TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Hii namba ya Tanesco Tanga au ya wongo, nimepiga kapokea mtu kabla ya kumuuliza chochote akaniambia umekosea namba na akakata simu!
Screenshot_20181204-194347_Simpler.jpeg
 
TANESCO, kwani kuna tatizo gani mbona umeme unakuwa haueleweki? Hauna nguvu hamuoni kama mnatuharibia vitu? Karibia mwezi sasa shida nini jaman!
 
Naomba kufahamu utaratibu, nimejenga umbali wa kama mita 900 toka ilipo nguzo ya mwisho. Gharama kwa mazingira kama haya inakuwaje? Au natakiwa kufuata utaratibu upi ili kufikisha Umeme site?
 
TANESCO Kurasini unakaribia mwezi sasa baada ya kufanya malipo stahiki ambayo nilitakiwa kulipa ili nirudishiwe umeme.
Niliambiwa ningefungiwa mita ndani ya siku saba za kazi lakini hadi Leo zii.Kila ninapofuatilia napigwa danadana,Mara tutakuja kesho,Mara tutakuja ijumaa,nk kifupi hali ndio hiyo.Tatizo ni mini hasa ? Hakuna mita za LUKU si mniambie!na kama mita hakuna ni lini zitapatikana?maana kiukweli hadi nawachumia dhambi labda mnataka mlungula ndio mkaniwekee hiyo mita??!!
Nitashukuru nikijibiwa /nikipatiwa ufumbuzi wa tatizo langu.
 
TUNAOMBA KUBADILISHIWA TARIFF KUTOKA tarif 1 kwenda tarif 4.

Umeme uliunganishwa toka mwezi wa 8 mwaka huu tukapewa Unit 50 na tukazilipia. Mpaka leo bado tunaendelea kutumia but zinakaribia kuisha.

Bila shaka tutakuwa na vigezo vya kuwa tarif 4.

MKOA: Mbeya

WILAYA: Mbeya Jiji

SIMU: 0653 137 501

METER NUMBER: 54 183 469 912

Aidha kama kuna Group la WhatsApp Namba hiyo iunganishwe
 
Salama wakuu
Kuna tatizo la umeme kukatika mara kwa mara kijiji cha Embaseni,Usa River,Arumeru Arusha.Tatizo limekuwa sugu.Tunaomba wahusika mshughulikie.Tumeanzisha viwanda vidogo bila umeme sidhani kama agizo la Muheshimiwa raisi kuanzisha viwanda kwa mtindo huu litafanikiwa.Tunaomba wahusika mshughulikie haraka.Hata sasa ninavyoandika hakuna umeme.
 
Tanesco nguzo iliyopo jirani nami ni mita 60 Hapo natakiwa kuvuta nguzo au nafanyaje ili umeme uingie ndani? thanks
 
Yani leo kutwa nzima Mwenge tumeshinda bila umeme,kwa mwendo huu Tanzania ya viwanda itabaki kwenye makaratasi tu
 
86 Reactions
Reply
Back
Top Bottom