TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Mgao wa umeme naona ratiba imebadilika? Tabata dampo juzi umeme umekatwa ,jana umeme umekatwa na leo umeme umekatwa
Sasa ile ratiba ya j,nne na j,tano haipo tena sasa imeletwa nyingine mbaka leo alhamisi umeme hakuna tena
Toeni taarifa rasmi wananchi tujue mgao huu mpya unakwenda mbaka lini?
 
Kwa jina naitwa ABBASY KAPERA Mimi naishi Mkoa wa tanga WILAYA ya Korogwe kata ya Kilole mtaa wa mikoroshini ombi langu kwenu kutuletea umeme watu yupo wengi tunaohitaji umeme kwanini msitulelee kama mradi ili wananchi tupate umeme na nyinyi mpate mapato Kwa maana Mimi peke yangu nguzo zaidi ya tano ni gharama kubwa sana ukilinganisha na kipato changu alafu mtu ukivuta wengine wanavuta kiulaini kwann sasa msilete kama mradi au nini kifanyike tuletewe kama mradiView attachment 940735
Kaka hutajibiwa n'go , watakaojibiwa na kuhudumiwa ni wale wenye fedha zao na mamlaka mbalimbali serikalin. We kaa ukisubiri.
 
Naomba kueleweshwa; Nyumba yangu ipo umbali wa nguzo tatu kutoka kwenye line ya umeme. Nikitaka kuingiza umeme nyumbani kwangu, ni nani anayepaswa kugharimia nguzo kati ya mimi na TANESCO?
 
Nimeharibikiwa na mita ya Luku Sikh ya 3 Leo nafatilia Tanesco mpk sasa hawajaja kuibadilisha na kwa mujibu wa kitengo chao cha Technical support Mikocheni wanadai mita za Luku zimeisha na hawajui lini zitapatikana. Naomba tupewe utaratibu tufanyaje kuliko kutulaza gizani Sikh ya 3 .
 
Tanesko wanafanya kazi vile wanavyotaka wao.sio wewe.na hakuna anaeweza kuwapangia chochote,yaani kama wako sayari nyingine.
 
Sasa huu uongo wao hivi utaisha lin?Mbona wanatuonyesha kila siku itv kuna kiwanda cha mita hapa tz.
Mi mwenzenu nimewachoka hawa watu basi tu yani
 
Tanesco Kigamboni, WARASIMU naomba mnirudishie hela yangu nikanunue solar hamtaki kuniunganishia umeme. Tanesco Makao Makuu mme kaa kimya naona mshirikiana na tawi lenu Tanesco hamtaki kunihudumia.
 
Tanesco Kigamboni, WARASIMU naomba mnirudishie hela yangu nikanunue solar hamtaki kuniunganishia umeme. Tanesco Makao Makuu mme kaa kimya naona mshirikiana na tawi lenu Tanesco hamtaki kunihudumia.
Umelipa kwa jina gani?tarehe na eneo gani tafadhali
 
Nimeharibikiwa na mita ya Luku Sikh ya 3 Leo nafatilia Tanesco mpk sasa hawajaja kuibadilisha na kwa mujibu wa kitengo chao cha Technical support Mikocheni wanadai mita za Luku zimeisha na hawajui lini zitapatikana. Naomba tupewe utaratibu tufanyaje kuliko kutulaza gizani Sikh ya 3 .
Jina

Namba ya simu

Namba ya taarifa tafadhali
 
Nilipata token zangu , kumbe ni swala tu la network . Nashauri tu usisubiri mpaka luku ifike zero kwani network inaweza kusumbua kwa mda ukiwa kwenye giza tororo
 
Umelipa kwa jina gani?tarehe na eneo gani tafadhali
Nilishataja jina,eneo ninalo ishi , mpaka namba yangu ya simu nimetoa humuhumu JF lakin sijapata huduma yeyote ni takriban miezi 4 Sasa utafikiri ninapewa huduma bure. Nimefunga mkanda na familia yangu kutafuta hicho kiasi, ili nipate huduma ya kuunganishiwa umeme kwa wakati lkn wapi. Tanesco Kigamboni ni tatizo sana, mbona mikoa mingine hawafanyi hivyo. Tanesco Makao Makuu inaelekea mnalifumbia macho au mnashirikiana nao kutenda maovu wanayofanya. Maana hakuna utatuzi.
 
TANESCO naombeni maelezo kwenye hili swala la tariffs mfano kuna mtu anatumia umeme mkubwa but still yupo tarrif 4 ila mm nina nyumba ina room 3 situmii fridge wala jiko la umeme but nimejikuta nimehamishwa kweny tarrif 1 ukizingatia kwa mwezi matumiz yangu ya umeme nimadogo mno
Tanesco nasubiri feedback ya hili swala
 
86 Reactions
Reply
Back
Top Bottom