ya 2 tubadilishe fomu kwakuwa sasa kuna punguzo la bei
Na sasa fomu haipatikani
Kwangu mm haya ni mazingira ya rushwa naomba mtupatie majibu sahihi nn tatizo tupo teyari kulipia gharama kwa mujibu wa taratibu iwe kunahitajika nguzo au hakuhitajiki nguzo
Maeneo nyumba ilipo ni Mkoa morogoro, wilaya Kilombero tarafa Kidatu kata kidatu kijiji Mkamba A karibu na msikiti wa Suni Jina la mmiliki ni Abdallah Mayowela
Mtoa taarifa ni mimi mwanaye Hassanaly Mayowela 0764726177 email mayowelah2019@gmail.com
 
Tunaomba maelezo zaidi ya mapendekezo yako ya nini kiboreshwe mpendwa mteja wetu
Huu utaratibu wa mtu mwenye matumizi makubwa akinunua umeme anapata units ndogo na mwingine akinunua kwa bei ileile anapata nyingi kisa yeye anamatumizi madogo huu sio utaratibu mzuri.... pendekezo langu ni kwamba umeme wa fedha kadhaa uwe na specific units... sio units za elfu kumi za mteja fulani zitofautiane na za mteja mwingine. Mtu atumie umeme tokana na mfuko wake ukiisha kabla ya mwezi anaweza ongeza kwa units sawa na mtu anaemaliza mwezi kwa units zilezile.... nawasilisha....
 
Tunaomba maelezo zaidi ya mapendekezo yako ya nini kiboreshwe mpendwa mteja wetu

Pia kwanini ukinunua luku haiwezi kujiingiza yenyewe kama kwenye ving'amuz vya tv?? Mfano ukinunua bando la startimes kwenye simu, automatically kingamuzi chenyewe kinaji unlock, hauna haja ya kwenda tena kwenye kingamuz uanze kuingiza manamba.. Inabid mbadilike.. pia itakua rahisi kwa mtu kumnunulia mwingine units kama vile ilivyo kwenye mtu kutumiwa vocha ya simu
 
Ndugu mpendwa mteja wetu swala hili tunalifanyia kazi
 
Navyo wafahamu TANESCO tangu shirika limepewa serikali yaani halina ubunifu wala huduma kwa wakati kwa wateja wao kabisa yote mutakayo jibiwa itakuwa ndoto kukamilika tuombe uzima
 
Nilishindwa kuunganishiwa umeme kijijini kwa wazazi kutokana na kuombwa gharama kubwa za kuunganishiwa mnanisaidiaje mfano niliambiwa laki Tatu kwa kila nguzo
 
Kwanini TANESCO mmeweka umeme barabarani tu afu maeneo yenye makazi mengi na watumiaji wengi hayana umeme kiasi kwamba umeme inakuwa kama huduma ya starehe badala ya huduma ya msingi na muhimu, mfano mvuti, dondwe, Chanika , fikeni maeneo ya yenye wananchi na muwawekeeni umeme ,
 
Pia kwanini ukinunua luku haiwezi kujiingiza yenyewe kama kwenye ving'amuz vya tv?? Mfano ukinunua bando la startimes kwenye simu, automatically kingamuzi chenyewe kinaji unlock, hauna haja ya kwenda tena kwenye kingamuz uanze kuingiza manamba.. Inabid mbadilike.. pia itakua rahisi kwa mtu kumnunulia mwingine units kama vile ilivyo kwenye mtu kutumiwa vocha ya simu
naona unapigia mbuzi gitaa
 
Tunaomba maelezo zaidi ya mapendekezo yako ya nini kiboreshwe mpendwa mteja wetu
Kuna wilaya inaitwa Tarime, sijawahi kuona sehemu yenye shida ya umeme kama pale, karibia kila siku umeme unakatika, sijui tatizo ni nini! Yaani utafikiri watoto wanachezea swichi, kuwasha na kuzima. Kila siku shida ni hiyo hiyo, kukata Mara baada ya dk tano unarudi, wakati mwingine usiju mji mzima hakuna umeme! Yaani ni shida tupu.
 
Eneo gani na namba yako ya simu mpendwa mteja wetu
 
Kwenye hoja hiyo hiyo nina kero kwa hawa TANESCO katika wilaya TARIME.

Huduma ya umeme ndani ya wilaya ya tarime imekuwa kama vile inamilikiwa na mtu binafsi
Umeme unakatwa muda wowote bila tarifa yoyote hata kwa siku tatu.
Shughuli nyingi zinasimama ukifika ofisini kwao hawa jamaa unaambiwa piga simu makao makuu ya mkoa Musoma, ukiwapigia hao wa Musoma unaambiwa wasiliana na ofisi za Tanesco wilaya.
Danadana inaendelea mwisho wa siku wananchi wanapata hasara kutokana na kukatika kwa umeme kusiko kwa msingi
Mapendekezo yangu ni kuwa Wahusika wamulikwe na shirika lenu na waelezwe hizi kero bayana vinginevyo waondoke maana watu wanapata hasara na hali yenyewe hii
Nawasilisha
 
Back
Top Bottom