Ndugu mpendwa mteja wetu sio kila anayeomba kubadilishiwa matumizi anabadilishiwa hapo hapo.kwanxa lazima akidhi vigezo pili tunaenda kumkagua nyumbani kwake.
Sasa Kama mnaenda kukagua nyumbani kwake ndio Mwezi mzima? Ina maana mmeelemewa na mizigo? Tangazeni kazi watu waombe wawasaidie. Kazi ya kukagua nyumbani inahitaji tena kukidhi vigezo? Mko serious kabisa kusema kumkagua mteja ichukue Mwezi mzima hujaenda? Lazima Kuna shida mahala.
 
Naomba kufahamu ni hatua gani zinafuata ili wananchi wa eneo lenye zaidi ya km 1.5 la mraba wanapohitaji huduma ya umeme kwa pamoja namaanisha eneo litakalohotaji nguzo zaidi ya 20, maana kuna mtaa upo manispaa ya songea unaitwa mkuzo-maliasili ni mwaka wa tatu sasa watu hawaletewi umeme... !?? Tunashindwa kuelewa mnafeli wapi Taneso au kila mtu napaswa kununua nguzo yake!?? Pia kuna baadhi ya watu wameamua kulipa kabisa hadi pesa za nguzo zao huko ili zoezi liharakishwe lakini hakuna kitu mpaka leo !?? Mnafeli wapi wakuu??

Naomba kujua utaratibu gani hapo unatumika hapo.. Na wanatakiwa wafanye nini hapo ili huduma iharakishwe??!.
 
Uongozi wa Tanesco naomba Muwasiliane na meneja wenu hapa ifakara. Siku ya pili sasa Transformer iliyopo hapa viwandani maarufu kwa Jibeha umeme upo single baadhi ya mashine.

Tumeripoti hili tukio ila halishughulikiwa kwa wakati. Mashine zinashindwa kukoboa kwa uzembe.

Cc: TANESCO
 
Nipo tabata old dampo magerage
Siku ya j, mosi kulitokea shoti kwenye nguzo kukapelekea waya za umeme kudondoka, raia wapita njia wakapiga sim Tanesco wilaya ya ilala ( tabata liwiti
Mafundi wa Tanesco wakaja wakapanda juu ya nguzo wakakata umeme wakaondoka zao moja kwa moja mbaka leo
Mimi na wenzangu kama wanne hivi tumekosa huduma ya umeme tangia j, mosi shughuli za kiuchumi zimesimama

Tumetoa taarifa jana asubuhi Tanesco tabata liwiti mbaka mida hii leo naongea hapa kimya hakuna kinachoendelea

Sasa nataka kujua shida ni nini?
Au kuna mipango hapa inatengenezwa ili sisi tutoe rushwa ndio tupate huduma ambayo ni haki yetu kama wateja wa Tanesco
Tanesco makao makuu ebu naomba mtusaidie katika ili shida hiko wapi?
Waya hakuna, mafundi hakuna au wanataka rushwa ndio waturudishie umeme mimi sielewi kabisa ukimya huu unatokea wapi
 
Kwanini mtwara vijijini kila siku saa Moja laxima umeme ukatike? Je Ni matatizo ya kiufundi na km Ni matatizo ya kiufundi kwann Ni muda unaofanana?
 
Naomba kufahamu ni hatua gani zinafuata ili wananchi wa eneo lenye zaidi ya km 1.5 la mraba wanapohitaji huduma ya umeme kwa pamoja namaanisha eneo litakalohotaji nguzo zaidi ya 20, maana kuna mtaa upo manispaa ya songea unaitwa mkuzo-maliasili ni mwaka wa tatu sasa watu hawaletewi umeme... !?? Tunashindwa kuelewa mnafeli wapi Taneso au kila mtu napaswa kununua nguzo yake!?? Pia kuna baadhi ya watu wameamua kulipa kabisa hadi pesa za nguzo zao huko ili zoezi liharakishwe lakini hakuna kitu mpaka leo !?? Mnafeli wapi wakuu??

Naomba kujua utaratibu gani hapo unatumika hapo.. Na wanatakiwa wafanye nini hapo ili huduma iharakishwe??!.
Halafu wanasema umeme umezidi watumiaji Wachache. Tanesco wana Vichekesho Sana. Huko Songea Kuna maombi mengi sana ya watu kuunganishiwa umeme lakini mizinguo ni mingi. Nilishangaa sana kuona taarifa ile Kuwa umeme umejaa umekosa watumiaji.
 
Tanesco gongolamboto ni kero hawafanyi kazi wakipigiwa simu hawapokei ukitoa taarifa ya tatizo katik eneo hawafiki kwa wakati au hawfiki kabisa tunaomba uongozi tanesco makao makuu mchunguze tatizo liko wapi imekuwa ni kero kubwa muda mrefu
Tanesco meter yangu inaanzia namba 43 ina remote jana umeme uliisha tukanunua tukaeka lakini shida meter haiiingizi umeme ndan

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanesco, BIHARAMULO, Nyakahura! Leo hatuna umeme siku ya Tatu na hatuna Maelezo! Tunaomba kurejeshewa huduma hii muhimu ktk uchumi wa taifa letu!

Tambue huku Kuna Mzani wa serikali, so endapo hakutakuwa na umeme kwa muda mrefu kutasababisha magari ambayo yanatumia barabara hii kwenda Rwanda, Burundi etc kuzidisha mizigo na kuharibu barabara zetu zaidi Kwan magari makubwa hayatapima Uzito

#CCM hoyeee

Maendeleo hayana vyama!
 
Tumepokea taarifa kwa hatua zaidi
 
Tanesco wilaya ya ilala wanatufanyia uhuni
Tumeripoti toka j, mosi waya za umeme zimekatika ofisi kwangu,wakaja mara ya kwanza wakakata waya zote wakazikunja wakaondoka zao,
Tukaenda tena j, tatu kulalamika vipi mbona mmeenda jumla wakaja wakachungulia chungulia wakatoa sababu kuna miti inatakiwa ikatwe, tukakata miti yote haya sasa njooni wakaja jana jioni wakazuga zuga wakaondoka
Ni kama vile watu wanaotengeneza mazingira ya kutaka rushwa ndio waturudishie umeme, tunaona kabisa mazingira yanatengenezwa hivi ya kutukwamisha tusipate umeme bila rushwa..
 
Eneo gani na namba yako ya simu tafadhali
 
Back
Top Bottom