TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Kama mh waziri upo humu au kuna wa kukufikishia ujumbe fanyia kazi hii changamoto,
Majuzi tulikua na shoti kubwa maeneo ya mwenge hiyo shoti ongeweza kusababisja kifo kwani nyumba karibia 6 hazikua na umeme nyaya zilianguka hadi chini tukapiga simu watu mbalimbali kwa mda tofauti wakachukua saa 24 hadi kuja tena kwa kusumbiliwa sana sasa je watu wangedhurika ingekuaje?
Yale magari mengi ya dharura yanafanya kazi gani au ni dharau za hawa watendaji?
Mbona huduma tunalipia ila tunapata huduma mbovu?
Na hii sio mara ya kwanza ni mara nyingi tu sijui na maeneo mengine wanafanyaga hivyo au?
 
Hapana maana Tanesco. Wanakata umeme mitaa ya ndani ndani ili isijulikane, ukiwa unatokea barabarani utakuta umeme. Wakati vichochironi Giza
 
TANESCO MBAGALA; wakazi wa mbagala tunapata shida sana kwa huduma ya UMEME kuanzia charambe kuelekea chamazi. Huwa unakatika katika na bila taarifa ya makato hayo ya umeme kutoka kwenu na ukirudi huwa unakuwa hauna nguvu mara unaongezeka nguvu na mwishowe unakatika teena. Tujulisheni nini tatizo maana kwa hali hii mali zetu zinakuwa hatatirini kuungua na kupote. #TUSAIDIENI TUNAPATA SHIDA SANA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanesco kwanini mmeweka madawati ya dharura simu zinapigwa hazipokelewi zikipokelewa watu wa dharura hawafiki eneo la tukio watz tunateseka sana

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Alimpa nani hiyo rushwa? Kwanini hakutoa taarifa? Tusijenge mazingira ya muzusha mambo badala yake tusaidie kuwabainish mnaona wanaomba rushwa sio kuchafua shirika zima tena kwa taarifa zakusikia

Sent using Jamii Forums mobile app

Achana na mimi endeleeni na rushwa zenu. Tangu siku ile nilipopost hapa nilipatwa na hasira sana. Nikalifanyia kazi na ndani ya siku mbili niliingiza umeme kwangu baada ya kutafuta 50,000. Usalama wa familia yangu ni muhimu kuliko upuuzi wenu. Nikae nasubiria taratibu ambazo kwa makusudi huduma inacheleweshwa. Nyumba inakaa giza usiku mtu anapishana na nyoka huku unaambiwa fuata sheria unakaa miezi miwili mitatu. Nonsense. Unakomalia nitaje jina hapa au niweke namba za simu ili iweje? Mnajifanya hamjui siyo? Ina maana nchi hii hakuna inteligence ndani ya shirika nyeti kama Tanesco kugundua uzembe na rushwa za wazi wazi kama hizi? Kuanzia mameneja hadi maengineer wote nonsense.

Hainisumbui akili kwa sababu wote tuko tunapikia jiko moja na sufuria moja. kwa taarifa yenu tangu nitoe hizo 50,000 nimeshapiga zaidi ya laki 2 kufidia pengo. Samaki hukaangwa kwa mafuta yake usijali sana. Tunajenga Tanzania ya viwanda, maendeleo hayana chama.

1061899
 
Hili mnaloliona hapa ni eneo la kimara kingongo kwa muheshimiwa au uwanjani dar es salaam nyaya za umeme zimeburuzika mpaka zimewekwa kwenye ukuta wa fensi ya mtu kuelekea nyumba husika na pia imegongelewa misumari kwa kushikiziwa na kamba na mwenye nyumba sidhani kama abafahamu kama kuna kitu kama hicho kin3fanyika maana ni hatari sana wamedanya hapo na hapa wamejaribu kuwatafuta bila mafanikio nakipindi hiki cha mvua mnadhani kikitokea kitu chochote hapo si hatari kwa watu wakaribu hapo pia kwa mwenye nyuma fanyeni haraka kutatua hili jambo kabla mambo makubwa hayajatokea kipindi hiki cha mvua isitoshe nguzo imeinama kabisa TANESCO
20190403_152637.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanesco kwanini mmeweka madawati ya dharura simu zinapigwa hazipokelewi zikipokelewa watu wa dharura hawafiki eneo la tukio watz tunateseka sana

Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu wakati mwingine wanafika eneo la tukio wanaliona tatizo ila wanasema kwamba hii nyumba hatuwezi kuirekebishia umeme kwa sababu mama mwenye nyumba huwa anasumbua sasa sijui huwa anasumbuaje...!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili la kupiga simu hazipokelewi linauma sana, alafu unatoa taarifa hapa unaulizwa namba ya taarifa na namba ya simu,wakati simu hazipokelewi.
Nyumbani kwangu na nyumba kadhaa za jirani na kituo cha watoto yatima Msongola hakuna umeme karibu siku ya 8 leo, taarifa inatolewa lakini hakuna huduma yoyote. Inauma sana, yaani ni kama vile sisi si binadam.
Inakera na inatia hasira. Shirika linalalamikiwa kila siku lkn huoni mabadiliko ya kiutendaji, as if watu wote ni corrupt na kutoa huduma kwa wananchi sio jukumu lao.
Turudishieni umeme Msongola Yatima, hamuoni hata kuwa dhambi kituo cha watoto yatima kukaa giza kwa siku zote hizo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangu nimeanza ishi wilaya ya Namtumbo iliyopo Ruvuma sijawahi sikia tangazo la kukata umeme. Ila cha ajabu wao mda wote wanakata. Mf; mda huu umeme haupo na kuanzia saa moja na nusu hadi saa mbili dak 15 wamekata mara saba(7). Kuna jirani yangu hapa kuunguza flati yake mpya tu na analalama sana. Nashindwa kuelewa umeme ndani ya dakika 1 wanakata mara 3 sasa marekebisho gani hayo? Any way labda mnatumia supersonic speed kutengeneza. Na vinguzo vya kutoa umeme toka Songea,vyembambaaa juu likitanda wingu tu vinaanguka. Mnashindana na king'amuzi cha azamu upepo tu wao wamekata na nyie mnakata,sujajua ofisi moja au laa. Matengenezo kila siku mnakela. Na ratiba ya kila juma mosi umeme hakuna mnamaanisha nn? Juma mosi umeme lazima mkate na jpili hadi ijumaa anytime mnakata kwa siku mara tatu hadi 5. Jamani mnakera sana.
 
Ni eneo gani na namba yako ya simu tafadhali tukuunge whatsApp ya Songea upate taarifa kamili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
86 Reactions
Reply
Back
Top Bottom