TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Mnakera sana wananchi jinsi mnavyotukatia umeme!
Kwanini mnatufanyia hivyo lakini?
Mnatukwaza sana!
 
Kero ya umeme naona imeshakuwa dondandugu!
Vyombo vya Habari na mitandao ya jamii pazeni sauti Mheshimiwa Rais na Waziri mkuu wajue jinsi Tanesco wanavyo tukosesha haki yetu ya kupata huduma ya umeme wakati wote!
Tena ngoja nikitulia nianzishe Uzi !
Yani naona mnatafuta kutumbuliwa!
 
Kero ya umeme naona imeshakuwa dondandugu!
Vyombo vya Habari na mitandao ya jamii pazeni sauti Mheshimiwa Rais na Waziri mkuu wajue jinsi Tanesco wanavyo tukosesha haki yetu ya kupata huduma ya umeme wakati wote!
Tena ngoja nikitulia nianzishe Uzi !
Yani naona mnatafuta kutumbuliwa!
Kiongoz.hakuna shirika la ki.sen.ge lilibak kama hili..utafkiri umeme tunapewa bure

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiongoz.hakuna shirika la ki.sen.ge lilibak kama hili..utafkiri umeme tunapewa bure

Sent using Jamii Forums mobile app

Eti jamani?!
Yani wanaona Kama ni hisani yao tu sisi kupata umeme Kumbe ni haki yetu kabisa kupata huduma ya umeme Kama zilivyo huduma huduma nyingine za msingi!
Umeme wa kukatika katika hivyo halafu majukwaani mnaimba kuelekea nchi ya uchumi wa kati kwa umeme upi?
 
TANESCO.

Je mna online service kwa huduma zifuatazo.
1. Kujua salio la unit zako ukiwa mbali na meter
2. Kuangalia mara ya kuongeza unit katika meter.

Nawasilisha
 
Habari naomba kuuliza kwenye tariff zero inatakiwa niweke shilingi ngap ili kupata units 75? mana huwa nanunua umeme wa 9000 na napata units 73 vipi kuhusu hzo 2 zilizobak?


Sent using iPhone XS Max
 
Heri ya mwaka mpya Tanesco, mwaka umepinduka tena hatimaye tuko ndani ya 2019 chonde chonde, kilio changu ni kwenye kitongoji cha KIJUKA kilichoko katika kijiji cha MABUYE wilaya ya MISSENYI mkoani KAGERA . Nawakumbusha tena juu ya suala LA kukosa umeme wa REA tafadhali sana naowaomba kitongoji hiki mkisaidie kwani kimebaki katikati kama kisiwa na kina kila sifa ya kupata umeme wa REA na hakijapata. Japo nimekuwa nikieleza suala hili hapa mara kwa mara na kuhaidiwa kuwa linashughulikiwa ila bado sijapata ufumbuzi wa hili suala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeme huku maeneo ya kimara ni wa kukatika katika mpaka kero sasa yaani unaweza katika mara 3 mpaka 4 kwa siku nzima alafu ikifika usiku ndo mnakata kabisa mpaka asubuhi mfano kama leo tangu saa 8 usiku hatuna umeme.Nahitaji ufafanuzi please

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni mteja mpya, nimekamilisha taratibu zote za awali. Sasa nikaambiwa nisubiri surveyor, karibu mwezi hajafika. Nimeenda kuulizia nikajibiwa subiri tu atakuja.

Naomba kuuliza, ni muda gani natakiwa nisubiri surveyor? Au naweza subiri hata zaid ya mwaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanesco lini wananchi wa mtaa Igombe B ulioko Ilemela MC Kata ya Bugogwa watafikiwa na Huduma ya Umeme ,kwani mtaa huu una wakazi zaidi ya 1400 kaya,Bahati mbaya Umeme Rea iliopita kaya zilizofikiwa na Huduma ya Umeme Ni asilimia 0.1%

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TANESCO Mimi nipo Dar es Salaam, Kimara, Korogwe karibu na baa maarufu hapa Korogwe iitwayo miti mitatu, au karibu na msikiti. Namba ya simu 0764086420.

Kwanza nasikitika sana kwa huduma mbovu niliyopata baada ya kupiga simu kwenu (Mbezi). Nilipokelewa simu na muhudumu wa kwanza nikaambiwa mafundi wanakuja japo nilinyimwa namba ya taarifa. nilisubiri siku nzima hawakuja. Nikapiga kesho yake ambayo ni jana kilichotokea ni kwamba nilipopiga namba ya airtel muhudumu akanipokea na kunipatia majibu ya ajabu sana na kunikatia simu. Nikarudia kupiga tena kama mara sita kila nikipiga muhudumu yule wa kiume anakata simu. nikaamua kubadili na kupiga namba ya tigo akapokea na pale alipogundua kuwa ni mimi akakata simu nikajaribu kupiga tena akawa anakata. kwakweli nilisikitika sana ikabidi tulale giza tu.

Tatizo nilionalo ni kwamba ni takiribani wiki moja sasa mara kwa mara kwangu umeme unakatika wakati majirani ambao tunashare nao laini moja ya umeme wanakuwa na umeme. Mpaka sasa ninapoandika sina umeme wakati jirani yangu ana umeme na wote tumechukulia kwenye nguzo moja. Hili tatizo limenisumbua sana. Naombeni mtume mafundi wenu waje kunisaidia. Pia boresheni huduma zenu za simu, tunapopiga simu kwenu tunatarajia kupata huduma na sio kuambulia matusi na huduma mbovu.
 
86 Reactions
Reply
Back
Top Bottom