TANESCO huu uhuni mliotufanyia leo watu wa sumbawanga ukome, mnapata wapi ujasiri wa kutukatia umeme zaidi ya masaa 8 bila kutupa taarifa? Tena iwe mwisho, hii huduma ya umeme hamtupi bure tunanunua huu ujinga ujinga wa kukatia watu umeme bila taarifa ikome kuanzia leo.

Sisi watu wa sumbawanga hatujazoea huu ujinga ujinga mnaotaka kutuanzishia masaa 8 kwetu ni mengi mno hatujazoea hata kidogo, huo utoto wenu wafanyieni hao hao vijana wa dar maana wao hata mkiwakatia wiki hawawezi kufanya kitu.

Nasisitiza hili suala lisijirudie tena iwe mwisho leo, huo upuuzi wenu wafanyieni hao ambao mlishawazoesha.
 
Wilaya ya Tarime hivi kuna nini maana karibia mwezi wa pili huu umeme unakatika kila siku mara 3 hadi 4, na sio kwa muda mfupi ni kwa masaa. Mfano unawashwa kwa nusu saa, halafu wanakata kwa masaa 5 unarudi kwa dakika 20 unakatika kwa masaa 4. Na siku nyingine kama juzi na jana umekatika kwa siku nzima (masaa kama 20 hivi). Hata apa ninapoandika hivi hamna umeme. Kama ni hivi, nini maana ya kuwa na umeme si bora mngefungua hii mitambo yenu tujue kabisa hamna umeme wilaya ya Tarime. Hata taarifa hawatoi. Watu watafanyeje biashara kwa hii hali?.
 
Nimelipia kufungiwa umeme toka january hadi leo nazungushwa tu sijui nini shida kituo cha HIMO MOSHI KILIMANJARO

Ac 991030719141
Received 990115294553
Kupitia EC100299949021

Mbona hamnipi jibu nini shida hapo au hapa wengine hawajibiwi?
 
kero yangu ni kuunganishiwa umeme mimi nko buhongwa mwanza nguzo zimefika hadi kwenye nyumba ila waya wa mita 50 umemosekana nimefuatilia tanesco ofisi za mkolani toka mwezi february hadi leo naambiwa hakuna nyaya mkoa mzima wa mwanza .naomba msaada kwani imekuwa ni kero 0752296496
 
IMG_1903.jpg
 
Jamani tanesco VP?nilienda oficin mbezi kubadili tariff, nikajaza form ,nilaambiwa nitajuzwa,,ilikuwa no mwezi was tatu mpaka Leo sijapigiwa simu ..tatizo nini? Au mnatufukuza kwa kutuambia tujaze form?
 
TANESCO hivi kweli mnasubiri hadi mje mtumbuliwe ndipo mpambane kuleta umeme pembamnazi ,kisarawe II, Tundwi, Kimbiji?
Hiki kiburi mnatoa wapi,kwani sisi sio watanzania, sisi hatulipi kodi ?
Dsm imejaa mno watu wanahitaji makazi ila nyie mmekaa ofisini tu. Tunataka umeme huku.
Mnatukwaza sana, mwishowe nije nitukane bure kwa sababu yenu pumbavu.
 
Kuna eneo la Mtaa wa Kigogo Kati wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salam liliwekwa nguzo zenye taa miaka takriban mitano iliyopita! Jambo la kushangaza ni kwamba umeme uliwashwa siku moja tu kwa majaribio na tangu wakati huo haujawashwa tena, hadi baadhi ya nguzo zimeanza kuoza na zitaanguka wakati wowote!
Tatizo ni nini? Kwa nini umeme haujawahi kuwashwa kwa kipindi chote hicho? Ina maana hamna kitengo cha Survey kugundua dosari?
 
Kuna eneo la Mtaa wa Kigogo Kati wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salam liliwekwa nguzo zenye taa miaka takriban mitano iliyopita! Jambo la kushangaza ni kwamba umeme uliwashwa siku moja tu kwa majaribio na tangu wakati huo haujawashwa tena, hadi baadhi ya nguzo zimeanza kuoza na zitaanguka wakati wowote!
Tatizo ni nini? Kwa nini umeme haujawahi kuwashwa kwa kipindi chote hicho? Ina maana hamna kitengo cha Survey kugundua dosari?
Huko ni uswahilini na walituomba tusiziwashe tutawaharibia mishe zao. Tuliheshim mawazo yao
 
Tanesco mnafeli wapi kumpangia mteja matumizi ya umeme..... fanyeni kama vifurushi kwenye mitandao ya simu mtu atumie umeme tokana na pesa yake.... Tuondoeni kwenye utumwa huo.
 
Back
Top Bottom