Mimi ni mteja nilikuwa nafanya marekebisho ya nyumba yangu
nikahama nyumba miezi sita na sikutumia UMEME miezi hiyo na mita ikasimama nilikuwa nalipia meter charges kama kawaida katika marekebisho ya jengo niliwàomba tanesco wanibadilishie mita wàniwekee mita ya luku nikafàñikiwa kupata mita hiyo ña Ofa ya units za kuanzia ambazo nilitumia miezi sita Leo mwaka 2018 tañesco wamenikadiria deni la mita ile ya zamani na units za Ofa wananicharge kila ninunuapo units za luku kama deni Nina masikitiko sana kwa utendaji huu usiokuwa na kumbukumbu za wateja
 
Hizo units walizokupa nadhani ni 50 ambazo kila mteja mpya wa LUKU hupewa na thamani yake kwa tariff 1 sio zaidi ya 18,000/= waulize deni lako ni kiasi gani ili ujue na sio kukutwa kila ununuapo umeme.
 
Naomba kuuliza
1) kilometa moja inachukuwa nguzo ngapi za Tanesco (nguzo kubwa)?
2)je, nguzo moja kwa kijijini inauzwa shilingi ngapi?
3)kilometa moja inachukua nguzo ngapi za Tanesco (nguzo ndogo)
4)je nguzo moja ndogo(ya Tanesco) kwa kijijini inauzwa shilingi ngapi?
 
Naomba kuuliza
1) kilometa moja inachukuwa nguzo ngapi za Tanesco (nguzo kubwa)?
2)je, nguzo moja kwa kijijini inauzwa shilingi ngapi?
3)kilometa moja inachukua nguzo ngapi za Tanesco (nguzo ndogo)
4)je nguzo moja ndogo(ya Tanesco) kwa kijijini inauzwa shilingi ngapi?
Wakikujibu jibu zuri nakutumia vocha ya 5000
 
Moja ya shirika la kipuuzi kuwahi kutokea hapa duniani ni Tanesco, Tumewachoka huku kigamboni matengenezo gani kila siku ndani ya mwaka mzima, hivi Magufuli maoni ya huku hayaoni kama mengine, ngoja tutafute njia nyingine ya kumfikishia haya malalamiko, wanaorudisha maendeleo wa kwanza kwa hapa Tanzania ni Tanesco.
 
Mimi nimteja mpya nimeunganishiwa umeme.Nilipounganishiwa nilipewa unit 10,nimetumia zimebaki 2 sasa nimeenda ofisi ya TANESKO iringa na sh 10000 ili nilipe deni na kununua unit.Nimetoa 10000 naambiwa haitoshi nilipe 18000 nnapojaribu kuuliza naambiwa niandike barua ya kudai unit 40.Anaeujua huu utaratibu ebu anijuze? maana nimelipia ambacho sijakitumia.
 
Leo ni siku ya 77 tangu nilipie pale Kibaha bado sijaunganishiwa umeme. Tanesco say something. Ikumbukwe waziri mwezi April alisema wale wote waliokwisha kulipia lazima.....lazima waunganishiwe kabla ya 30 days. Sada Tanesco na waziri nani mkubwa ??
 
Mimi ninaomba kufahamishwa kama kweli shirika letu lina uhaba wa nguzo kwa wateja wapya. Maana ninamiezi 4 sasa naambiwa hawana nguzo pamoja na kuelekezwa nilipie gharama za kuingiza umeme. Pia nikapewa surveyor akaja kukagua mfumo wa umeme na kusema sawa na kunielekeza kwamba inatakiwa nguzo 1 tu hivyo nilipie kama nilivyoelekezwa wakati najawa form lakini mpaka naandika hapa naona tatizo sasa ni kuambiwa hawana nguzo. Mm ni mkazi wa Dar.
 
TANESCO Kigamboni nzima hamna umeme. Umeme umekatika muda wa saa moja jioni. Hii ni coincidence au mmeamua kwa makusudi tusiangalie Champions League Final? Kuna kitu kililkuwa kinaniambia leo umeme utakatika muda wa mpira au kabla.
 
TANESCO, kuna tatizo gani mbona mnakata sana umeme huku kibangu? Ni umeme wa mgao au? Kwa nini hamtoi taarifa ya kukata umeme?
 
Tanesco moshi angalieni emergency crew yenu inawatia aibu sana,haiwezekani jirani yangu ametoa ripoti ya hitilafu ya umeme toka jumatatu hadi Leo hakuna response yeyote,report number 3791 inasikitisha sana!
 
Wako
Tanesco moshi angalieni emergency crew yenu inawatia aibu sana,haiwezekani jirani yangu ametoa ripoti ya hitilafu ya umeme toka jumatatu hadi Leo hakuna response yeyote,report number 3791 inasikitisha sana!
Lunch mpaka jumatatu
 
Ni siku tano sasa umeme mdogo, u unapungua nakuongezeka kila dakika,radio,tv,frij na kadhalika vimeungua,tumepiga simu tumewaeleza lakini hamjali ,hivi tumewakosea nini sisi watu wa Nguzo, Msingwa? Kama vipi zima tu umeme wenu tuwashe vibaya.Inashangaza,unapiga simu mnapokea halafu mnaongea kama vile hakuna tatizo.Tanesco Mbezi nyambafu na Fumbafu thana nmeniboa sana .
 
Siku nyingine ukiona umeme unapungua na kuongezeka usisubiri mpaka uharibu hivyo vifaa vyako! Ungevizima mpaka umeme utakaporudi katika hali yake yakawaida.
 
Back
Top Bottom